Lady Jay Dee akitumbuiza kwenye mnuso wa Mo Ibrahim usiku kuamkia leo ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar
Jide na madansa wake wakiwajibika
JK, Dk. Salim Ahmed Salim na Mo Ibrahim wakimshangilia Jide
JK akiwa na Jide na Gadna G. Habash kwenye hafla hiyo. JK alisikika akimsifu Jide kwa kufanya vyema jukwaani na kumpa changamoto alenge waliko kina Youssu Nd'our na Angelique Kijo katika anga za kimataifa
Youssou Nd'our akiwa kala konozzz na JK na Jide ambapo alimpongeza Jide kwa kipaji na kumtaka akaze buti.
JK akimpigia ndondogo Jide kwa Yossou Nd'our ili naye awe wa kimataifa. JK alisikika akimwambia mwanamuziki huyo wa kimataifa toka Senegal kuwa msaidie kijana wetu huyu apasue anga za kimataifa. Nd'our, ambaye kumbe ni rafiki wa siku nyingi wa JK, alifurahi sana na akasema atalifanyia kazi swala hilo. Jide oye!
Picha zingine nenda kwa Jide







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. jamaa kabeba pochi hapo.lol

    ReplyDelete
  2. kwani akibeba pochi tatizo liko wapi? ulitamani uibebe wewe?

    ReplyDelete
  3. jamani mimi mbona bado sielewi.
    hii kokuteli pati ni ya kuhusu nini hasa.
    And who is Mo Ibrahim?
    Nitashukuru sana kama kuna mtu ataweza kutuelezea.

    mdau
    Nje ya nchi

    ReplyDelete
  4. anon hapo juu umenchekesha! ,lol na bado!

    ReplyDelete
  5. Huh nakuaminia dadaa Jide...!!!
    Mungu alikunyima mengi lakini sauti, vipaji,ability to stay well focused unatisha. Keep it up wangu, hata mie music yako huwa inanikuna saana tu.

    ReplyDelete
  6. cha ajabu ni nini? beba la wako nawe hujakatazwa lol.

    ReplyDelete
  7. ndiyo kabeba pochi si ya mkewe kama wewe hujui ustaarabu utajiju ulitaka akapafomu na pochi?? acha hizo ushamba mwingine bwana hongera jide utafika mbali zaidi ya hapo jitaidi tu kuwa mbunifu

    ReplyDelete
  8. Gadna anashow some Love kwa kubeba pochi ya Wife safi sana

    ReplyDelete
  9. Hongera sana jide, wewe ni kichwa hakika tunajivunia wewe. nakuomnea ufike mbali na mungu akulinde.

    umependeza sana halikadhalika mr.

    Jamani kubeba pochi ni kawaida sana na ni mapenzi tu wala sio kama ulivyowaza wewe hapo juu.

    mungu mbariki jide, mungu ibariki tanzania.

    maida

    ReplyDelete
  10. Mhh ndugu Maida kwa kweli Jay Dee hajapendeza, tena mimi naona kama anachekesha, huyu dada anaimba vizuri sanaaa ana sauti na anajituma kiasi. Kuvaa ni ZERO inabidi apate mtu wa kumsaidia kuvaa hajui anatakiwa kuvaa nini huwa anachekesha sana anavyovaa, shape na sura yake haviendani na nguo zake, hajui kuvaa na wala hapo juu hajapendeza hata kidogo anachekesha, hiyo function na jinsi alivyovyaa mhhh hakuna kitu hovyo kabisa. Ila kazi yake ni nzuri

    ReplyDelete
  11. heee jamani mbona wengine mwamshambulia annon #1???amesema tu ivo wengine mwaaza lecturez puuh?safi sana Gadner

    ila JK poa sana ila uyo askari wake ndo nn kuvaa migwanda?kaambiwa apo sooo official or what?kwanza ilikua all black suit event

    ok Nd'our cjawai msikia afu hii cjui kutoa zawadi kwa mapresidaa afrika SIJAIELEWA KABISA nielimishwe wadau

    ReplyDelete
  12. wee Mdau Unaeuliza who is Mo just google ya self an u ll c who hes

    ReplyDelete
  13. mmmmmmmmmmmh, wewe uliyenibu nakushukuru, ila naweza kusema kuwa "KIPENDA ROHO HULA NYAMA MBICHI, AU UKIPENDA CHONGO UTAITA BORITI"

    Basi mimi namuona jide yuko ok hata kimavazi, kwa ujumla ana muonekano mzuri sasa kama wengine hawavutii basi samahani.

    me nasema JIDE UKO JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU, KAZA BUTI DADA,

    maida

    ReplyDelete
  14. mmm kweli wabongo mna mambo kwani gadna kubeba pochi ya jdee imekuwa kosa?

    ReplyDelete
  15. Watasema sana ,lakini mie namkubali Lady Jay dee- ni mwanamuziki maridadi sana katika fani,kuimba lugha 7 tofauti sio mchezo kati karne hii.
    Nae asiye mjua Mo Ibrahim-yuko sayari gani jamani?
    mdau wa Lisungo Ipinda Kyela.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...