HAYATI ABUSHIRI KILUNGO

MZEE ABUSHIRI KILUNGO (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NYUMBANI KWAKE TANDIKA,MTAA WA KIVUNGO BAADA YA KUUGUA UGONJWA WA KISUKARI KWA MUDA MREFU.

MAREHEMU KILUNGO AMBAYE ALIWAHI KUWA NAIBU MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM MIAKA YA NYUMA NA PIA ALIWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA DAR (DRFA).

MAREHEMU KILUNGO AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO WATATU WAKIWA NI WA KIUME NA WAWILI WA KIKE.MAZISHI YATAFANYIKA LEO (17/11/2009) SHAMBANI KWAKE TUANGOMA,NJE KIDOGO YA JIJI LA DAR.

TUNAMUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MZEE WETU ABUSHIRI KILUNGO MAHALI PEMA PEPONI

-AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. R.I.P

    Mwenyezi Mungu amlaze mahari pema
    merehemu Bushiri Kilungo,marehemu Chitete,kaka Kapera,Bona Max,Shaaban "Pacho" Ramadhani wa Navy Zanzibar na balozi Cisco Mtiro tumekuwa na kucheza mpira pamoja tokea tuna umri wa miaka mitano mwembe yanga Tandika,kifo chake kwa ugonjwa uliyomsumbua miaka mingi ni masikitiko makubwa saana katika maisha yangu.

    Mickey Jones-Denmark

    ReplyDelete
  2. R.I.P You will always be remembered for your kind heart. you were always ready to help when it was within you ability.

    Innalillah Wainna Lillahi Rajiooon.

    ReplyDelete
  3. nyerere wa tandika!!INNA LILAHI WAINA LILLAH RAJIUN..
    ULIKUA MTU MUHIMU SANA KWETU MAJIRANI ZAKO ..
    MATURUBAI ULIWEZA KUTUPA BURE WAKATI WA MISIBA.

    ReplyDelete
  4. Hey poleni familia ya abushiri kilungo,tulikwa naye Alaf na msemo wake"eee bwanaeee"
    rip Kllungo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...