Mdau akijinafasi na kilaji cha Ndovu, akisema kwamba toka kilaji cha Ndovu kije kwa muonekano mpya na maridadi pengine kuliko vilaji vyote nchini, kimepanda chati ya ajabu na kuwashangaza hata TBL wenyewe. Yaani ukikaa kiti kirefu bila ndovu inakuwa....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kweli kabisa Michuzi. Hiki kitu ni balaa tupu. Tokea siku ya kwanza nilipokionja bahati mbaya (nilikuwa sijui kama imebadilishwa na bia yangu favorite zilikuwa za moto), sijaweza kuiacha. Halafu asubuhi unaamka freshi kama ulikuwa unakunywa maji. TBL hapo nimewakubali.....

    ReplyDelete
  2. shida tuna kaugonjwa na chupa za kijani kwa taarifa hata safari ukiitia humo utaona shughuli yake maana hata wanywa sprite wameiingia humo,mwasimba,tandika

    ReplyDelete
  3. We are taking so much pride in destroying our nation.

    ReplyDelete
  4. huyu ni rama majungu bwan michuzi?

    ReplyDelete
  5. Haaa kweli hii bia tamu mana huyu kaka mtaalam sana wa kinywaji jamani Ndovu (TBL) mpeni deal kaka huyu kauza kweli hata mie leo nitaanza kunywa hichi kinjwaji, kaka wa nguvu handsome haswaaaa duuuuh kudadeki

    ReplyDelete
  6. ASHA MADINDAOctober 20, 2009

    MICHUZI HIVI NA WEWE UNAPENDA BIA? BASI NAULIZA TU

    ReplyDelete
  7. Siamini Ustaazi unapigia debe kilevi namna hii!!!hii globu ya jamii debe za vilevi vingekaa kando kidogo una - deal na watu wa namna mbalimbali!

    ReplyDelete
  8. Huyu ni Ramadhan Majungu? kaka yake moshi majungu au? namkumbuka wa Kinondoni Mwenzangu!!!!

    ReplyDelete
  9. Watanzania hicho ndicho tunachojua kazi kushangilia matoleo mapya ya pombe but mambo muhimu yanayotokea nchini kwetu haaa, duh sijui tutakuwa namna hii mpaka lini yaani tanzania ndio nchi kama sikosei pekee duniani viongozi wake wana relax kupita kiasi maana asilimia 99 ya watanzania ni MAZOMBI(WATU WASIOJUA NINI KINAENDELEA) maana kuna mambo ambayo yanaendelea nchini kwetu but watanzania haha kama hatuoni vile 1)Angalia mikataba ya madini 2)Angalia mgao wa umeme 3)angalia EPA 4) Angalia DOWANS na mjomba wake RICHMOND lakini cha kushangaza sijawahi kusikia umma wa watanzania wameonyesha kutokuridhika na mambo haya angalau hata kuandamana tu tena kwa amani TANZANIA TANZANIA TUAMKE JAMANI ni wakati wa kukaa na kutafakari mustakabali wa taifa letu jamani watanzania tumezubaa sana thats y kila mtu anafanya analotaka embu angalia hata RWANDA tu jamani hii mpaka lini?

    ReplyDelete
  10. watu wenbgine bana wao kulalama tu kama hutaki habari za hapa kasome kwengine nani kakulazimisha . kazi na Dawa bana wewe kama unashida zako huna uwezo wa kula green bottle u must go to he... sio unatutolea mimacho tu sie watu wa kilaji na biashara zetu tunapata wateja wapya humohumo na marafiki pia kwahio baaabu kubwa kilevi juuu

    ReplyDelete
  11. Watanzania tunapenda sana show off zisizokuwa za maana,kwa hiyo wakiweka kwenye chupa za PINK are we still going to say hata ukiamka asubuhi ni kaa ulikunywa maji jana yake...wake up people,we don't just jump when watani wetu wakisema ruka...damn it...nikipewa urais mimi sijui,maana yake nina Reformation Plan for ulimbukeni wa wabongo,shida zimetujaa kaa nini lakini aah raha tu ndo the order of the day.

