Flashaback June 20, 2008: Kelly Rowland (shoto) mmoja kati ya wanamuziki waanzilishi wa kundi maarufu la muziki lililojulikana kama Destiny’s Child akimkabidhi Eliza tuzo maalumu ya MTV Staying-Alive kutokana na mchango wake katika kuelimisha vijana kuhusu janga la ukimwi na jinsi ya kujikinga na maradhi hayo nk.
Globu ya Jamii inamrejesha shujaa Eliza wa Uwanja wa Fisi kufuatia hoja mbalimbali za wadau kutaka kujua nini kinaendelea ama amewahi kusaidiwa katika harakati zake za kukomboa wasichana hapo Uwanja wa Fisi baada ya kuonya video hii:http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM
Anko nanihii ndiye aliyekuwa mpiga picha maalumu siku Kelly Rowland alipofika na kusambazwa kila mahali. Habari za karibuni zinasema Eliza anaendelea vyema ingawa misaada ya hali na mali bado inahitajika. Hii ikiwa ni baada ya kurejea kwao Iringa kwa ufadhili wa mradi wa MTV Staying Alive.
Soma stori ya Eliza
na

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Muddy Nice TZOctober 30, 2009

    HI KAKA MITHUPU,
    AISEE UNAJUA KUNA JAMAA MMOJA PINDI TUMETOA MAONI YETU JANA KUHUSU HUYU DADA ELIZA AKAKUOMBA WEWE UTUPATIE MAWASILIANO YAKE EITHER NAMBA YAKE YA SIMU NA MENGINEYO AU HATA UTUJULISHE JINSI YA KUMFIKIA JAPOKUWA NIMEJARIBU KUFUATILIA LINK ULIZOWEKA LKN BADO HAIJASAIDIA KUJUA ANAPATIKANAJE UKO IRINGA. KWAKWELI STORY YA HUYU DADA INASIKITISHA SANA, LKN HAKUNA JINSI NDIO MAISHA YA KISWAHILI YALIVYO, YAANI KUNA WAJINGA FURANI HAPA DAR ES SALAAM WANASIKIA RAHA KUHONGA PESA KWENYE MABENDI ILI WAIMBWE MAJINA YAO LKN SIO KUJARIBU KUWASAIDIA WATOTO WANAOPATA TABU MITAANI.YAANI IT IS VERY PAINFUL, HIVI HAWA VIONGOZI WATAMUELEZA NINI M/MUNGU SIKU AKIWATIA MIKONONI?, KWAKWELI SIKU YA MWISHO KUTAKUWA NA KAZI MNO. ANGALIA VIONGOZI WANAVYOJICHEKESHA OVYO UKU WANANCHI WA KAWAIDA WANAVYOHANGAIKA NA MAISHA, YAANI ELIZA KAOKOTA SHILINGI 200 ANAONA KAMA AMEPATA MILIONI NA ANAIPIGIA BAJETI YA VIAZI VYA SHILINGI 100 NA ILIYOBAKI ANAINGILIA KWENYE JUMBA LA VIDEO UKO USWAHILINI, HIVI WATANZANIA TUJIULIZE, JE WATANZANIA WANGAPI WANAOCHEZEA MPAKA SHILINGI ELFO MMOJA KWA SIKU, HIVI SISI KWANINI TUNAKUWA HATUNA UTARATIBU WA KUSAIDIANA KAMA WENZETU WAZUNGU, ONA WAZUNGU MPAKA LEO BADO WANATULETEA MITUMBA TUNAVAA, YAANI MPAKE LEO BADO WANATUFIKIRIA SISI TUAISHIJE, LKN SISI KWA SISI TUNAFIKIRIA JINSI YA KUMALIZANA NA KUIBIANA KIDOGO KILICHOPO. KWAKWELI KAZI IPO.
    OK KAKA MITHUPU MBUNGE WA JIMBO LA NINI KIBARUA BADO NINAKIRUDISHA KWAKO TAFADHARI TUTAFUTIE MAWASILIANO YA HUYU DADA NA AHARAKA SANA TUWEKEE KWA WINO MWEUSI ILI TUHANGAIKE NAE, HATUNA PESA NYINGI LKN HIZO HIZO NDOGO TUTAGAWANA NAE INSHAH ALLAH.

    NI MIMI,
    MUDDY NICE, DSM-TANZANIA

    ReplyDelete
  2. Mwenyenzi Mungu akulinde Eliza katika mkakati wako wote wa kutaka kuwaokoa maisha ya watanzania wenzetu.Endelea kuwa shujaa na kweli kama ulivyosema siku mmoja nawe uweze kujulikana duniani,hakuna lisilowezekana mbele za Mungu.
    mdau scandi...

    ReplyDelete
  3. Hata mimi nataka kujua baada ya kupata tuzo ya mtv, anafanya nini sasa hivi huyu dada. kuna wakati nilipata email kutoka NIKE (kitengo cha Africa) nafikiri, walikuwa wanamtafuta kwa ajili ya tuzo wanazotoa kila mwaka kwa wanawake wanaofanya mabadiliko ktk jamii.

    Kupitia website ya hyena square, niliwatumia email lakini sijasikia chochote wala hawakunijibu.

    Hivi ni vitu ambavyo vinaturudisha nyuma, yaani website ipo lakini hawafanyi update au kucheki barua pepe angalau hata mwezi mara moja tuu

    ReplyDelete
  4. Uncle Michuzi, BADO HUJASOLVU TATIZO, SISI TUNATAKA KUPATA KONTAKT ZAKE ILI TUMSAIDIE TUMEKWISHA SOMA STORI ZAKE KIBAO, KWA NINI UNAKUWA HIVYO MJOMBA????

