Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Amani Abeid Karume, akimlaki Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad alipowasili Ikulu ya Visiwani leo katika ziara ya kihistoria kwani toka Mh. Karume Maalim hajawahi fika Ikulu kwa mazungumzo rasmi isipokuwa katika dhifa za kitaifa na sherehe zingine. Kulia ni Mh. Ismail Jussa, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa wa CUF. Kilichoongelewa bado kutoka nje
Picha na mdau wa Ramadhani Othman Ikulu Zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. mbona WAARABU?

    mh...

    ReplyDelete
  2. Maalim seif anadili gani tena au anakwenda kuchukuwa chake kabisa

    ReplyDelete
  3. Mwanzo mzuri.Lincohn mwanademokrasia wa kimarekani alisema nanukuu: " A house divided against itself cannot stand". Elewaneni kwa ajili ya Zanzibar na Tanzania.
    Mdau

    ReplyDelete
  4. Nani mwarabu hapo!!!! XCZCHWIIII!!!!!!!, pusi we>

    ReplyDelete
  5. Hawa wakiwa waarabu, je waliozaliwa na kukulia kwenye vivuli vya mitende watakua nani???

    Mwarabu atakula ugali na vibua?? Jamani acheni ubaguzi namkumbuka sana Nyerere.

    ReplyDelete
  6. ndioo waarabu sio machogoo

    ReplyDelete
  7. hii mijitu mingine bwana haijui tupo 2009 sasa wao bado wana mambo ya kusema mwarabu sijui nani mbona hayo mambo ya kiukabila yamesahauliwa duniani

    wewe ANONY wa kwanza unafaa kurudishwa kwenye miaka ya 47 bado una ukabila kwani kuwa kiongozi kwenye nchi yako kunaangalia rangi au kabila???????

    ikiwa ni watanzania sasa tatizo lipo wapi????????

    mtu kama wewe ukisimama kwenye vijana wa sasa uanze kuongea mambo ya ukabila vijana wanaweza kukuzalisha hata kama wewe ni mwanaume.

    ReplyDelete
  8. mijitu mingine bwanaa..eti mwarabu...mwarabu kakusea nini....ni mambo ya mlo mzuri ndugu yangu...sijui huyo miongoni mwa mafisadi...ndio walewale wasipenda maendeleo ya tz...elewa wewe "mazengo" kutulia kwa znz ndio mafanikio kwa nchi nzima....

    ReplyDelete
  9. OF COURSE WANA DAMU ZA KIARABU

    ReplyDelete
  10. NDIO NI WAARABU SO WHAT??????

    KAJINYONGE SASA KAMA UNAWEZA NDIO MAANA SHIDA HAZIKUISHI NJAA TUPU IMEKUNZUNGUKA ETI OOH MWARABU KWANI OBAMA MZUNGU?????????

    HII MIJITU YA KALE KUMBE BADO IPO KAJIBANIKE KAMA KUKU SASA WENZIO WAPO IKULU WANAKULA KUKU KWA UJANJA WAO

    NAWEWE KATAFUTE UGALI WAKO KWA UJANJA WAKO ANGALIA NJAA YAKO USIANGALIE MAKABILA YA WATU NGEDERE WE.

    ReplyDelete
  11. rais amani mjanja kweli anamkaribisha maalim seif atlast

    ReplyDelete
  12. ama kweli viongozi africa noma,
    muda wote seif alishindwa nini kumtambua rais amani?
    na rais amani nae aliogopa nini kumwita maalim ikulu?
    au kwa sababu sasa ivi jahazi limeshagonga mwamwmba?
    haya! natuone. nini kitafuata!
    lakini ninawaomba ndugu zangu wa unguja napemba waachane na siasa zisizo na mbele wala nyuma,ni ULAGHAI TU, ndugu zangu wazanzibari, tuendeshe maisha yetu, seifu na amani hawatusaidii lolote,ispokua ni juhudi zetu wenywe ndio tutafika.
    .I LOVE ZANZIBAR.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...