    ReplyDelete
  12. wewe acha ubwege wewe biashara gani unafanya ukiwa umezungukwa na watu hata kifingua kinywa hakijui, hata nauli ya kumpeleka mtoto wake shule kesho hana, acha ujinga wewe now sio wakati wa kujifanya unapapa hizo green bottle sijui now ni wakati mwa watanzania wote kushikamana na kujaribu kupunguza haya matatizo yalioyotuzunguka sio kujifanya unafanya starehe tanzania kuna starehe? usiangalie hapo dar angalia kule liwale lindi kwa bibi zako angalia kule mpanda kwa mjomba wako ndio ujue kama una starehe au vp tutatue matatizo ya msingi kwanza yaliotuzunguka then ndio utafanya hizo unazozita biashara zako vizuri sasa wewe umezungukwa na mtanzania ambaye hata mlo mmoja kupata tabu utafanya biashara gani hapo we bwege?Tuamke jamani tukumbushane ,tuelimishane na pia tukosoane ndio tutaweza kulijenga hilo taifa letu
    hicho kidogo tulichonacho nchini tukikitumia vyema na usimamizi ulio bora na wenye ufanisi tanzania angalau tunaweza kupiga hatua kidogo tuna madini tuna ardhi ya kutosha TUAMKE JAMANI

    ReplyDelete
  13. wewe anony hapo juu, ni kweli hii blog ya jamii na ina deal na watu mbali mbali lakini kumbuka hao watu mbali mbali ni pamoja na WALEVI NA WANYWAJI wanaotumia hicho kilaji hapo....

    ReplyDelete
  14. I'm dropping Nyumbani next week. nikifika tu first thing is wapi ndovu? hebu lete bariiiidi, huku macho yakikodolea jikoni tayari kwa ku-order nyama choma.

    ReplyDelete
  15. Huyu Bwana siyo Ramadhani Majungu Kaka wa Moshi Majungu mchezaji wa zamani wa yanga??
    Mdau, USA

    ReplyDelete
  16. jamani tutawaza na kudiscuss RICHMOND NA EPA kila dakika na wakati?kwa hiyo kama nchi ina matatizo hatuna muda wa kujirefresh?hata mfiwa hufarijiwa ili kupoteza mawazo na kujipanga upya na maisha yake,kwani kunywa pombe kwa muda muafaka na kwa kipimo ni kosa......hv Mtanzania akifanya kazi yake kwa wiki nzima then akatenga muda wake wa kupumzika ni kosa?kisa nchi inamatatizo?
    blog ya jamii ndio hilo halina ubishi na ni kwenye jamii hii tunayoishi bia na pombe mbalimbali hupatikana sasa nini cha ajabu....au ulitaka mithupu atoe picha za vinywaji vyajamii ya Mwezini au juani?
    mi nadhan hapa suala ni kunywa pombe kwa kiasi na kwa wakati muafaka,kila mtu na starehe yake cha kukumbuka ni kwamba starehe zina mipaka ili zisiwe karaha kwa mwingine.

    ReplyDelete
  17. NINAPENDA KUTOA SHUKURANI KWA BLOG NA WADAU KUWEZA KUTUTANGAZIA BURE KINYWAJI CHETU KITU AMBACHO KIMETUPUNGUZIA GHARAMA.
    ASANTENI ENDELEENI KUNYWA PIA MSIWANYIME WATOTO WENU KINYWAJI HIKI.

    ReplyDelete
  18. ndiyo kabisa huyo ni ramadhani majungu aankoo nakuona tulikuwa wote kinondoni morroco enzi zilee

    ReplyDelete
  19. STAREHE SIO KITU KIBAYA. KILA MTU ANAHITAJI KUSTAREHEKA. LAKINI KITU CHA MSINGI NI KWAMBA WATANZANIA WENGI WAIENDEKEZA SANA STAREHE ZA KUNYWA POMBE NA NYINGINEZO. WATANZANIA FANYINI KAZI KWA BIDII ZAIDI KWANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. STAREHE HASITATUSAIDI SANA.

    HATA KUNA WIMBO UNASEMA ZIDISHA JUU KATIKA KUFANYA KAZI.

    ULIMBUKENI WA KUVAA MICHUMA SHINGONI NA MIWANI AMBAZO HAZIJIDHITISHWA KWA AFYA YA MACHO NA KUKUMBATIA CHUPA ZA BIA UMEPITWA NA WAKATI.

    HATA MKIPINGA KAZI NI KITU MUHIMU KULIKO STAREHE.

    KINYUME NA HAPO TUTAISHIA KUWA WEZI, MATAPELI NA MAFISADI. NA HATIMA YA HAYA MAMBO INAJULIKANA.

    ReplyDelete
  20. afu baada ya kunywa hii na nyama choma,,,kwishney kabisaaa afya zero na ivi hamfanyagi mazoezi?magonjwa kutwa kucha....nyoooo
    mtajutaa,mtakomaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...