hapa ni mikocheni B karibu na daraja la mlalakuwa njia iendayo coca cola kutokea mwenge ambayo inapigwa mkeka kama ilivyo kwa barabara nyingi za mitaa hiyo.
hapa ni msasani kwa mwalimu ambapo leo greda limeonekana likibomoa lami kukuu juu ya barabara ya old bagamoyo road, na kwa mujibu wa vifusi vinavyomwagwa kutatandikwa mkeka mpya katika kuboresha miundo mbinu ya jiji hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Walikuwa wapi kabla ya uchaguzi kukaribia? Hizi sera zao tunazijua, wakishachaguliwa wala hatutawaona.
    Wananchi tuweni makini kuchagua viongozi wanaosikiliza kero zetu bila kujali uchaguzi umekaribia au ndo wameingia madarakani.
    Kazi ipo.
    Michuzi usibanie, maana hata wewe ulikuwa unatuhabarisha wakati wa mvua watu wanapiga makasia barabarani na hatukuona viongozi wakihangaika, sasa muda umekaribia wanajidai kujisafisha. Mi hawanipati!

    ReplyDelete
  2. wasijenge barabara tu wapanue na hilo daraja la mwaka 47.

    ReplyDelete
  3. michuzi ni vema wangekwenda na kule mburahati, kawawa, mabibo makutano tabata kimanga nk huko barabara ni mbovu na ni kama utadhani kuna sheria imewekwa kuwa barabara hizo zisinuse rami milele. kila kukicha mikocheni, msasani, masaki, kwani huko ndo wanapoishi binadamu pekee jamani??? hebu serikali kuweni na huruma mbona hivyo!!! watu huko mabibo ni vifua kila siku vumbi ni kali sana!!!
    yani basi tu!!! tanzania hii!!
    mdau mzawa, Masaki.

    ReplyDelete
  4. Ningeiyomba serikali ifanye itikadi ya kuongeza barabara nyingi Dar na mikoa minginge. Kwanza pale Kigogo wangechana barabara kwenda buguruni ili wa2 wanaotoka magomeni, manzese, kinoclain na kadharika kuepuka foleni za rush hour kwenda buguruni. Barabara hiyo itengenezwe ktk bonde la sukita. 2naona magari mengi Dar, kumbe barabara ndio ndogo. Serikali lifanyieni kazi jambo ili tanueni barabara nyingi

    ReplyDelete
  5. Rekebesho lakizushi hili michuzi. Sio barabara ya old bagamoyo road. Ni Old bagamoyo road. barabara na road ni same thing tofauti ni lugha.....ahh

    ReplyDelete
  6. Raha ya uchaguzi hiyo. Safi sana.

    ReplyDelete
  7. JIJI LINATENGENEZA BARABARA ZA KINONDONI NA ILALA TU HALINA MPANGO WOWOTE WA KUTENGENEZA BARABARA ZA TEMEKE.

    ReplyDelete
  8. Ama kweli mwenye nacho huongezewa, kuna barabara nyingine hata hizo lami kuukuu hazina....sijui tumlaumu nani mbunge, madiwani au wa serikali za mitaa?

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi,

    Hiyo tambarare unayoisema si kwa bongo yote ila ni kwa baadhi ya maeneo tu tena yale yanayokaliwa na wao (vigogo). Hebu tembelea maeneo kama ya yombo huko barabara ya kwenda buza ujionee maisha wanayoishi watu na mausafiri! Yaani kipindi cha kiangazi hilo vumbi linalotimka utaona huruma kwa raia wakazi wa maeneo hayo hasa watoto maana ni mwendo wa kukohoa na mafua kwenda mbele! Na wakati wa masika kama huu ni tope lililoenda shule....yaani kwa kifupi sio sehemu ya kuishi binadam.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...