Home
Unlabelled
siku mwili wa baba wa taifa ulipoletwa dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nilikuwa MAZENGO wakati huo? Form sics
ReplyDeleteyan hii siku ilikuwa ni masikitiko,, kipindi hicho niko shule, hatukwenda shuke kwa wiki moja, it was a very sad week.. and it was so shocking...
ReplyDeletelakin Mungu amempenda ...but for us he remains as a legend!!!
we miss you J.K.Nyerere...
Namna pekee ya kumuenzi Mwalimu ni kwa kumfunga sumaku maiti yake na kuzungusha coil jeneza lake.
ReplyDeleteNamna hiyo, wakati anazunguka kwenye kaburi lake anapoangalia nchi inapoelekea, atakuwa anatengeneza umeme na kupunguza makali ya mgao.
mi naona tuache kudiscuss huu upuuzi na tuangalie mambo ya maana.
ReplyDeleteHe has died already...kuna vitu vingi vya maana zaidi ya hivyo,na si kwamba alikuwa kiongozi bora kuliko wote,ingawa kweli aliheshimiwa sana.
but we face 21st Cent. challenges,
NAKUMBUKA NDIO NILIKUWA NAMALIZA DARASA LA SABA NILIKUWA KWA MJOMBA WANGU NAYE PIA HATUPO NAYE DUNIANI KIPINDI HICHO NIKIWA NA MIAKA KUMI NA NNE,.MUNGU AMETOA NA MUNGU AMETWAA NAMUOMBA MUNGU AMMPE MWANGAZA MWEMA BABA YETU WA TAIFA.
ReplyDeletenililitegesha manzese darajani pale kusubiri jeneza lipite. nyomi lilikuwa si la kitoto!! for sure the guy was great!!! kifo chake kilikuwa cha kipekee. nakumbuka mzee mzima pale manzese darajani nilikuwa nawashangaa wanaolia mi nikajikaza kwa sabuni lakini nilipoliona tu gari lililobeba jeneza nikashangaa na mie ninalia ka mtoto. nilikwenda St joseph pia wakati wa misa, nikaenda uwanja wa taifa pia nikapanga foreni kuuaga mwili. wakati anazikwa mvua kubwa ilipiga. ama kweli alikuwa mtu wa kipekee
ReplyDeletealiyoyatabiri kwenye speech yake pale kilimanjaro hotel 1995 yote tunayaona yanatokea sasa hivi!! alisema huwezi watumikia mabwana wawili, mabepari/mafisadi na wananchi maskini pia!! akasema serikali ikiwatumikia wenye nazo basi itajikuta haikusanyi kodi kutoka kwa wenye nazo itajikuta inaishia kukimbizana na vijitu vidogovidogo barabarani!! haya ndo tunayaona sasa!! akasema pia ukimwona mtu anatumia pesa kutaka kuingia ikulu basi muogopeni kama ukoma. unapotumia pesa kuingia ikulu hizo pesa utazirudishaje? mtu anayetumia pesa kuingia ikulu yeye binafsi ni fisadi na atawalinda sana mafisadi washkaj zake waliomsaidia kuingia pale!! anyway ngoja ninyamaze manake michuzi nae dakika tano mbele ukikamua sana anakuchinjilia baharini anakupotezea tegeta!! ha ha ha usinibanie mwanangumwenyewe michu!!
katika hotuba ya kuomba kura ya kukiwakilisha chama katika ugombea uraisi Mark Mwandosya alisema 'siwezi kuwaahidi chochote wajumbe na wanachama ila ninaahidi kuwatumikia watanzania wote' what a genius!!!. wengine wao walitoa ahadi kedekede na matokeo ya ahadi tumeyaona!!!
Ah michuzi samahani nilijisahau tena nikapitiliza nisamehe mwana basi naishia hapahapa, mengine nitakwenda kuyamwaga kule mtaa wa kaka make lile ni jiko la shamba halichagui kuni!!!
duh Nyerere was great wazungu wenyewe walikuwa wanakoma, waandishi wa habari wa kizungu waliokuwa wanamfanyia nyerereinterview walikuwa wanatamani kulala mbele wakati maswali wanayauliza wenyewe!!!
