Mwalimu Msuya Shaabani ( kulia) ambaye ni mke wa mmoja wa wafugaji wa kabila la kisukuma akionyesha ishara eneo la makazi yasiyorasmi ya wafugaji wa kabila hilo ambao watoto wao wamelazimika kuwapatia elimu ya darasa la kwanza ndani ya msitu wa hifadhi ya asili wa Nanji, katika kijiji cha Igumbiro, Tarafa ya Lupiro, Wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro, kama walivyokutwa juzi msituni humo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machiibya , (wapili kushoto waliosimama mstari wa nyuma) , akiwa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Ulanga wakishanagazwa na kuwepo kwa darasa la kwanza la watoto wa jamii ya wafugaji wa kisukuma ndani ya msitu wa hifadhi ya asili wa Nanji, katika Kijiji cha Igumbiro , Tarafa ya Lupiro, Wilayani Ulanga , zaidi ya kilometa 12 toka kijijini, wakipatiwa elimu na mwalimu asiyerasmi Msuya Shaaban ,kuwawezesha kujua kuandika, kusoma , kuhesabu na lugha ya kiswahili. Picha na John Nditi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hapo ndio wajue kuwa wazalendo bado wapo nchi hii, wao wa level ya juu tu ndio wanatuangusha....

    ReplyDelete
  2. tunaposema bongo tambarare tukumbuke bado kuna maisha kama haya,tusibweteke na vikwangua anga vya wahindi kariakoo

    ReplyDelete
  3. Pongezi kwa mwalimu wa kujitolea Mwl. Msuya.....naomba serikali ya mkoa iwajengee banda la kusomea watoto wale....hapo tunao akina kikwete wengitu.

    ReplyDelete
  4. Mahali penye mkusanyiko wa binadamu kama hapa vitu muhimu vya kuangalia ni huduma muhimu kama choo, jengo litakalowalinda kwa mvua na jua na maji salama ya kunywa. Kama choo hakuna, ni wazi wanamalizia shida zao majanini, ukikangalia waliovaa viatu hapo ni wachache sana, miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru hali ni kama hii.

    ReplyDelete
  5. Ndio maana TZ ni maskini mpaka leo. Angalia watu 4 wa mwanzo walivochangia. Ni kama wanawapa moyo walimu kwa kazi ngumu wanayofanya badala ya kukemea system nzima ya nchi yetu ambayo imeshaoza na kusababisha matatizo yote tunayojionea kila kukicha. Mungu tusaidie.

    ReplyDelete
  6. huyu mkuu mkoa hua habidilishi hiyo suti?la

    ReplyDelete
  7. JAMANI WANANCHI WENZANGU HII PICHA MNAVYOONA INATIA HASIRA NA HURUMA NA JAZBA KUWA HADI LEO HII KUNA WATU TZ WASIO NA VIATU YAANI WANAPEKUWA!!! HALI HII INA SIKITISHA SANA KUTWAAA MNAWAONA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU KWENYE PICHA, WAKIKATA RIBONI NA KADHALIKA WAKATI WATOTO KA HAWA HAWANA HATA LAPA MGUUNI!! KHAAA NI AIBU SANA TENA SANA! VIONGOZI WA TZ MTAAMKA LINI USINGIZINI??? AMA MTALALA MAISHA?????

    ReplyDelete
  8. anon wa Nov 24, 03:47:00 AM, unafikiri 'walimu' hao hawastahili pongezi? unahisi nani anawalipa kuwapatia japo elimu brashi hao vijana? kwa mtazamo wako, unafikiri maisha yasimame kusubiri hiyo system inayokemewa itengemae? mwisho kabisa, wewe binafsi unafikiri unaweza ukafanya kujitolea hata siku moja kwenda kuwapiga brashi hao vijana huko waliko?

    Tafakari....

    ReplyDelete
  9. Michuzi tx 4 this blog...Nipo hapa saa tisa usiku nasearch online toys za kumnunulia mwanangu ....nimeingia kwenye blog yako nimeona hii picha machozi yakanitoka.... Yaani nimewaza sana kwanini hawa wazaliwe kwenye mazingira hayo etc etc..imebidi hata niache nilichokua natafuta...my nephew hii picha lazima aione kesho...kila siku nataka hiki nataka hiki..ukimnunulia tu rangi asiyoipenda basi ametupa na hataki kabisa kugusa...wakati wengine hata shule wanasoma kwenye national park..jamani...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...