Mbunge wa Singida Mh. Mohamed Dewji akisakata ngoma na bendi ya Twanga Pepeta iliyokuwa inatumbuiza uwanja wa Namfua Singida karibuni. picha na habari zaidi nenda kwenye libeneke lake kama ilivyooneshwa hapo chini

Kaka Michuzi,
Ninakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya ya kutupasha habari mbalimbali za kijamii. Ningependa kuwaomba wadau mtupe ushirikiano wa kutoa mawazo na pia kuitembelea blog yetu ya Mhe. Mohammed Dewji "Mo", ambapo tutakuwa tunapeana habari mbalimbali na pia kujadili masuala mbalimbali yanayohusu jamii yetu ya kitanzania.
Blog hii ni changa lakini ninaamini tutafika mbali kwa msaada na ushirikiano kutoka kwa wadau. Vile Vile Mo atatumia uwanja huu kujadiliana na wadau jinsi ya kuboresha na kuleta maendeleo ndani ya jamii

Tovuti yetu ni
www.mohammeddewji.com
na blog yetu ni
----------------------------------
Globu ya Jamii inampongeza Mh. Mohamed Dewji kwa uamuzi wa kuanzisha libeneke, ikiwa ni njia mojawapo ya kupasha na kupata habari kwa njia ya kisasa ambayo ni ya haraka na isiyongoja kesho. mambo ni papo kwa papo. Natumai Wah. wengine, ambao bila shaka wana kigugumizi endapo kama kuna haja ya kuanzisha libeneke ama la, wataiga mfano huu. Hongera Mo.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Unajua Mh Mo anajua kula na vipofu,unafikili wananchi wanataka makubwa basi,unafikili matatizo ya jamii ya waliowengi ni makubwa basi,unafikili mategemeo ya wananci kwa viongozi wao ni makubwa kiasi hicho.Tatizo hata hicho kidogo baadhi wanashindwa kukitimiza.

    Mimi binafsi namkubali Mbunge huyu,sijali waosha vinywa watasema nini ila ukweli unabaki pale pale,kwamba hata kukaa na waliokuchagua, kuwasikiliza na kutatua baadhi ya shida zao kwenye huduma kuhimu za kijamii inatosha kabisa,na hapo ndipo nampatia big-up Mh Mo.

    Sisemi yeye hana matatizo yake,ebu niambie nani msafi asiye na matatizo,wewe,hapana,wazazi wetu,hapana,wachungaji,hapana,maaskofu,hapana,mashehe, hapana.Kumbe soote tu matatizo.Ninachoongelea hapa ni wepesi,ni udogo wa matatizo ya huyu Mh.Naongelea yale ninayoyajua mimi kwayo nipo tayari kubadili msimamo kama nitajihakikishia matatizo yake ziada.

    Ni mfanyabiashara, ni kijana,ni mjanja,ni msomi,na zaidi anajua kusoma nyakati na ni mzuri wa kula nao,hakombi,anabakisha kidogo kwa ajili yao. Hima hima nyie wenzetu wa wilaya nyingine tusile na kukomba na kusahahu kwamba na kesho kuna kula tena.

    ReplyDelete
  2. ...unafikili...Oh, maskini mwalimu wangu Mrs Uledi!

    Hivi karibuni tumeona "nadiliki", "kuhudhulia" na pengineyo.

    Dokezo: Kwa mwenye kufikili akumbuke fikra siyo fikla. Kwa mwenye kudiliki akumbuke madaraka siyo madalaka na kwa mwenye kuhudhulia akumbuke hadhra siyo hadhla. Naweza sasa kuelewa kwa nini Kizungu kinatupa taabu...

    ReplyDelete
  3. Hata mimi namkubali ingawaje simjui kwa undani sana ila mara nyingi nikisoma matukio aliyokuwepo anatia moyo, mfano hichi kitendo cha kujichanganya kusugua kisigino na twanga pepeta, sio wabunge wengi wanaoweza kufanya hivyo, pia kuna baadhi ya habari za nyuma ila sikumbuki ni zipi alinitia moyo wa kuona anafaa na wala watu hawakukosea kumchagua kua mbunge, coz anajua kula na vipofu. sio wengine wanakula na vipofu na sio kuwagusa mikono wanaondoka na sahani kabisaaaa, kipofu akitaka kula anagusa meza.

    ReplyDelete
  4. Nothing but psychology

    ReplyDelete
  5. Mimi namkubali Kapteni John Komba kwa mwili wa ubwanyenye inabidi aongee na hassanali yule mwanamitindo ampe siri ya kuloose weight yake khaa maana anatia imani jamani komba!!!

    ReplyDelete
  6. ANAFAA NA ANA SIFA ZOTE ZA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. KWANZA ANA-HISTORIA YA KIPEKEE, PILI ANA-ELIMU YA KUTOSHA, NA-TATU ANAJALI.

    TANZANIA FOR DEWJI.