Mzee wa PhD
Uswisi.
kaka vekesheni zako siku moja tia timu geneva hapa ule maisha, hapa ni kama peponi vile!
TULIVUNJA VIPINDI MPAKA ALIPOZIKWA TULIKUWA ST MARY'S NYEGEZI SEMINARY MWANZA
ReplyDeleteMichuzi mimi nilikuwa Bugando hospitali huko Mwanza nimelazwa. Nilikuwa napata taarifa kupitia kwa ndugu na jamaa waliokuwa wanafika kuniona. Ni kweli nchi yote ilizizima.Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.
ReplyDeleteDuuuh! Wewe anony.. wa October 15 12:07PM subiri wakushukie wenyewe. Nisichoelewa ni kitu gani kipya katika hili. Maana baadhi ya komenti zinazoendelea kutolewa kuhusu JKN zina miaka 9 sasa. Kimsingi hakuan jipya, matatizo yapo pale pale tangu Nyerere mwenyewe akiwa hai. Tatizo watu ni wepesi kusahau na wagumu kukumbuka.
ReplyDeleteJKN aliondoka madarakani na kuacha nchi hii ina hali ngumu kuliko maelezo, viwanda karibu vyote nilikuwa mochwari na mipaka ilifungwa kuzuia bidhaa za nje kuingia.
Bidhaa zilipatikana maduka ya ushirika na RTC tena kwa miezi kadhaa manapata bidhaa mara moja.
Nania alikuwa na TV nyumbani kwake wakati wa JKN? Sitakia hata kukumbuka hayo mambo mimi, aaaaaaaaaaaaaaaaah!
KICHWA CHA HABARI HAKIPO SAHIHI, KINATAKIWA KISOMEKE HIVI " SIKU MWILI WA BABA WA TAIFA ULIPOTOLEWA DAR" MAANA ULIPOLETWA ULILETWA NA NDEGE TOKA UK, NA HAPO NI SIKU ULIPOKUA UNAONDOLEWA.
ReplyDeleteNaikumbuka sana siku hiyo nilikuwa Aga Khan hospital nimefanyiwa operation kwenye alfajiri ya saa 10. Wakati nazinduka kutoka kwenye dawa ya usingizi ndio nasikia manurse wanakwenda kuangalia mwili unapitishwa kwenda Msasani nyumbani kwake.
ReplyDeleteMama Sweet
dah nakumbuka nlikuwa napig boksi uk kama kawa
ReplyDeleteNilikuwa shuleni SHYCOM form 5.Tulikuwa na wasiwasi labda machafuko yanaweza kutokea nchini.
ReplyDeleteNilikuwa mmoja wa watu waliokuwa katika barabara maeneo ya buguruni karibu na relini, nilishuhudia huu msafara, ilinitoa machozi sana hii scene na nilikumbuka tukio la aina hii wakati marehemu Sokoine anapelekwa kuzikwa Monduli 1984. Wakati huo TVT now (TBC)walikuwa kwenye Test Signal hivyo kila jioni walikuwa wakionyesha matukio ya siku nzima. Nilirekodi kila siku na nina kumbukumbu za matukio hayo yote na historia nzima ya Mwalimu pamoja na hotuba zake zilizokuwa zikirushwa wakati ule.
ReplyDelete...huko Mazengo Form sics ulifaulu?
ReplyDeleteAnon 12.07, acha kufuru!
ReplyDeletePumbavu nini...machafuko gani?
