Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akiwapungia mkono wananchi wa jiji la Mwanza walipompokea rasmi jijini humo jana,aliyesimama kushoto ni mmoja wa waandaji wa Vodacom Miss Mwanza Anita Zimbire.
Jinsi maandamano ya mapokezi ya Vodacom
Miss Tanzania Miriam Gerald yalivyofana jiji Mwanza leo
Wananchi wa jiji la Mwanza wakimpungia mikono Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kuwasili kutokea uwanja wa ndege jijini Mwanza

Mzee Yahaya Msabaha (81)(kushoto)akisalimiana na Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald (kulia)kwenye ofisi za Vodacom jijini Mwanza alipoenda kupatiwa huduma za M Pesa, mara baada ya mrembo huyo kuwasili kutoka Dares Salaam (katikati)Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania Steven Kingu.
Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akiwapatia vinywaji watoto waishio katika mazingira magumu katika maeneo ya Bwiru jijini Mwanza mara baada ya kuwasili rasmi katika jiji la Mwanza akitokea Dar leo
Afisa habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akimpatia maelekezo Meneja wa Simba Telecom Bw.Rajendra(kulia) aliyekuwa mwajiri wa Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald, namna atavyompatia maua aliyeandaa kwa ajili ya mrembo huyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Vema imependeza, ila nina angalizo moja. Bado tuna matatizo sana katika usimamizi, hebu angalia hao waendesha pikipiki, kati yao hakuna hata aliyevaa helment, sasa jamani linapotokea la kutokea tulaumu nani? Yawezekana walipewa usaidizi na askari wa usalama barabarani, maana hata kwa namna nyingine kwa barabara zetu finyu, msururu huo umeleta kero na pia hata kupunguza utendaji kazi kwa wengine. Tunapenda nadhanria sana kuliko vitendo, maana mie sioni umuhimu wa kukusanya watu wote (na hii yaonyesha watanzania wengi hatuna la kufanya) na kujipanga kama tulivyozoea kufanyishwa na ccm; mwenye blg usibanie maana kila mara ati mawazo yangu kwako hayakubaliki

    ReplyDelete
  2. Kaka nanihii! hivi kweli mpaka wa leo huwa mamiss wa tanzania wanaandaliwa ratiba za kugawa Juice na vitu vingine vingii kwa mayatima? mbona suala hilo ni jukumu la kijamii zaidi na sii la kumpa ujiko sana kihiiivyo miss Tanzania?? Kuna maeneo mengi sana ya kufanyiwa kazi ambayo yataleta maana na mtazamo tofauti wa miss Tanzania. Ni kipi anachokiendeleza toka kwa mtangulizi wake ambacho kitakuwa ni sehemu ya kipimo cha utendaji wake kwa jamii kwa wakati wote atakapokuwa akishikilia taji hilo? Miss aanzaishe mradi endelevu utakao toa misaada kwa yatima na pia abuni kitu kitakacho bakiza kumbukumbu kwakwe.

    ReplyDelete
  3. This is too low

    ReplyDelete
  4. tusubiri miss world!sijui kama ataonekana huku! pumba tupu!

    ReplyDelete
  5. Hapo hamna cha miss Tanzania wala nini,ila ni Vodacom wanatangaza biashara yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...