Kamati ya Nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) hilo imetengua adhabu za kufungiwa maisha kwa mwamuzi Osman Kazi, ambaye anaonekana wa pili toka kulia pichani.

Kamati ya Nidhamu iliyokuwa chini ya Kamanda wa zamani wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ilifikia uamuzi huo na kutangaza jana mbele ya wanahabari, ikiwa ni mara nyingine tena ikitengua ama kupunguza adhabu zinazotolewa na Kamati ya Mashindano.

Kazi pamoja na waamuzi wenzake wasaidizi watatu ambao ni Omari Miyala, Omari Mfaume na Kamwanga Tambwe walifungiwa kuchezesha soka maisha na TFF wakihusishwa na rushwa kutokana na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na Majimaji.

Hata hivyo katika uamuzi huo wa Tibaigana ni Kazi pekee aliyepunguziwa hadi miezi mitatu, wakati wenzake watatumikia adhabu ya miaka mitatu.
Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kazi ipo hili lijamaa simba damu. ukisikia anachezesha simba na yanga andaa kilio mapemaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...