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi mimi huwa sicomment humu,lakini leo uzalendo umenishinda. Ile video ya Eliza (Uwanja wa Fisi) kwanini usionyeshwe kwenye National TV?! Ile kila mtu aione...wanaongoza nchi waione?! Kweli serikali inashindwa kuteketeza ilo eneo, na maeneo mengine kama hayo?! Serikali inaachia wananchi wenye uwezo mdogo kutatua tatizo hii!!! Mafisadi wanajilimbikizia mabilioni...kwanini wasisaidie watu kama hawa?!! Serikali yetu iko wapi?! Hii ni AIBU! Kelly Rowland sio mtanzania na kadhalika SIO kiongozi wa serikali yetu...wahusika wako wapi???!!!
    Kaka Michuzi unge-campaign mambo kama haya yaonyeshwe kwenye TV zetu huko Tanzania!

    Mdau mwenye hasira sana!

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha sana kuona Tanzania kuna jamii ina maisha magumu kiasi hiki,hivi hii serikali haya yote yanatendeka uwanja wa Fisi ,serikali inatazama tu kwa nini isichukue hatua madhabuti? wizara husika,hizi ndiyo kazi za kufanya,saidieni vijana pale wenye maisha magumu, anzisheni kituo cha kuwasaidia na kutafuta misaada k.m budget haitoshelezi na kufunga lile eneo permanently period!yaani mpaka wakina Kelly Rowlands waje all the way from US, si aibu hii?

    ReplyDelete
  7. yaani nimetumiwa jana documentary ya huyu dada imenitisha sana na kunifanya nijiulize ni jinsi gani ya kumsaidia huyu dada na wengine wote walioathirika na huu ugonjwa michuzi hizi ndio habari tunazotaka tafadhali tufahamishe jinsi ya kumsaidia huyu dada. Mimi siishi huko ila ninaweza kutoa msaada wa kumsaidia arudi shule kama anavyotaka, tafadhali kaka michuzi tufahamishe jinsi ya kusaidia ndugu zetu.
    Mdau North America

    ReplyDelete
  8. halafu alivyoongea tu nilijua huyu dada ni ndugu yangu "Mnyalukolo"
    Go Eliza Go.

    Mdau Mkwamis

    ReplyDelete
  9. kaka michuzi nimeguswa sana na mkasa wa huyu dada kwa kweli inahuzunisha sana kama wadau kweli wanampango wakumsaidia mimi natoa mchango wangu kwa kuwapa direction ya offisi za mkurugenzi wa KIWOHEDE anaitwa J.J MWAITUKA ambaye ndio mtu anayemsaidia Eliza hadi hivi leo pia offisi zake zipo buguruni malapa nyuma ya kituo cha mabasi kuna ghorofa limeandikwa kiwohede. kweli Tusaidiane Watanzania.

    ReplyDelete
  10. kaka michuzi sie wengine hatuishi bongo ukitupa njia ya kwenda ofisini kwa huyo bosi wake inakuwa tabu kujua (muda mrefu hatujarudi) kuna western union/money order tupe namba zake tumsaidie dada yetu. Mie niko chuo kikuu napenda sana watu wakiwa wanatafuta mabadiliko leta namba zake au zako utuwakilishe.

    dadio, Mkwamis Mnyalukolo

    ReplyDelete
  11. Nashangaa kuona kuwa kuna baadhi ya makampuni makubwa kabisa hapa nchini yanafadhili mashindano ya ulimbwende,mashindano ya mbio za mbuzi n.k. yanaacha kusaidia juhudi binafsi za watu kama huyu wanaoiokoa jamii ya kitanzania isiangamie!!! Eliza, mungu akubariki, akuzidishie ujasiri na zaidi ya yote akuongezee umri ili uyakamilishe yale yote uliyoyapanga kuyafanya kwa watanzania wenzako. -Yosi

    ReplyDelete
  12. anko asante sana kwa kufuatilia ingawa bado haitoshi we need her contacts. Huyu binti angefaidika zaidi kama angerudi dar es salaam. sidhani kama alirudi kijijini kwa hiari yake, possibly kwa kushindwa kumudu, but mjini ndipo anapoweza ku meet her goals like kusoma, na kama tunavoona wadau wengi wako radhi kumchangia, she can start up some biznez bcause lets face it ameshawahi kuwa mtoto wa mjini kijijini hakumfai, pia kiafya mjini atakuwa na advantg kimatibabu, sasa ivi atawapa stress bure wazazi wake ambao most likely hawana uwezo, kama tulivomcheki ktk maelezo yake she is a very intelligent girl, she communicates very well!, na hiyo ni advantage sana in todays world, na personality yake she is very likable, she has no biznez wasting in the village. wanablog wote tulioguswa na hii habari ya huyu binti tukimsaidia right away nakwambia miaka michache ijayo atakuwa mbali sana na tutamsikia. she has what it takes, lakini ni muhimu sana arudi dar panga chumba na sebule anza shule kwa misaada toka kwa wadau and things will fall into place.Niko tayari kutoa kodi ya mwaka wa kwanza. Hey anko kabla sijamaliza, muombe rafiki yako maggid mjengwa amtrace huko iringa (he has been to every village in TZ) he will find her in a few hrs, he is very nice you know hatamaind!,,,
    grasuj@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...