    ReplyDelete
  7. Shikamoo Anko

    Hivi mimi nina swali. Je inawezekana Mo akaja kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania wa asli ya kiasia? Yaani kuna uwezekano Mo akawa Obama wa Tanzania? Huyu Mbunge anatosha jamani na asibaguliwe kama ataomba kuwania kiti hicho kiteule.

    Bwana PK

    ReplyDelete
  8. JE FILIMBI IMESHAPULIZWA TUWEMO?

    ReplyDelete
  9. Nadhani tanzania tuna uwezekano wa kupata rais mwenye asili ya kihindi, ndani ya miaka 30 ijayo (awamu 3 zijazo), inawezekana huyu. Kumbuka siongelei kama utakuwa uamuzi mzuri, natoa tu utabiri wangu. Wadau mnasemaje?

    ReplyDelete
  10. DEWJI ANAJUA ILE METHALI ISEMAYO, "UKILA NA KIPOFU USIMSHIKE MKONO."

    ReplyDelete
  11. SAFI SANA MO DEWJI KUMBE UNAJUA KUTWANGA NA KUPEPETA HIVYO?.

    NYAMWELA NA LILIAN ANGALIENI ASIJE AKAHATARISHA NAFASI ZENU KAIKA UNENGUAJI.

    BRAVO DEWJI TUNAKUPENDA KWA JINSI UNAVYOJICHANGABYA NA WAPIGA KURA WAKO

    ReplyDelete
  12. our future "yes we can". I will vote for him in a heart beat, hey Bill Clinton won twice on womens vote, its all about the looks for me! One important question, are you single?...

    ReplyDelete
  13. Well, Nilikua simjui lakini baada ya kuingia kwenye blog yake...kitu kimoja kimenivutia...Lishe bora...Kiongozi yeyote anayeweza kuwahamasisha watu wale chakula bora na matunda....Huyo anapata kura yangu.....

    I like him...sio wabunge wengine hapo wa singida wameishia kuishi mijini wanaadress za Dar es Salaam sijui huko kwenye majimbo yao wanaendaga lini....

    Kweli huyu akigombea uraisi...mimi nashuka nije nimpe kura yangu...

    Kiongozi wa kuigwa.

    Big up MO

    ReplyDelete
  14. Al Musoma, Chukua TANO ndugu yangu.
    Ni Tatizo kubwa sana la 're' kuwa 'le'. Sijui ni ulimi unakuwa umelegea au vipi.

    Utaona mtu anaandika 'inanibuludisha loho'. Nidyo nini? Ulimi umelegea? Aaaghhhhhhhhhhhhh!

    ReplyDelete
  15. Mhhhhhhh huyu mbunge wa ukweli. Nimemkubali. Pics zake zinaonyesha anawajali wananchi
    Big up.
    Mdau DSM

    ReplyDelete
  16. Ubunge sawa ....Urais ??? Mungu epushia mbali....Tanganyika nchi yangu Tanganyika...ni ugonjwa gani huu unatunyemelea??? tuta sutwa na vizazi vijavyo....

    By LOBOKO LOBII PAPAA...

    ReplyDelete
  17. Ok, baada ya kuingia na kusoma kwenye tovuti yake, nimemkubali. Nilikuwa nimemuoverlook siku za nyuma, lakini story ya maisha yake iko inspiring sana. Kiasi naweza kusema tunafanana, kwa sababu na mimi nina nia kubwa ya kurudi nyumbani na kwenda mbali na Dar es Salaam kusaidia kulijenga taifa (huku ndugu na marafiki wakinikatisha tamaa). Singida ilikuwa moja ya mikoa iliyokuwa nyuma sana siku za nyuma, lakini huyu mheshimiwa yuko mbioni kuifanya moja ya mikoa iliyotatua matatizo ya msingi. Sina pesa kama yeye lakini nadhani nia na matumaini yangu ni makubwa kama yake. MO nitafuata nyayo zako. Mwenyezi Mungu akubariki.

    N.B Kuna kitu moyoni kinaniambia watu kama hawa watanzania wapo, ingawa siyo wengi. Wanahitaji tu mwamko. Tusikate tamaa jamani, yote yanawezekana.

    ReplyDelete
  18. MIMI SIMPENDI JOHN MASHAKA LAKINI KAMA AMEKAA MASHAKA NA HUYU DEWJI NI BORA MASHAKA HAWA WENZENU WANA URAIA KWA KILA NCHI HACHELEWI KUIUZA NCHI.

    ReplyDelete
  19. Nasema hivi ndugu zangu wazawa wa Bongo endeleeni kumfagilia mdosi hivyo hivyo kama ambavyo tumekua tanafanya miaka nenda rudi.Halafu tutafute wabongo wangapi walofagiliwa Udosini,ok..????

    ReplyDelete
  20. Kwa kawaida mimi nimpinzani namba one lakini nilipoona blog yake huyu jamaa kura yangu ataipata.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...