Habari kaka Michuzi,
Mimi ni mwanaume Mtanzania, ninaishi katika mkoa wa Arusha.
Nina sifa zifuatazo:
Umri: miaka 28. Elimu: msingi/ufundi. Kazi: fundi. Urefu: futi 6 Rangi: mweusi. Kipato: kima cha chini. Natafuta rafiki au mchumba wa kike mcha Mungu na anayejiheshimu mwenye sifa zifuatazo:
Umri: kuanzia miaka 20 - 28. Elimu: kuanzia ya msingi ila isiwe elimu ya juu sana. Dini: mkristu kama siyo awe tayari kubadili. Sibagui rangi, kipato, kimo wala umbile. Asiwe na watoto wala ambaye amewahi kuolewa. Ambao wapo serious tuwasiliane kwa email address
Umri: miaka 28. Elimu: msingi/ufundi. Kazi: fundi. Urefu: futi 6 Rangi: mweusi. Kipato: kima cha chini. Natafuta rafiki au mchumba wa kike mcha Mungu na anayejiheshimu mwenye sifa zifuatazo:
Umri: kuanzia miaka 20 - 28. Elimu: kuanzia ya msingi ila isiwe elimu ya juu sana. Dini: mkristu kama siyo awe tayari kubadili. Sibagui rangi, kipato, kimo wala umbile. Asiwe na watoto wala ambaye amewahi kuolewa. Ambao wapo serious tuwasiliane kwa email address
jaduong1981@yahoo.com
Jaduong.
Arusha.
Jaduong.
Arusha.


Wazo zuri ila tu si lazima awe na elimu ndogo, akiwa na elimu kubwa na anakupenda wala usimkatae. Ni hayo tu. Nakutakia heri na ufanikiwe.
ReplyDeleteBabu kutokana na hali yako, tafuta mwenye elimu ya kutosha(Msc.Economics/Law/HR/Marketing) na ikiwezekana mtoto wa geti kali ili mambo yakunyookee huko mbele ya safari. Kazi yako kubwa ni kumtosheleza na kutia karufundi kwenye malavidavi. Hao walalahoi wenzako watakuzeesha mapema na kukurudisha nyuma kimaendeleo.
ReplyDeleteHata mimi natafuta mwanaume wa kunioa ila kwa kweli napenda mwanaume mwenye kipato cha juu. Unajua baadhi ya wanawake tunapenda kuolewa na wanaume wenye mali nyingi na kipato kikubwa. Ok by the way, utapata tu mchumba asiyekuwa na tamaa na atakaekupenda kwa dhati endelea tu kumwomba Mungu.
ReplyDeleteAngelie.
We Jisajilly hujui kwamba mwenzako akikuzidi elimu kwa kiasi kikubwa sana utanyanyasika? Lazima wanandoa muwe na hali angalau zinazofanana kidogo. Ndio maana watu maarufu wanaoana wenyewe kwa wenyewe. Sasa huyu bwana ni std seven akioa professor kweli wataendana? Kumbuka J.Lopez aliolewa na mcheza show wake na watu wengi walitabiri ndoa haitadumu kwa sababu hawaendani na kweli ikawa hivyo.
ReplyDeleteTangazo hili ungeliweka pale Rorya au Tarime mbona ungewapata wengi tu ndugu yangu. Nakutakia kila heri.
ReplyDeleteMichuzi tuma hiyo ombi marekani kwa wabeba box, hapa bongo hatuhitaji wachumba hasa wenye vipato vya chini sisi huku matawi ya juu peleka ulaya na marekani wabeba box wavunjane mbavu.
ReplyDeleteHuyu anony wa 12:16:00 PM anataka kuleta ndoa za ukabila. Badilika acha kuleta mambo ya mwaka 47. Wengi hawajamwelewa mtafuta mchumba anataka kuoa na sio kuolewa ndio maana hapendi wanawake wenye elimu kubwa sana. Eti umri mzuri zaidi kwa mwanaume kuoa ni kuanzia miaka mingapi? Mbona mi naona huyu mshikaji kama anataka kuwahi sana?
ReplyDeleteduh... hanifai wakina sisi wengine high maintainance au vipi Angelie?
ReplyDeleteapigane huyo aongeze elimu hiyo elimu bado ndogo sana na umri unamruhusu,akioa sasa hivi atamtesa huyo mwanamke na hicho kima cha chini.
ReplyDeleteKweli anony wa Mon Nov 23, 07:33:00 PM, wanawake wengine bwana sisi ni wa gharama sana kwa siku mbili tu tunamaliza kipato chake cha mwezi. Ila hatufanani kwa hiyo mi nampa moyo aendelee kutafuta. hahahaaa!
ReplyDeleteAngelie
kwa kipato hicho usiwe picky..akija cougar mwenye elimu na mtoto mmoja au wawili jichukulie...bora mapenzi ..material things havina maana ..unaonekana down to earth but a little picky....
ReplyDelete