ReplyDeleteYAANI ILIKUWA NI SIKU YA MASIKITIKO MAKUBWA KWANGU. HAIELEZEKI. SIJUI KAMA KUNA VIDEO YAKE INAUZWA MAHALI ITABIDI KUITAFUTA
ReplyDeleteda nilikuwa sumbawanga maeneo ya majengo nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari ya sauti ya ujerumani nakumbuka ilikuwa saa 7 mchana na mtangazaji alianza na maneno yafuatayo:MWANAHARAKATI,MKOMBOZI,MPIGANIA UHURU NA MTETEZI MKUBWA WA UHURU BARANI AFRICA MWL JK NYERERE AMEFARIKI DUNIA HUKO UINGEREZA KATIKA HOSPITAL YA SAINT THOMAS nilisikitika sana siku hiyo na roho iliniuma sana,mdau nipo dc-usa
ReplyDeleteNakumbuka nilishinda barabarani pale nyumbani kwetu kinondoni mkwajuni ili nione sanduku la baba yetu mpendwa J.K NYERERE kwa mara ya mwisho,na nilienda uwanja wa taifa kumuaga,MUNGU AILAZE ROHO YA MPENDWA WETU PEMA PEPONI AMEN.
ReplyDeleteMwl mpaka anaondoka madarakani aliacha viwanda kumi na mbili vinafanya kazi,kweli kila binadamu anakasoro zake hata Mwl alishawahi kukiri hivyo, mpaka anaondoka madarakani(siyo anafariki) hakuna mgodi hata mmoja wa dhahabu aliwapa wageni(mnaita kubinafsisha),hakuna mbuga hata moja ya wanyama wetu aliwapa WAARABU,zilikuwa chini ya serikali maana huo ni urithi wa vizazi vyetu,Mwl mpaka anaacha madaraka kulikuwa hakuna neno"FISADI" niambieni mfano wa waziri mmoja tu wakati wa mwl alituhumiwa kwa ufisadi,natoa changamoto kwa wachangiaji,na je mpaka leo tunaviwanda vingapi vinafanyakazi??,migodi mingapi wamechukuwa wageni na je wazawa wanafaidika vipi?
mimi mdau toka, Bradford uk
Nilifaulu na ndio maana kwa sasa na browse tu kwenye net sweetie.....ukwapi she wangu now days?
ReplyDeleteshe wangu?ukwapi unanijua hata kiswahili hujui sijui ulifaulu nini
ReplyDeleteWapi na wapi. Ufaulu halafu uandike SIX kuwa ni SICS! Huko Mazengo mitihani ilikuwa katika Kiswahili mpaka na wewe ufaulu?
ReplyDeleteNilikuwa kidato cha nne ndani ya mtihani wa mock wa somo la civics, taarifa ya msiba ilitusikitisha sana.
ReplyDeletemimi nilikuwa mjamzito nimechoka mbaya nilijifugua mwezi uliofuata mtoto wa kike anaitwa ESTHER ni jina la mama yangu mwezi ujao nae atakuwa na miaka kumi nimemwambia kashangaa sana
ReplyDeletekusema kweli ilikuwa hudhuni sana
kama alivyoeleza
anon WA THU OCT 15,03:53 PM
MWALIMU ALITUDHAMINI SANA KWANI KAMA KIONGOZI ALITUNZA MALI YA ASIRI NA ARIDHI KWA AJILI YA KIZAZI HUONI KAMA ALITUJALI SANA WANAINCHI WAKE NAJUWA MWALIMU KABARIKIWA TU NA NDIYO MAANA ALICHUKULIWA MAPEMA NA BABA MUUMBA KWANI ANGEKUWEPO ANGETESEKA SANA NA UFISADI UNAOFANYWA NA WENYEKULAANIKA
nilikuwa ndio kwanza nimemaliza darasa la 7 kipindi hicho.
ReplyDeleteBraza michuzi, hiyo ni picha ya nini?!
ReplyDeleteAnyway, ukirudi kwenye topic. nadhani Mkapa ndo alikuwa anaogopa kuliko mtu yeyote hapo.
mi nilikuwa hapa Madison Square napiga kikapu, warm up/jaramba.
= = =
Buffalo, (karibia na butiama)
New York.
huyo aliesema machafuko atakuwa kama sio mrwandwa basi mcongoman tu,machafuko yaletwe na nini sasa
ReplyDeleteProfessor Ali Mazrui on Mwalimu:
ReplyDeleteThe two top Swahili-speaking intellectuals of the second half of the 20th Century are Julius Nyerere and Ali Mazrui". That is how I was introduced to an Africanist audience in 1986 when I was on a lecture-tour of the United States to promote my television series: The Africans: A Triple Heritage (BBC-PBS.) I regarded the tribute as one of the best compliments I had ever been paid. In reality, Mwalimu Nyerere was much more eloquent as a Swahili orator than I although Kiswahili was my mother tongue and not his.
