MAPACHA WANNE - CHOKORAA, CHAZ BABA, JOSE MARA NA KALALA JNR
WAMEJIPANGA KUFANYA MAAJABU YA KUTIKISA ULIMWENGU WA MUZIKI NCHINI TANZANIA KWA KUTAMBULISHA ALBAMU YAO TAR 30/11/09 KATIKA UKUMBI WA KINONDONI STEREO. WANAOMBA SAPPORT KWA MASHABIKI WA MUZIKI WA DANCE
NDANI NA NJE YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hi! ndugu zetu msiwe na wasiwasi
    wanamziki wenzenu wa ndani na nje ya tupo pamoja nanyi,tena tunawatakia mafanikio mema katika uzinduzi wa Kitu chenu kipya,daima mbele kwa mbele.
    wenu
    The Ngoma Africa Band aka FFU!

    ReplyDelete
  2. Big up Michuzi kubandika hizi habari. Huu ndio muziki wetu wa asili na sio flava (play back), kati ya hawa jamaa wanne, hakuna hata mmoja wao aliye feki ila kidogo bwana mdogo Joseph Michael (Mara) naikubali sauti yake. Huyu jamaa ndiye mbongo pekee F.M. Academia lakini anamzima kila mtu sauti pale....Jose na wenzako kazeni buti, nyinyi ndio zawadi yetu.

    ReplyDelete
  3. Kweli Michuzi Jose yuko juu sana huyu yanki, jamaa anajuwa kuichezea sauti yake. Alinua na mapande yake katika ile album ya "Dunia Kigeugeu." Jose, Big up!

    ReplyDelete
  4. taifa hili la kesho kweli ni hatari, hapa Ali Choki na kina Muumin wasipoangalia watasambaratika hivi hivi. Banza anarudi punde tu toka hivi sasa, msikilizieni mapande yake...kazeni buti vijana muue flava muziki usio na akili na vipaji.

    ReplyDelete
  5. Mmmmmh! Hayo majina.

    ReplyDelete
  6. mapacha wanne au mapacha wawili ?!

    ReplyDelete
  7. Natamani ningeipata hiyo album, nina imani itatisha mbaya! maana hao vijana ni tishio!nawapa BIG UP

    ReplyDelete
  8. safi sana brothers.

    mi nawaaminia sana nyie maana nyote ni moto wa kuotea mbali, mnatisha yaani kwakweli itakuwa bonge la colabo,

    big up sana Mwenyezi atawajaalia kwa kile mlichopanga.

    ReplyDelete
  9. unamanisha ao ni mapacha kwa kuzaliwa?

    ReplyDelete
  10. Mimi ni fun wa Jose Mara yaani nampenda sana huyu kaka kwanza mstaarabu anaheshima na ndoa yake yaani hongera sana mke wa Jose Mara kwa kuwa na mume unaempa tafu kiasi hicho..

    ReplyDelete
  11. Aaah, vijana nawakubali sana, sana! yaani nikifikiria balaa mlilofanya katike ile truck 'kuachwa', hapana vijana mnatisha.
    Kaka Chaz baba, kama kuna shabiki wako namba moja, basi ni mimi. Kwa jinsi ulivyochana ktk ile truck sumu ya mapenzi na msinijadili, aah we ni noma kaka

    Kalala jr, vp kaka mbona cijacikia truck uliyotunga hapo Twanga?? ila mi nakukubali unavyocheza na verse unazoimba.

    kwa kifupi hii albam ya hawa jamaa, naisubiria kwa hamu sana coz nimeshaanza kuhisi utamu wake.

    Kinyero

    ReplyDelete
  12. wadau, hivi kinyero maana yake nini? au mi naelewa tofauti?

    ReplyDelete
  13. Jose Mara yuko juu kaza buti tu.
    Wengine punguzeni ubishoo.



    Rafikiye Abuu wa Namanga.

    ReplyDelete
  14. mi nampa BIG UP Jose, upo juu kaka kama gari la HAMMER ila wengine punguzeni kukuadia hao mapredeshee wa mjini wanawake unatubore tu

    ReplyDelete
  15. we anony wa hapo juu, kinyero maana yake ni kitako, teh teh, teh!

    ReplyDelete
  16. Nimefurahi sana kuona vijana mmeamua kupiga kazi.Cha msingi ni kuwa serious na sio kubweta,kazeni buti mtafika mbali..acheni ubishoo usiokuwa na maana.
    Choki na Muumini kaeni macho maana sasa hivi tutawasahau,kazi kutuchanganya akili,leo hapa kesho kule na kujiona bila nyinyi hakuna mziki!
    Big up Mapacha kama mnavyojiita!

    ReplyDelete
  17. i believe hawa wakaka watatoa kitu cha nguvu. haya tunasubiri kazi yenu. jamani mie namzimikia sana Jose mara, nipatieni namba yake nimtafute hahahah

    ReplyDelete
  18. Jose Mara kwa sauti hakuna cha ali choki sijui muumin wala nini, huyu jamaa yuko fiti kichizi. Anawaziba sauti wale wazaire wa F.M. Academia kinoma, Jose angekuwa demu ningekula naye sahani moja tu, sauti yake inachengua sana.

    ReplyDelete
  19. Michuzi hapa umefanya jambo la maana kupost hii ishu. Hawa mapacha ndio watakaobeba bendera ya muziki wetu si watu wa flava. Kina Kalala Jnr leteni vitu jamani wadau wa nje/majuu tunawasubiri kwa hamu saana

    ReplyDelete
  20. Vijana leteni ngoma za ki ukweli, hatutaki ujinga wa flava muziki usio na kichwa wala miguu

    ReplyDelete
  21. Nani kasema flava ni muziki jamani? Ule ni ujinga tu, na ndio maana unaona wasanii wake hawadumu kwani hawana vipaji. Kitu kimepikwa na kompyuta kisha mtu anatia tu sauti halafu anajiita mwanamuziki ni kweli jamani? To death with flava, hiyo waachieni hao wajinga wa kimarekani!

    ReplyDelete
  22. Jamani flava si muziki yaishe hapa. Kina Jose tuleteeni vidonge hata kwa dolla 30 nitanunua hiyo cd yenu ila nawaomba tu, msilete tungo za kijinga kama za flava! Tunataka tungo zilizoenda shule.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...