Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle (pichani) akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Chifu Marealle 2009 leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO akizungumzia mashindano ya Kombe la Chifu Marealle II kwa mwaka 2009 ambayo amesema yatazinduliwa rasmi Mjini Moshi tarehe 9 Disemba ili kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Uhuru.

Aggrey Marealle amesema mashindano hayo yatapambwa na maandamano yatakayozihusisha timu zote shiriki na washabiki kutoka kata 17 za Manispaa ya Moshi hadi Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCOBS) ambapo mechi ya ufunguzi itachezwa.

Marealle amesema zaidi ya timu 20 za soka, na timu 10 za netiboli kutoka wilaya za Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha, Hai na Vunjo zote za mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu. Mashindano hayo yatafanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Moshi kama vile Pasua, Ikulu KDC, Majengo na viwanja vya George Memorial. Fainali zitafanyika katika uwaja wa MUCCOBS siku kumi baada ya uzinduzi.

Marealle alimema washindi watapata zawadi kabambe na za kuvutia na akaongeza kuwa mashindano hayo yatahusisha watu kutoka Nyanja mbalimbali na watashiriki katika michezo ya vijana kama vile soka na netiboli pamoja na michezo ya kujifurahisha kwa ajili ya wazee kama kuvuta kamba, kukimbia na gunia na kufukuza kuku.

“Mashindano haya yana lengo la kumuenzi Chifu Marealle akiwa ni kati ya waliotetea uhuru wa Tanganyika na kama mwanamaendeleo aliyechangia kuleta maendeleo mkoani Kilimanjaro. Marealle pia ameongeza kuwa mashindano hayo yana lengo la kuwakutanisha vijana pamoja na kushiriki michezo ili kuweka afya zao katika hali nzuri, kuwa na nidhamu, kujifunza sifa za uongozi na kuendeleza michezo kati ya vijana nchini”, amesema Marealle.

Mashindano hayo pia yanatumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwafundisha vijana jinsi ya kuishi maisha bora. "Tunaamini kuwa mashindano haya yataunganisha watu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuweka msingi imara wa vijana na maendeleo ya michezo na kuchangia kutoa elimu kuhusu Ukimwi.
Mwaka 2008 maandamano ya uzinduzi na kufunga mashindano yalikuwa na wanamichezo zaidi ya 700 na wakati wa mashindano pamoja na fainali watazamaji wapatao 7,000 waliudhuria mashindano hayo ambapo Mkuu wa Mkoa wa wakati huo Mhe. Mohammed Babu alikabidhi zawadi zikiwemo pesa taslimu shilingi 600,000, ng’ombe, vifaa vya mpira wa miguu, mipira na kombe la kifahari kwa washindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kweli bongo sio mchezo,unaweza kubuni kitu fulani ukatengeneza mikwanja,watoto wa chifu fundikira mpooooo?dili hilo,anzisheni na nyie Tabora ni hela tupu hizo,waswahili wanasema kufa kufaana,amkeni familia za ki chifu,hela hiyo mwenzenu amebuni,baadae kutakua na mechi za koo za machifu,mtatengeneza,dili hilo.

    ReplyDelete
  2. Sio vibaya kumuenzi Chifu Marealle.

    Lakini pamoja na kumuenzi huko, historia ya "Tanganyika" na Tanzania ni lazima iandikwe kwa uwazi bila kuipotosha!

    Kuambiwa kuwa "...Chifu Marealle akiwa ni kati ya waliotetea uhuru wa Tanganyika...wengine tunasita kutamati hivyo!

    Tunakubaliana kwa kusema, "kama mwanamaendeleo (Chifu Marealle) aliyechangia kuleta maendeleo mkoani Kilimanjaro."

    Huyo Chifu Marealle, wakati Julius Nyerere anakwenda Umoja wa Mataifa, Gavana Edward Twining alimtuma eti aeleze msimamo wa Tanganyika mpya (kulingana na matakwa ya Mkoloni).

    Chifu Marealle aliliambia Baraza la udhamini la Umoja wa mataaifa kuwa Tanganyika haikuwa tayari kujitawala.

    Badala ya kudai uhuru, Chifu Marealle alidai tupewe mahindi...ikiwa ni pamoja na siri ya chini chini ya uhuru wa Kilimanjaro (Wachagga)!

