mshambuliaji hatari wa simba, uhuru selemani, akisherehekea goli lake la kwanza dhidi ya jkt ruvu neshno ya zamani jijini dar leo. simba iliendelea kushinda bao 4-1 katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom
kocha wa simba patrick phiri akiwa neshno leo kabla vijana wake hawajaibamiza jkt ruvu 4-1

beki wa ruvu jkt akiwa kachelewa wakati ngoma inaingia kimiani kuandika bao la 3
ni bao la nne na kipa wa jkt ruvu na mabeki wake hawana la kufanya wakati wavu unatikiswa
hekaheka langoni pa jkt ruvu
kipa wa simba juma kaseja akichekelea karamu ya magoli na wenzie dhidi ya jkt ruvu

wachezaji wa simba wakimshangilia uhuru selemani baada ya kufunga
stori kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. juma kaseja karudi simba lini?mdau nipo usa

    ReplyDelete
  2. aaahh, jamani mwaka huu raha tuputupu,
    Mashetani Wekundu oye,Wekundu wa Msimbazi raha.
    Poleni wapenzi wa bwawa la nini sijui,washika manati wa london,na watu wa darajani.
    Vijana wa jangwani vipi?kiu kali?naona ni nchecheme nchecheme tu.

    ReplyDelete
  3. Uncle usipobadili jezi mwaka huu basi tena!!! kwa kweli Simba tunatisha tena kwa kishindo yaani mnapotuombea balaa ndo kwanza mafanikio yanakuwa mara nne yake lloh...haya nanyi hongereni kwa kutoa sare na Viazam

    ReplyDelete
  4. Kweli huu mwaka wetu bado yebeyebo-asanteni sana wachezaji kwa kutupa raha-bariidi Madega upo.
    mdau iPINDA lUSUNGO kYELA.

    ReplyDelete
  5. mdau wa kwanza kwenye maoni we inaonyesha kabisa soka la nyumbani haunalo mawazoni yaani hata kaseja haujui kuwa alisharudi simba. any way mi nafurahia tu vijana wanavyofanya kazi, hii ndo soka ila sasa bado mechi moja tu msimu huu hii ikiisha basi unazi utapungua mwaka huu. Simba ina unguruma kweli kweli msimu huu!!
    simba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
    nitakuwepo kwenye mechi na watani!!!

    ReplyDelete
  6. Nilivyosema Phiri mkali kuliko Maximo kuna watu wenye fikra za kitumwa bado wanababaika na rangi ya Maximo. Pimeni uwezo jamani tusiwe wajinga kama madondoeka.

    ReplyDelete
  7. Haitwi James Phiri ni Patrick Phiri

    ReplyDelete
  8. michuzi eeh!!
    hizi jezi ziandikwe basi majina. licha ya kampuni kubwa the serengeti sijui au the TBL kuwa mfadhili wa hawa ndugu wawili, bango kubwa kilimanjaro majina ya wachezaji hayapo, duu. mda wa kusonteana kwamba yule si ndiyo falani nomaaaa.

    ReplyDelete
  9. MUHESHIMIWA MICHUZI..!!!
    MICHUZI TOKA UANZISHE HII WEB SITE/BLOG HUWA NAPITIA TU KUANGALIA MAONI NA COMMENTS NA KWA KWELI HUWA ZINA NICHEKESHA NA ZINGINE ZINASIKITISHA HASA PALE WALENGWA WETU WANAPO TUSIWA PASIPO NA SABABU, IN FACT MIMI MWENYEWE NIMETUSIWA SANA HUMU LAKINI HII NDIYO FREEDOM OF SPEECH. SASA MIMI NAPENDA WEWE MICHUZI UNIDOKEZE TU KWA KIFUPI AMA MDAU YEYOTE ANAYE JUA, KWA SABABU SIMBA NA YANGA ZIMEKUWA ZIKITAMBIKIA NA KUJIHUSISHA NA USHILIKINA JE NI ALBINO WANGAPI WANAWEZA KUWA WAMEUWAWA KWA SABABU ZA IMANI HII POTOFU YA KICHAWI? MICHUZI SINA EMAIL YAKO LAKINI NAOMBA UITOE HII COMMENT PEKE YAKE KAMA MADA MUHIMU WADAU WANIELIMISHE. ASANTENI
    MUNGU IBARIKI SOKA YA TANZANIA.

    JACK PEMBA
    LONDON, UK

    ReplyDelete
  10. Mdau unayejiita "Jack Pemba" unatoa maoni kama hayo halafu unashangaa watu wakikuporomoshea matusi.
    Usajili wa Simba ulikuwa wa kuziba mapengo tu lakini kikosi chao cha mwaka huu ni sawa na cha mwaka jana. Kabla ligi haijaanza waliingia Zanzibar kufanya mazoezi. Wamekuwa na kocha mmoja mjuzi na mzoefu katika soka pia mazingira ya Afrika tokea katikati ya msimu uliopita. Wana wachezaji wenye vipaji. Hawana kelele za migogoro. Sasa hivi wanashusha kipondo kwa kila timu wanayopambana nayo. Ushirikina uko wapi hapo?

    ReplyDelete
  11. Weye Jack Pumba, aka Pemba tunakujua usanii wako wa siku nyingi sana! Ndiyo maoni gani hayo ya kipumbavu unayoyatoa mtu kama wewe unaejifanya mtu wa spoti?

    Hii timu imeandaliwa kisasa, hatujasajili mabondia kama yule wa cameroon, na players wametayarishwa kisaikolojia. Wanalala na kula vizuri, na wanajua kazi yao. Wanajua sera yetu mpya ya kuwasaidia kupata timu nje. Mambo yenu ya usangoma tumewaachia nyie, na ndiyo ujue mpira sio pesa za ufisadi, ni maandalizi ya kitaalam tu.

    ReplyDelete
  12. Tarehe 31/10/2009/.

    YANGA 3 SIMBA 0

    NANI ANABISHA?

    ReplyDelete
  13. Ni kweli Phiri ni kocha mzuri sana ameonesha mafanikio makubwa. Maximo hamuingii Phiri kwa utaalamu hata kidogo, TFF wanababaika naye kwa kuwa katoka Brazil, waangalie performance yake mbovu, ona Afrika Kusini wamemtimua kocha mbabaishaji wa Brazil, Santana ndio type ya akina Maximo, wenzetu hawataki mchezo. tatizo la bongo wanaosimamia soka wengi wao ni washamba hawataki kusikia ushauri wa kitaalamu. Ona kipa wa Maximo, Shaban Dihile amefungwa magoli 4 ya kijinga kabisa eti ndio chaguo namba moja la Maximo. Ki ukweli performance ya Juma kaseja ni zaidi maradufu ya Dihile, huwezi linganisha na ya Dihile hata siku moja, kama ni ufupi
    wa Kaseja mbona kipa Kidiaba wa timu ya taifa ya DRC au klabu ya TP Mazembe ni mfupi na anafanya kazi nzuri. Tanzania tunapoteza bahati zetu kwa kusikiliza washamba fulani wanaojitia wanamichezo wazoefu kumbe hakuna kitu.

    ReplyDelete
  14. Haaa haaa haaa haaa. "tatizo la bongo wanaosimamia soka wengi wao ni washamba hawataki kusikia ushauri wa kitaalamu". Jina la mtaalamu halikuweza kufahamika kwa mara moja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...