Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Tawi la Roma unapenda kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliofika kumuaga Marehemu Moses Kiumbi jana tarehe 31 oktoba mjini Roma, kabla ya kusafirishwa kwenda Tanzania. Moses alifariki tarehe 22 Oktoba 2009 kwenye Hospitali ya Umberto I Roma ambako alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kuanguka baada ya kushuka kwenye Bus tarehe 17 Oktoba 2009.
Uongozi unapenda kuwashukuru Watanzania wote waliokuja kwa wingi wakitokea Napoli, Modena na Genova. Viongozi pia unatoa shukurani za dhati kwa Ubalozi wetu wa Tanzania hapa Italy kwa kutusaidia kwa Documentations na misaada mingine mbali mbali.

Marehemu Kesho 2 Oktoba ndio atasafirishwa na ndege ya KLM itakayoondoka Rome Fiumicino Airport saa mbili na dakika kumi za usiku na kufanya Transit Amsterdam kwenye mida ya saa tano asubuhi siku ya jumanne tarehe 3 Oktoba.
Marehemu anategemewa kuwasili Julius Nyerere Airport jijini Dar siku ya Tarehe 3 Oktoba saa tano na dakika thelathini na tano za usiku ambapo atapokelewa na ndugu zake. Mungu amlaze mahali pema ndugu Moses Kiumbi. Kwa habari zaidi na Picha zaidi tembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Tawi Roma hapa:
www.watanzania-roma.blogspot.com
Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Tawi la Roma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. R.I.P Moses

    ReplyDelete
  2. Kaka michuzi naungana na wote waliofikwa na msiba huu mzito wa mtanzania mwenzetu. POLENI NDUG ZANGU, KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA,YEYE ALIMTOA KWETU MOSSES NA YEYE AMEMTWAA, JINA LAKE LITUKUZWE.
    Kaka ila nimesikitishwa na mtu aliyetoa tangazo hilo kuhusu kiswahili alichotumia. Ukisoma vizuri na kisha kutafakari zaidi, unapata uchungu mara mbili, ninasema hivi kwasababu ifuatayo; sijapenda kiswahili alichotumia na sidhani kama kuna kiswahili cha namna hii kwetu Tanzania kusema..... marehemu anatgemea kuwasili..... saa... na atapokewa na..... Kaka Michuzi sidhani kama hiki ni kiswahili fasaha (hata kama ujumbe umefikishwa), ninaamini lugha nzuri ilikuwa... mwili wa marehemu utawasili... na utapokelewa na ...... nadhani hiki kingekuwa kiswahili fasaha kidogo.
    Samahani kwa kutoa mawazo yangu katika tangazo.

    (nami nikotayari kusahihishwa)

    ReplyDelete
  3. mzee misupu vp tena,october ipi tena unayozungumzia hapa au ndio siku zarudi nyuma?poleni sana wafiwa.Mungu ailaze roho ya mareheu mahali pema.amin

    ReplyDelete
  4. Tarehe jamani mbona mnatuchanganya tu! hakuna editor??????????????!!

    ReplyDelete
  5. Asante ndugu hapo juu kwa kusahihisha kwako..Kipindi hichi si cha kulalamika sana. Aliyeandika alikuwa anania nzuri tu. so naomba hata kama kuna kajikosa kadogo muhimu ujumbe umefika.Poleni sana.

    ReplyDelete
  6. NAONA KAKA MICHU ALIPITIWA KIDOGO KWENYE TAREHE..LAKINI NDUGU TUSILAUMU SANA MUHIMU UJUMBE UMEFIKA! R.I.P Moses.

    ReplyDelete
  7. R.I.P Moses.

    ReplyDelete
  8. poleni sana wafiwa ndugu jamaa na marafiki bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe alimpenda lakini MUNGU alimpenda zaidi poleni sana wapendwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...