Geofrey Kibogoyo
Ndugu wanajumuiya ya Manchester mnakaribishwa katika party ya kumuaga mwanajuiya mwenzetu Geofrey Kibogoyo anayerudi nyumbani moja kwa moja kulijenga Taifa.
Sherehe itafanyika Novemba 7, 2009
saa moja jioni katika address hii
34 Falcon Court,
Old Trafford,
Manchester M15 5QD.
Chakula na kinywaji vitakuwepo kufika kwenu ndio kufanikisha shughuli ya kumuaga mwenzetu ambaye kwa muda aliokuwepo amejitolea kwa hali na mali kufanikisha shughuli za maendeleo ya jumuiya yetu,
karibuni sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. SEMA TU MDAU KASTAAFU KUBEBA BOX SASA ANARUDI BONGO KUPUMZIKA SIO KUJENGA TAIFA.

    KAMA KUJENGA TAIFA ANAWEZA TU KUJENGA AKIWA HUKO HUKO MANCHESTER. HUKU ATAKUJA TU KUONGEZA IDADI YA WATU KWENYE FOLENI ZA BONGO.

    ReplyDelete
  2. Alikuwa akifanya nini na kwanini anarudi?

    ReplyDelete
  3. mimi nimeona hiyo picha nikajua jamaa kafa, kumbe nikumuaga ya tutaonana mbele kwa mbele.I hope ana makaratasi ngoma ikidunda bongo arudie boxi lake uk.

    ReplyDelete
  4. watu hamkosi yakusema?mwenyewe kaamua kurudi nyumbani for good,kashamaliza kilichomleta uk..tutakuja kukuaga bila kukosa.

    ReplyDelete
  5. kaka hongera kwa uwamuzi wako wambie na wazee wenzio wasiongopa kurudi home kwani nyumbani ni nyumbani tu, wapo wengi Manchester.

    ReplyDelete
  6. uamuzi bora huo mbona AFRICA maisha poa tu pesa yako

    ReplyDelete
  7. Wabongo haooooo mtu akiamua kurudi nyumbani mwachukia, akikaa huku huku mwachukia jamani tufanyeje? Well, tutakuja tubanane tu hapo....na + sign ni kuwa wawekezaji wakubwa kutoka south wanatupenda kweli kweli hata degree hatuna lakini tukikanyaga tu airport na kazi mkononi tunayo....

    ReplyDelete
  8. duh hata mimi nilivyoona picha nikajuwa jamaa "AMESHARUDISHA SEAT NUMBER" JAMANI PICHA ZINGINE ZINATAFSIRIWA VINGINE...MME KAA ULAYA LAKINI MMESHINDWA KUSOMA KWA HILO..?!!!"KWA LUGHA YA WATU NI "BODY LANGUAGE". APART OF THAT , SI VIBAYA KURUDI NDUGU YANGU NIA YAKO NDIO ANAYOJUA MOLA WAKO..KWA HILO SIKUJAJI. MUNGU AKUFUNGULIE...AMIIIN

    ReplyDelete
  9. Welcome back ... Na mimi nilikuwa USA nimerudi bongo kitambo na sijuti

    ReplyDelete
  10. Waosha vinywa hamumuonei huruma mzee mzima, mnampiga madongo tu. Anyway, chaguo la picha halikuwa zuri, ukijumuisha na kichwa cha habari, wengi tulidhani 'mwingine huyo'!

    ReplyDelete
  11. we anony wa 12:12:00 PM umeongea pumba kweli. Eti "body language" katika picha yake inaonesha kuwa amekufa!? Kwani hiyo ni picha ya maiti au? Pumbaavvuuu

    ReplyDelete
  12. mzee karibu Bongo huku kuna future.mimi mwenyewe nimekaa udengani (denmark)miaka 9 nimeguza majeshi mwaka huu mwanzoni.kuja kutumikia taifa langu na naona sikuchukua uhamuzi mbaya.Ni better asikuwambie mtu.
    Engineer.Vodacom

    ReplyDelete
  13. VISA YA KUENDELEA KUISHI KUPIGA BOX IMEGOMA NDO MAANA ANARUDI, ASITUDANGANYE. MAANA SIKU HIZI UK BOADER AGENCY NI WAKALI WE ACHA TU!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...