Hello Ndugu Michuzi!
Naitwa Daniel, ni mtanzania niliyepo Korea ya Kusini nasoma.
Niliingia kwenye mgahawa (coffee bean) hapa jijini Seoul, kupata kawaha kidogo manaake hivi sasa huku baridi ya kufa mtu.
Nikakuta tangazo ambalo linaloonesha kuwa ati mlima Kilimanjaro upo Kenya na kwamba kahawa ya Kenya inalimwa maeneo hayo. Nakutumia picha ya tangazo lenyewe uwahabari watanzania wenzetu waone tunavyonyongwa na hawa watani wetu wa jadi.
Mdau Daniel,
Seoul –Korea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Sidhani kama watani wa Jadi wamesema kama Mlima uko Kenya, walichosema ni kwamba kahawa yao inalimwa kwenye slope(mteremko) ya mlima Kilimanjaro, jambo amabalo pengine ni kweli, kwani upande wao pia wanayo slope wa mlima Kilimanjaro...Kwa mawazo yangu nadhani wako sahihi.

    ReplyDelete
  2. Jamani ebu tuwe serious Kidogo! hawa wakenya ndio zao mimi huku Italy nilishabishana sana na wataliano kuhusu juu ya mlima wa kilimanjaro. Wenyewe wanasema eti upo kenya? ujue wakenya wanautumia sana huu mlima wetu kuvutia Watalii?? shida iko wapi? tunaweza kusema wajinga au ni wanjanja? infact bahati mbaya hatutapata nafasi ya kukutana na raisi kulingana na ratiba yake kuwa busy hapa Roma, otherwise nilikuwa nataka kumuuliza swali hili, serikali yetu ya Tanzania inachukua hatua gani zikisoma na kusikia wananchi wanalalamika kuhusu hii issue ya Wakenya kutangaza mlima upo kwao? tunawachekea tu then wenzetu wanaingiza hela au la? naomba wadau mchangie sana..mimi kama Mtanzania naumia sana kuona wenzangu wanashida ya njaa kumbe wanjanja ndio wanasababisha!! Siku njema!

    ReplyDelete
  3. Hii haina madhara yeyote kitalii, ni kama IPP wanaposema maji ya Kilimanjaro yanatokana na chemchem ya mlima Kilimanjaro, ni promo tuu, ubora wa kahawa unatokana na mbegu, matunzo na ardhi nzuri, sasa mtu akisema kahawa yangu nalima eneo fulani haiwezi kuwa sababu kuu ya kuwa kahawa bora.

    ReplyDelete
  4. acheni tu watusaidie kuu adivataizi manake sisi tumeshindwa mwisho wa siku hao watalii wakija africa watajua ukweli ila kwa sasa acheni tu watusaidie kuutangaza sisi hatuwezi na hatujui

    ReplyDelete
  5. Hiyo isiwasumbue sana zamani walikuwa wangesema kahawa kutoka mlima Kilimanjaro ulioko Kenya, siku hizi wanasema kutoka miteremko na bondeni mwa Kilimanjaro baadae wakikua waataacha sababu ya search engines kama google zinawaumbua... Mtu akikubishia mwambie aende ku-google wala msibishane atapata majibu yake.

    ReplyDelete
  6. EMBU SOMENI HII LABEL KWA MAKINI KABLA YA KUANZA KUCHANGIA KWA SABABU MNIWEZE MKAWA MNACOMMENT KITU AMBACHO SIO SAHIHI.

    NI WAPI PAMEANDIKWA "KILIMANJARO" KWENYE HIYO LABEL? LABEL INASOMEKA KILAMANJARO.

    KWA KWELI MLIMA KILAMANJARO SIJUI UKO WAPI.

    KWA NJIA HII HATA UKIENDE MAHAKAMA MTABISHANA SANA HUKO.

    ReplyDelete
  7. Kahawa ya kwenu iko wapi? bora hata wao wanamanage ku export kahawa ya kiwango. Hapa Belgium kahawa za Kenya ziko kila mahali, Sijawahi ona kahawa ya kibongo Halafu kazi yenu kulalamika tu Ooooh MLIMA!!!!!!!! wa kwenu ndio lakini kama hamuutumiii ipasavyo wao wautumie umarufu huo

    ReplyDelete
  8. Kwaukweli hakuna sehemu inayosema Mt.Kilimanjaro uko Kenya. Ila unaweza kuwa na little effects on perception of individuals. Na yule anon wa 10:40:00 AM aliyesema hii kuwa haitapunguza haina madhara yoyote ya kitalii usiwe unalopoka elewa kwanza shughuli za taratibu za kitalii then lopoka sawa.

