Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Chrisant Mzindakaya akianglia moja ya malighafi ya kuzalisha chuma katika Eneo la Liganga mkoani Iringa.. Kulia ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanziba ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo Dk Gharib Bilal na katikati ni Katibu Tarafa wa Ludewa.Bodi hiyo ilitembelea miradi mbalimbali ya Makaa ya mawe na Uzalishaji chuma.
Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Masoko Joyce Mapunjo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Gideon Nasari (wapili kushoto) na mjumbe wa Bodio ya NDD Prof. Idris Kikula (wapili kushoto) wakiangalia moja ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika macho ya Ngaka Wilayani Mbinga unaofanywa nakampuni ya Tancoal Enegy. Wajumbe wa Bodi ya NDC walitembelea mradi huo na ule wa kuchimba chuma Liganga mkoani Iringa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tanzania Tanzania, nchi Tajiri kwa maliasili, lakini masikini haisemeki. sasa faida yake nini kuwa na maliasili zote hizi? au ndio kwenye miti hakuna wajenzi? any way Mungu ibariki Tanzania, may be maliasili zikiisha itaendelea kimiujiza!

    ReplyDelete
  2. tatizo ni kutotumia lasilimali katika kutatua matatizo ya ndani. tunafikiria tu kuwauzia wenzetu weupe.
    so far hakuna mkakati unaoonyesha jinsi gani wabongo wanatatua matatizo yao kwa hizi maliasili za ndani. tunaweza kupunguza umasikini kwa kuwawezesha watanzania wenyewe kuwa good consumers wa bidhaa za ndani.

    ReplyDelete
  3. viongozi msiwe mnaonyesha wakati wa kukagua miradi tu, muwe mnaonyesha na matumizi ya hiyo miradi imeendaje jamani, mweee, lakini inajulikana pesa mnatia mfukoni,acheni hivyo, halafu mnasema ulaya kuna ubaguzi, afadhali wazungu wana utu, wanajali watu wao,na watoto, sisi wenyewe kwa wenyewe hatujaliani, duuuuuuuuuuu aibu.Tuna miradi mbali mbali bado tunaomba misaada ulaya.heheheheh huruma.

    ReplyDelete
  4. Haya basi hicho kijiji yanapotoka hayo makaa ya mawe kiwe na maji au maendeleo basi hakuna kitu. yaani utakuta kijiji kina almasi angalia wananchi hawana hata visima au mabomba, ivi kweli ulaya kuwe na almasi waafrika wakachukuwe hizo almasi kwa bei ndogo, halafu waje kujenga Afrika ingewezekana? kitakacho tokea ni maandamano kila kona ya Ulaya, kwa kifupi haiwezekani, amkeni viongozi wa kibango.

    ReplyDelete
  5. Raisi Mtarajiwa wa Zenji, babu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...