Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Rished Bade, wakilinyanyua juu Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza la Barclays , katika mkutano na waandishi wa habari, baada ya kuwasili Dar leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Duh hii sasa too much, hivi huu ukoloni mamboleo katika nchi zetu hutaisha lini? kombe la ligi kuu ya England Tanzania inasaidia nini kama sio ujinga tu? sijawahi hata siku moja kusikia hilo kombe likipelekwa hata scotland au wales kwa wajomba wao, kwa ujinga wa watanzania watasema hilo kombe lipo hapo kuhamasisha mpira wa miguu tanzania hiyo si kweli hilo kombe lipo hapo kahamasisha mpira wa miguu wa ENGLAND na kujaribu kuua mpira wa miguu wa tanzania jambo ambalo ni hatari katika jamii yetu maana kuna baadhi ya vijana watakosa ajira kupitia mpira wa miguu kama kweli wangekuwa wanania ya kweli ya kuhamasisha au kuendeleza huo mpira wa miguu hao BARCLAYS BANK angalau hata wangejaribu kufadhili hata soka ya vijana walio na umri mdogo ili baadaye na sisi watanzania tuje kuwa na timu nzuri ya mpira wa miguu lakini kuja kutuletea huo mkombe ni ujinga tu na kutufanya watanzania tuzidi kuipenda ligi kuu ya england na kujisahau na ligi yetu ya nyumbani sikatai kweli ligi yao ni nzuri na inaendeshwa kwa utaratibu mzuri ndio lakini hicho sio kigezo cha kufanya tuisahau ligi yetu ya nyumbani na kuzidi kuitukuza ligi yao mpaka kufikia kutuletea huo mkombe nyumbani maana kichofanyika hapo ni kuitangaza ligi kuu yao kitu ambacho ni faida kwao maana hapo nyumbani hiyo ligi kuu yao inaonyeshwa kwa kulipia, jamani watanzania tuamke sasa ni wakati na sisi kuifanya ligi yetu iwe na ubora kidogo kama kweli tunapenda starehe ya mpira

    ReplyDelete
  2. UKWELI NI KWAMBA HUO NI MFANO WA KOMBE LA UINGEREZA SIO LENYEWE, TUNAWEZA KULIITA NI LA KICHINA.

    ReplyDelete
  3. wewe ngamaya acha ujinga wako wewe unakaa uk gani mimi niko scotland na nimeisha piga nalo picha na walileta hilo kombe mwana na kama mdau anavyosema ni mfano tu wa lile kombe sio lenyewe original

    ReplyDelete
  4. I second you #1. Hata mimi nimejiuliza hili kombe linaletwa Tanzania la nini? lakini baada ya kusoma point zako nimekubali...Tutaishia kuangalia mashindano ya Nje na kusahau timu zetu za nyumbani. Na vipaji, ajira vyote vitapotea...

    ReplyDelete
  5. PREMIER LEGUE HAPA INAFADHILIWA NA BARCLAYS BANK HATA HAPA HUWA WANALITEMBEZA KWENYE MATAWI YA BANK HIYO HA UK U.K. HATA KWENYE TAWI LANGU HAPO LONDON LILIPITA, SO SI AJABU KUWA LIMEKUJA HUKU KWENYE MATAWI YA BANK HIYO YA NJE YA U.K. SO PENGINE WAKAONA NI VIZURI NA CHAMA CHA MPIRA CHA HUKO WAKASHIRIKISHWA.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli huu ni ukoloni. Hivi kwa nini viongozi wetu ni rahisi kurubuniwa hivi? Je ni ulimbukeni? Ligi ya Uingereza, ni hype kuliko substance, ndiyo maana timu yao ya taifa inastruggle mpaka leo. Tupromote vya kwetu jamani, muziki, kazi za mikono, filamu, michezo.....wakati ni huu.

    ReplyDelete
  7. baada kuomba mue mnaletewa makocha wa timu za uingereza kuwapa darasa makocha wetu once a while mnafurahia kuletewa kombe.kweli mjinga ni mjinga tu.

    ReplyDelete
  8. Wenye akili watamuunga mkono mdau wa kwanza.Ingawaje naipenda sana ARSENAL lakini inafikia muda najiuliza kwa nini kila kitu tufuate na kujilinganisha na hawa mazeruzeru? Huu ni ujinga badala ya kupromote ligi yetu wana promote ligi ya England.Nakumbuka mwaka jana waingereza walitaka baadhi ya mechi zao zichezwe nje ya England kitu ambacho kilikuwa upuuzi na uchu wa hela mtupu kama huu.

    ReplyDelete
  9. Kumradhi, Hivi ni "wakilinyanyua juu au "wakilifunua juu"?? Maana sioni kama kombe limenyanyuliwa juu, pengine ninachoona ni kwamba limewekwa juu.

    Mchambuzi wa Kiswahili.
    (kifimbo cheza)

    ReplyDelete
  10. Wewe mdau wa kwanza kwa jina Ngamanya naunga mkono kwa asilimia zote maoni yako.....lakini jifunze pia kuweka "punctuation mark" ktk maandiko yako.Unatupa wakati mgumu kusoma ujumbe wako mrefu, pasipo kuweka alama hizo muhimu; tunashindwa kupumua.....zamani wapi wewe???!!!

    ReplyDelete
  11. Wewe anon wa tatu acha ujinga wako wewe hapa hatuongelei kuhusu kupiga nalo picha kama wewe unavyodhani hapa tunajaribu kujiuliza kuna faida gani kwa TANZANIA au MTANZANIA kwa hilo kombe kuletwa nyumbani? sasa wewe kama unaona watanzania kupiga nalo picha ndio kitu cha muhimu kwako kaa na ujinga wako huko scotland

    ReplyDelete
  12. SASA HUU NI UJINGA!!!!!!

    ReplyDelete
  13. HII NI AIBU!!!!!.....KWANI HATUNA LIGI ZETU? WAMEPEWA PESA NINI HAO KINA IDDY KIPINGU WATUDHALILISHE KIASI HIKI

    ReplyDelete
  14. zeruzeru si watu???sijamwelewa mtoa maoni anazungumzia zeruzru as positive thing or negative? Im offended nikiwa kama zeruzeru. the fun thing hakuna mtu hata mmja aliyeona hili. tutfika kweli namna hii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...