    Watalii popote wanapotoka wakawa wanakuja kuona mlima Kilimamnjaro wakashukia Kenya then wakavushwa mpaka kuja Tanzania basi wale watalii wanaesabiwa ni wa Kenya na pato kubwa la utalii linaingia kwao.
    Kenyan trying to articulate thier Marketing strategy in smart way kiasi kwamba ukitazama kiundani wanatushinda. Kwa mfano wanaposema in Kenya u can have a better view of Mt.Kilimanjaro na wanatoa picha ya mlima kilimanjaro na picha za twiga na pundamilia kama wewe kweli unania ya kuona mlima kilimanjaro live where will you go? Tanzania uliko ambako hawasemi lolote kuhusu mlima japokuwa uko kwao au utaenda Kenya to have a better view na kuona wanyama waliopo kwenye mwinuko wa chini wa mlima?

    Watanzania kuamka siyo kuwazuiya Kenya haki yao ya msingi ya kusema kile wanachoona kinafaidisha nchi ila na nyinyi mbuni mbinu mpya ya kuutangaza mali zenu sawa. Halafu wengi wanaoandika humu baba zao au ndugu wa karibu wana nyadhifa kubwa tu na wanaweza kuwa influencial kwa gov kutake measure lkn greedness and selfishness imewatalawa na tutakuwa mashini daima.
    Mtanzania wa kweli.

    ReplyDelete
  9. Kilimanjaro is not part of a mountain range, but rather a single free- standing mountain which rises like a lone warrior above the plains of Tanzania and Kenya.link http://www.indigoguide.com/kilimanjaro/kili-facts.htm

    AND

    Mount Kilimanjaro is situated entirely within the borders of Tanzania, although it is situated close to the border of Kenya. link
    http://www.mtkilimanjarologue.com/mt-kilimanjaro-facts

    Yule aliye-suggest mtu akikuuliza mwambie aingie google hizo ni baadhi ya links tu which one is accurate assume wewe si mtanzania na trying to find the truth about Mt.Kilimanjaro.

    VERY CONFUSING INDEED
    THANK YOU!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. Sie wabongo kwa maneno mengi hatujambo! Hii ndio Dunia ya kisasa ukizubaa kidogo umelaliwa. Tukikaa kubishania hilo tangazo tunazidi kupoteza muda kwani hapo hakuna la kulalamikia hata tukienda mahakamani ushindi hamna.Tusome kwa makini na tuelewe changamoto iliyopo badala ya kubwabwaja wa Tz wenzangu.

    ReplyDelete
  11. Slopes/Mteremko wa Mlima Kilimanjaro unafika mpaka Kenya na tangazo liko sahihi kabisa. Fikiria zaidi hakuna mashamba yoyote yanayozunguka pale juu mlimani lakini mteremko wake ni mrefu sana wilaya nyingi za mkoa wa Kilimanjaro ziko kwenye slope za mlima huo. Na kwa upande wa kenya wilaya za karibu na mlima pia ziko kwenye slopes za mlima kilimanjaro. Kama umetokea Kilimanjaro hilo utalijua maanake hata kama kwenu ni mbali utaona jinsi ardhi inavyonyanyuka kuelekea mlimani.

    ReplyDelete
  12. Sawa sawa mdua. cha msingi tutangaze mlima wetu .. na kiusisitiza kuwa Kilimanjaro upo Tanzania.. period... tuache kulalamika lalamika.. manake mdau anasema kinamuuma sana .. sasa kinakuuma nini? chukua hatua..na serikali ichukue hatua ni simple marketing tuu hapo .. yeah tukilala wengine watatake advantage ... watanzania tuacvhe ulalamishi.. take responsibility.
    Mdau , USA

    ReplyDelete
  13. VILEVILE NATAKA KUSEMA KUWA UCHUMI TUNAO LAKINI TUMEUKALIA,
    VILEVILE HAWA JIRANIZETU WANATUCHEZEA SHERI ATI MLIMA UKO KWAO JAMBO HILI NSHAMWAMBIA HATA SITI KUWA LANIKASIRISHA.

    HAHAHAHAHAHA ACHENI WAKENYA WAFAIDI MALI YA AFRIKA NI WAAFRIKA WENZETU KUNAUBAYA GANI WAKIFAIDI MANUFAA YA MLIMA TUSIOUFANYIA KAZI.

    NADHANI TUNGEWAPA WAKENYA MLIMA WAFANYIE KAZI HALAFU WATUPE 50% YA MAPATO.