In the month of Nyerere's death (October 1999), the comparison between the Mwalimu and I took a sadder form. A number of organisations in South Africa had united to celebrate Africa's Human Rights Day on October 22. Long before he was admitted to hospital, they had invited him to be their high-profile banquet speaker.
When Nyerere was incapacitated with illness, and seemed to be terminally ill, the South Africans turned to Ali Mazrui as his replacement. I was again flattered to have been regarded as Nyerere's replacement. However, the notice was too short, and I was not able to accept the South African invitation.
With Julius Nyerere and I, it was a bond of genuine ups and downs. Nyerere was once angry with me because I had written a citation for an honorary doctorate which was too long. The honorary doctorate was for an elderly American academic, and Nyerere was awarding the degree as Chancellor of the University of East Africa (which at that time consisted of the campuses of Makerere, Nairobi and Dar es Salaam).
As University Orator, I had written the citation, and was reading it as the elderly gentleman knelt before Nyerere. My oration was indeed too long. Nyerere did not speak to me that evening after the ceremony. He deliberately snubbed me. He had been disturbed that the elderly recipient of the honorary degree had to kneel for so long while I delivered the oration praising him. I had not struck the right balance. I felt truly chastised by the Mwalimu.
Let me also refer to Walter Rodney. He was a Guyanese scholar who taught at the University of Dar es Salaam and became one of the most eloquent voices of the left on the campus in Tanzania. When Walter Rodney returned to Guyana, he was assassinated.
Chedi Jagan, on being elected President of Guyana, created a special chair in honour of Walter Rodney. Eventually I was offered the chair and became its first incumbent. My inaugural lecture was on the following topic: "Comparative Leadership: Walter Rodney, Julius K. Nyerere and Martin Luther King Jr."
After delivering the lecture, I subsequently met Nyerere one evening in Pennsylvania, USA. I gave him my Walter Rodney lecture. He read it overnight and commented on it the next morning at breakfast. He promised to send me a proper critique of my Rodney lecture on his return to Dar es Salaam. He never lived long enough to send me the critique.
Nyerere's policies of Ujamaa amounted to a case of Heroic Failure. They were heroic because Tanzania was one of the few African countries which attempted to find its own route to development instead of borrowing the ideologies of the West. But it was a failure because the economic experiment did not deliver the goods of development.
On the other hand, Nyerere's policies of nation-building amount to a case of Unsung Heroism. With wise and strong leadership, and with brilliant policies of cultural integration, he took one of the poorest countries in the world and made it a proud leader in African affairs and an active member of the global community.
Julius Nyerere was my Mwalimu too. It was a privilege to learn so much from so great a man.
http://www.africaresource.com/index.php?option=com_content&view=article&id=56%3Anyerere-and-i&catid=85%3Aoral-history&Itemid=341&limitstart=1
Wakati huo nilikuwa naishi ukonga mombasa, hivyo nikajongea hadi uwanja wa ndege wa zamani, nikaenda kushuhudia jeneza likitolewa kwenye ndege, kulikuwa na halaiki!
