Kaka Issa,
Leo nimejaribu sana ku google nyimbo za kizalendo lakini hazipatikani. nikaamua kuziandika kutoka katika daftari la mwanangu wa shule. Naomba uwawekee wadau wanaoipenda nchi hii ili waweze kujikumbusha na kuendelea kuitukuza nchi yetu.
kila la kheri
Mdau wa Globu ya Jamii
SHUKURU MOHAMMED
---------------------------------------------------
TAZAMA RAMANI
Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2
------------------------------------------------------------
TANZANIA NAKUPENDA
Tanzania, Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa...
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama we
Tanzania, Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa,
Nakupenda kwa moyo wote.
Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu
Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi
Mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaa,
Nakupenda kwa moyo wote
Tanzania Tanzania
Watu wengi wanakusifu
Siasa yako na desturi
Ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi
Mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaa,
Nakupenda kwa moyo wote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kweli ulikuwa na muda..! nwyz asante kwa kutukumbusha utotoni! sasa chukua daftari la mwanao usahihishe hii sentensi; "Unilinde name nikulinde hata kufa" I think it should read "Unilinde nami nikulinde mpaka kufa".
    Peace out!
    I LOVE YOU TZ.

    ReplyDelete
  2. Kuipenda Tanzania kwa moyo wote nadhani ilikuwa zamani, siku hizi hakuna vinginevyo, kungekuwa hakuna UFISADI katika Tanzania tuipendayo kwa moyo wote!!!

    ReplyDelete
  3. SIJUI KWA NINI NIMELIA BAADA YA KUSOMA HIZI NYIMBO,LABDA NI KWA VILE NI KWELI NAIPENDA TANZANIA LKN NINAYOYASHUHUDIA TANZANIA SIYAPENDI,IIIIIIGHH.

    ReplyDelete
  4. Nyaisanga, Mwananyamala KisiwaniOctober 17, 2009

    Tuwekee na lile shairi lililoko katika kitabu cha nne cha kiswahili lisemalo;

    KARUDI BABAMMOJA TOKA SAFARI YA MBALI
    KAVIMBA YOTE MAPAJA NA KUTETEMEKA MWILI
    WATOTO WAKE WAKAJA ILI KUMTAKA HALI
    WAKATAKA NA KAULI IWAFAE MAISHANI.

    ReplyDelete
  5. Shukrani! Nani anamusic? Tusaidie please!

    ReplyDelete
  6. ahsante sana uliyetutumia maneno ya nyimbo hizi za kizalendo.
    lakini na wewe anony wa kwanza, kwani lazima uandike?

    ReplyDelete
  7. yaaani imenikumbusha mbali sana, nakumbuka na ule wa bendera ya tanzania ndiyo ya kujivunia, ilianza kupepea mwaka sitini na moja.........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mm pia naupenda sana bendera ya tanzania

      Delete
  8. ah wadau mmenikumbusha mbali sana. haswa huyo aliyeweka "karudi baba mmoja". nakumbuka hadi bibi yangu aliyekuwa na miaka 71 (R.I.P now)alikuwa anaimba karibu beti zote kwa jinsi nilivyokuwa naimba kila siku nikitoka shule.hahaha..kweli tumetoka mbali.

    ReplyDelete
  9. mnakumbuka wimbo wa - Kibanga kampiga mkolonix2tumsifux2,kibanga ni shujaa mkuu..

    ReplyDelete
  10. MAONI BINAFSI
    wimbo wa pili ungefaa kuwa wimbo wa taifa.au ungekuwa wimbo wa ikulu!
    Pia wimbo wa sasa wa taifa ungebakizwa ubeti wa "Mungu ibariki Tanzania"

    ReplyDelete
  11. Ebu tuletee ule"sisiii tutawasha mwenge". asante.

    ReplyDelete
  12. Kabisa kutoka moyoni mwangu naipenda Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...