    ReplyDelete
  14. swala la mlima Kilimanjaro na utata kuhusu ni wapi kweli mlima uliko ni kwa sababu ya uzembe na kutokua na nia hasa wizara ya utalii na barozi za Tanzania kujitangaza kibiashara na kuacha Kenya kufaidika kwa mamilioni ya dollar kwa mgongo wa vivutio vya utalii visivyo nchini mwao. Swala la utalii innabidi lipatiwe kipaumbele na serikali iwe tayari kughalimia matangazo kwenye Cable network kubwa za kimtaifa "as a promotion of mount Kilimanjaro in Tanzania. Angalau wameanza kufanya hivyo hapa USA " CNN".Na sisi watanzania tuwe mabalozi wazuri wa kutangaza nchi yetu kama Wakenya. Kuna watalii wataondoka kwenda Tanzania mwakani baada ya mke wangu kuniambia kwamba waende nchi kagani africa baada ya Kenya hasa kuangalia Mt Kilimanjaro" niliomba nitoe lecture free of charge kuhusu vivutio africa na kutoa utata kwamba hakuna haja ya kwenda Kenya maana mlima uko Tanzania, they were so sceptical ,but" Watakwenda tanzania baada ya kuwaelimisha. it's a group of 10 people. Let be good amssadors"

    ReplyDelete
  15. usipoteze muda wako na Tanzania....yaani we fanya mambo yako popote pale ulipo na kula maisha kivyako maana mchawi wa kwanza wa Tanzania ni viongozi we wategemea mwananchi utafanya nini zaidi ya kulalamika kila siku...
    NOTE...naanzisha programe ya kutangaza biashara na utalii wa Tanzania then ntawapa feedback hapahapa kwa anko nanihii jinsi viongozi watakavyoiblock hiyo programe kisa hamna 10%.

    ReplyDelete
  16. COME TO KENYA A COUNTRY THROUGH WHICH YOU CAN VISIT SERENGETI, NGORONGORO AND A BETTER VIEW OF MOUNT KILIMANJARO. NAIPENDA KENYA YANGU WATANZANIA BADO MUPO MUMELALA USINGIZINI. NA TUKIWA JUMUIA NDO BAAASI TENA

    ReplyDelete
  17. Hivi kwa mfano tukiamua kuweka unafuu kwa mtalii anayekuja moja kwa moja Tanzania na kuwapiga bei kali wale wanaoingia kwa kupitia Kenye kwani kutakuwa na nini! nani atatushitaki?
    Hawa jamaa wanatumia mwanya kwamba njoo kwetu utauona Mt Kilimanjaro. wanafikia kwao halafu wanawaleta kwetu wanawazungusha kisha wanarudia nao.
    Yaani kuoa tuoe sisi wao wale kombe la solo. Hii kitu ifike mahali iishe.
    Wee balazo print haya maoni uwape hao jamaaa wa Maliasili. Si ajabu wao wanaona kawaida. si wanapata mshahara wao kila mwezi?

    ReplyDelete
  18. Moimi niliwahi kuchukiwa na mkenya kisa nilisema kuwa mlima K'njaro uko Tz na sio Kenya. Alinijia juu na kusema nisitake kumpotosha alivyofundishwa na mwalimu wake. Eti alifundishwa kuwa mlima K'njaro upo katikati ya Kenya na Tz.
    Na matangazo mengi tu ya utalii yanayotoka Kenya yanautangaza mlima K'njaro.
    Kazi kwetu kujitoa muhanga ktk kujitangaza. La sivyo inakula kwetu. Wao wananeemeka. Tunashindwa hata kuwatumia hao ma supper star wanaokuja kinyemela ktk kuutangaza utalii wetu. Matokeo wanakuja kimya kimya na kuondoka kimya kimya. Tunachokiona ktk Tv ni nyumba za udongo, njaa na vita tu kuhusu Afrika. Hivi hata BBC hakuna m tz atusaidie kujitangaza?

    ReplyDelete
  19. Come on guys, lets drop it.. I dont see Kilimanjaro mentioned on the post. Its Kilamanjaro and I dont know what that is. Leave Kenyans alone, blame it on your leaders with big tumbo.

    ReplyDelete
  20. Watanzania mkaweke matangazo ya biashara, utalii na mazao ya viwandani ktk uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge jijini London.

    Maana Chelsea ndiyo yenye inayoingiza watazamaji matajiri kupita klabu yoyote Uingereza. Kipato cha wastani cha mashabiki wa Chelsea kinawatosheleza kufanya utalii, kupromoti bidhaa kama kahawa iliyokwisha sindikwa n.k

    Watanzania tusikae kupiga kelele wakati 'mnofu wa nyama unatuozea mkononi'. Abramovic bilionea alivutiwa kuja Tanzania, sasa baada ya ujio wake, ni mikakati gani imefanywa ili tupate ya zaidi ya ujio wa Abramovic?

    Kazi kwenu watu wa TTB, Wizara utalii, wizara biashara, Vyama ya Ushirika vya Kahawa, wenye mahoteli, na mtanzania mfanyabiashara.

    Mdau
    Marangu. Moshi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...