ReplyDeletemdau wa 12:07 wewe tunafahamu uko kundi moja na na jamaa fulani wakati mwl anaumwa yeye akawa anamuombea afe
ReplyDeleteMAFISADI OYEEEE MAPAPA WATU OYEEEE MAFISADI NA MAPAPA WATU NAWAPA HONGERA SANA KWA UJANJA MLIOKUWANAO
ReplyDeleteENDELEENI HIVYO HIVYO KULA MALI ZA WANANCHI NA MKAJIACHIE NCHI ZA NJE WAACHENI WALALA HOI WAFE NA MAGONJWA NA NJAA NA WAKOSE ELIMU BORA
KULENI KWA KWENDA MBELE IKIWEZEKANA HATA IKULU IPIGENI BEI MHAMIE HUKO ULAYA AU AMERICA
WAACHENI HAO WALALAHOI WALIOPIGWA SINDANO ZA UNDONDOCHA WABAKIE WAKIIMBA SISIEEEEEEEMU OYEEEE SISIEEEEEMU YAJENGA NCHI
MAANA HAWATAKI KUAMKA WANAIBIWA KILA SIKU MALI ZAO ZINALIWA NA MAFISADI WAO WANABAKI KUFATILIA HABARI UTASEMA MPIRA WA SIMBA NA YANGA
KILA KITU MNAMTUPIA MH,RAIS ETI AMALIZE UFISADI UNAFIKIR ATAMULIZA VIPI KAMA HAKUPATA MSAADA WENU KATIKA KUSHIRIKIANA NAE KUMALIZA UFISADI
MH,KIKWETE HONGERA SANA KWA KAZI UNAJITAHIDI KWA KIWANGO KIKUBWA KISICHOFANANA NA VINGOZI WOTE WALIOTANGULIA MBELE YAKO.
Nilikuwa katika sherehe yangu ya kumaliza darasa la saba nakumbuka walituzuhia tufanye sherehe tukakataa wakatwambia basi tusipige mziki, sherehe ilikuwa kama kilio vile. vipi wenzangu wahitimu wa darasa la saba 1999 ilikuwaje kwenu? mlisogeza hadi tarehe 29 kama amri ya serikali ilivyokuwa au hamkupiga mziki kama sisi??
ReplyDeleteNyerere? He was a leader a philosopher, a prophet, a teacher, a politician, a diplomat, a socialist, a parent,....In short he was a great man. Wakati huo I was 49 years of age. Nilikaa siku zote kwenye TV nikilia kama mtoto mdogo. Yule mzee jamani hapana he was a jewel that Tanzanians will never forget.
ReplyDeleteBinafsi alitusaidia mimi na wadogo zangu wawili. Wakati wa kutaifisha majumba nyumba ya baba yetu aliyotuachia urithi ilitaifishwa. Hiyo nyumba ilikuwa ya mkpo wa serikali na mama yetu ilimsaidia sanakutusomeshea sisi.Wakati huo mimi nina miaka 21.
Waatendaji wa serikalini pale wizara ya ardhi hawakutaka kusikia kelele za mama yetu. Kimuujiza siku hiyo mama yetu kaenda kusali pale st Peter akamvizia Rais Nyerere wakati anatoka kamfuata Rais na kumeueleza masahibu yake. Pale pale kamwagiza Butiku na appointement mama akapewa for the next day. Siku iliyoifuata Nyerere akamsikiliza na kutoa amri nyumba irudishwe na deni lifutwe. Sasa niambie mimi au mama yangu tutamsema vibaya Nyerere? Nonono. Kweli siku hiyo nililia!!!!!
SIKU HIYO NILIKUWA RIGHT IN-FRONT OF THE PLANE AT THE AIRPORT NILITEMBEA KWA MIGUU TOKA AIRPORT HADI MSASANI, SASA NIKUPE KITUKO KILICHONITOKEA NI HIVI TULIPOKUWA AIRPORT TULIKUWA KUNDI KUBWA SANA TUMESONGAMANA NA KIBAKA MMOJA AKAINGIZA MKONO NDANI YA MFUKO WANGU KULIKUWA NA PESA ZA KUTOSHA, NIKAUSHIKA MKONO NA KUUTOWA NJE NA KUMUONYA KUWA AKIENDELEA BASI NITAMWIITIA MWIZI AKASEMA SAMAHANI MZEE YAISHE, SASA UNAJUWA YALIYOTOKEA BAADAYE, NILIPOFIKA BUGURUNI KUJIPAPASA MFUKONO PESA YOTE IMEENDA, NIKABAKI KUCHEKA TU NIKASEMA MWIZI AKITAKA KUKUIBIA ATAKUIBIA TU.
ReplyDelete