Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association bwana Saleh Jaber (kulia) akiwa katika maonesho ya Arts akimpa tafu Mbongo mwenzake kwenye fani ya uchoraji bwana Eddy Raza (shoto) ambaye mwakani anachukua nondo kwenye fani ya uchoraji kwenye chuo kikuu cha uchoraji mjini London.Katikati ni mgeni wa heshima katika maonesho hayo, bwana Tim Allen wa kutoka chuo kikuu cha uchoraji mjini London.
Eddy amenaswa akiwa anachukua picha ya moja ya kazi zake alizozileta katika maonesho hayo ambayo yalifanywa kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake watatu kutoka chuo kikuu cha uchoraji jijini London.

kuna mzee alikuwa anaitwa raza alikuwa pale mwenge ni mchoraji mzuri sana je ni baba yake?
ReplyDeletekama ndiye, je bado nae anachora? maana mwaka huu nilikuwa dar nilijaribu kumtafuta sikumpata.
Edna
Asante kaka michuzi kwa kutuletea huyu ndugu yetu.
ReplyDeleteEddy mwana mambo super kinoma nakwaminia.. Kipaji ndugu yangu unacho achana na wanga wasionampango.
All the best mungu atakujalia inshallah
AMIN
Mdau UK
bosi nakutafuta sana , simu yako sina na kila nikija mitaa ya barking sikupsti wala sijajua pa kukupata , ukipata ujumbe niandikie kwenye donmicky@yahoo.co.uk muhimu sana
ReplyDeletekuhusu fani hio nakuaminia, watachoka wao, ma abstract , ma nini wao tu
thx
huyu ni mtoto wa Mzee.Raza wa mwenge, ambaye naye ni mchoraji mahiri sana !.Eddy wasiliana nami kwa mmzushi@yahoo.com.ni muda mrefu sana hatujaonana.
ReplyDeleteNdio mwana wachawi wajinyonge. Rizki atoae ni m.mungu. Wamesiliba mpaka wamechoka na kichaa wangu unatwita. Hamna mungu mtu. Wajipendekeze sasa. Endelea na sisi wajuba tupo nyuma yako kama kawaida.
ReplyDeleteWakati ni huu walitaka ukabebe maboksi hali kipaji unacho. Hongera kubakia na bilivu na kila heri.
Mdau UK