    Tunawasikia watu wakijitokeza kusema yale ambayo hatukuwahi kuyasikia wakati Julius Nyerere akiwa hai! walikuwa wakingoja kumdanganya nani?

    Mwingine: Ujamaa wa Nyerere zilikuwa ni "ndoto"!

    Wengine, Nyerere kawanyang'anya Waislamu uongozi wa kuleta uhuru!

    Na mwingine: Baada ya Nyerere kukataa pendekezo la Benki Kuu ya Dunia (hapo nyumbani kwake Msasani), alienda nyumbani kuandika barua ya kujiuzulu u-waziri wa fedha.

    Huyu hatuambii wazi kuwa Nyerere alipowaacha hapo sebuleni ilikuwa ni ishara kuwa kamfukuza kazi kwa kuhujumu uhuru wa Tanzania akishirikiana bega kwa bega na (na kutii amri kutoka) Benki Kuu ya Dunia, mjini Washington, DC!

    ReplyDelete
  3. Nasikia Liverpool watashiriki kombe la Marealle baada ya kutolewa UCL.Unaweza ku confirm tetesi hizi anko???

    ReplyDelete
  4. Haya mambo ya bongo haya, wasambaa nao waanzishe kombe la Kimweri, wahehe la mkwawa, wanyamwezi la Mirambo na wasukuma la Makwaia

    ReplyDelete
  5. Jamani this is just a cup hamna political agenda yeyote! Alipotawazwa chief wa Wasukuma hamkupiga kelele while hapa ni tamasha tu kama Kilimanjaro Marathon ili kukuza utalii

    ReplyDelete
  6. Hakuna siasa hapa!

    Maana ya "ni kati ya waliotetea uhuru wa Tanganyika" ni nini, kama si siasa, per excellence?

    Hata ya Wasukuma nayo yamepitwa na wakati kwa viongozi kuchaguliwa kwa miktadha ya kitanda badala ya kura!

    ReplyDelete
  7. IF THERE WAS NO POLITICAL AGENDA THEN HOW COMES ON EARTH ISSUE YA MOSHI IJE ITANGAZWE MAELEZO KWENYE VYOMBO VYOTE VYA MEDIA VYA TANZANIA NA VYA NJE, NI UTOTO, JUST LOOKING FOR CHEAP PUBLICITY. LAKINI SI SHANGAI NDO ZAO HAO, NI HUYU ALIENDA UN KUSEMA TANGANYIKA BADO MUDA WA KUJITAWALA NA NI HUYU HUYU ALITAKA KILIMANJARO IPEWE UHURU WAKE PEKEE, KAMA VILE
    KWAZULU NATAL BONDENI ILIKUWAGAWA WATANGANYIKA WASIWE NA SAUTI YA PAMOJA, NAYE MWNGINE ANASEMA ALIJIUZURU UKUU WA PESA KUMBE ALIFUKUZWA NA MCHONGA NA BENKI YA DUNIA KUONA WAMENYOFOLEA KITUMBUA CHAKE BASI WAKAMPE NAFASI YA KAZI KUMPOZA NA KUFICHA UOVU WAO

    ReplyDelete
  8. Swala si ya kuwa ati so and so alifukuzwa kazi na Mchonga suala ni kuwa ukiwa Rais sikiliza mawazo ya wataalamu! Mchonga huyo huyo unaemwabudu kama Mungu alijiuzulu miaka mitano baadae kwa aibu na ili kupisha mabadiliko ya kiuchumi kwa vile aliona aibu kumeza matapishi yake ya Ujamaa!

    Na kuhusu ati Huyo Chief Marealle ati alipinga uhuru Tanzania hizo ni propaganda zisizo na kichwa wala miguu! Misupu unaweza ukaweka kwenye blog yako hapa speech aliyotoa huko UN archive zipo! Tuache chuki zisizo na msingi! Na hata kama kabila lake lilikuwa resistant kujiunga na TANU mwanzpno hiyo ni rebellion nature ya watu wa Kilimanjaro hawaburuzwi tu na ukumbuke walikuwa na utawala mzuri na ilibidi wapime faida na walipoona faida walimuunga mkono huyo Mwl Nyerere na kumpindua hata huyo chief wao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...