Home
Unlabelled
nondozzzzz chuo kikuu huria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hongera Mama kazi nzuri.
ReplyDeleteNashauri Wizara / Kamishina ya Elimu ya Juu wakae chini wawe wabunifu waandike 'a white paper' na kuisogeza mamlaka za juu ili yumkini kuwepo mjadala wa kutunga(kuboresha)sheria juu ya:-
a. Utambuzi na udhibiti wa viwango na vyeti, stashahada shahada za elimu mbalimbali (si mnaona mabishano ya sasa ya dondo feki toka majuu).
b. Taratibu za mahafali (zikiwemo mambo ya majoho, rangi n.k maana kwa kweli sasa ni vurugu tupu.
Mfano hapa kwa nini nondo tu ya Bcom mtu avishwe kofia? Itakuaje aki Panda hadi Darini (PhD) yaani haipendezi kabisa kama isivyopendeza chekechea kuruka na majoho na kofia za tarabushi wanapojiandaa kuanza elimu ya msingi.
Anayesema mambo ya mavazi, vitambaa na rangi hayana tija wala haja ya kudhibitiwa basi sote turuhusiwe kuvaa pia magwanda ya Unajeshi na Upolisi maana tukitaka yatapatikana madukani.
Na kila mtu yeyote aweze kupeperusha Bendera ya Taifa lolote au ya Bunge kwenye gari au bajaji yake hata usiku wa manane popote si vitambaa hivyo vinaweza kupatikana tu.
Na kila Wanachama wa Chama cha Siasa waweze kuandamana wakiwa na bendera za wapinzani wao na kuzichoma barabarani kama wanavyotaka tu.
Na Wambunge waruhusiwe kuingia mjengoni kama madansa kwa mwendo wa vi-pico pico micro mini skirts na vi-skin tight na mitepesho kama wakati wa Fiesta si mavazi hayana stahili wala so?
Na ajisikiaye kuingia Msikitini na viatu iwe ruksa kama ambavyo mcheza wa timu ya mpira wa Miguu atakavyoamua kuingia na jeans na kofia la kuvunia mpunga uwanjani au ambavyo karani wa mahakama ataruhusiwa kutinga na joho la Majaji maana yanauzwa na kukodishwa tu?
Hapo ndipo nitamshauri baba yangu Bwana jela ampe tenda Remtu.... awashonee Wafungwa mashati meusi na kuwatengenezea kola nyeupe za kichungaji si itakuwa fashion tu ya kuwaongezea ujoto shingoni?
Kisha mwanamitindo huyo awaletee tracksuits laini Madaktari wote maana ndio litakuwa vazi lao mahospitalini.
Kama vile haitoshi uwanja wa fisi nako pawe panafunguliwa kwa kusimika siwa (rungu la Bunge) mahala palipoandaliwa na kuanza kwa maombi kabla biashara zile hazijaanza si hizo ni 'symbols' ambazo hazina maana?
Na bila kusahau kuwa ma-boy-girl Scauts wahitimu wa mafunzo nao sasa waruhusiwe kula viapo vyenye matamshi sawia kabisa na Wabunge si nao wanatakiwa kuwa waaminifu na kuilinda katiba ya nchi au nimekosea?
Mwisho kama mahafali na sherehe zinaweza kusherehekewa vyovyote alimradi una uwezo, basi mimi naanza kukusanya fedha maana wakati wa mazishi yangu familia italipa tu fedha jeshini na nitapigiwa mizinga 21 kama heshima maana hakuna athari yeyote alimradi wananchi wamejulishwa mapema na uwezo wa kulipia gharama za mabomu, mizinga na Walipuaji upo.
Degree zilikuwa zinatisha miaka ya 1960s hadi 1970s Siku hizi ni kama njugu sokoni universities kila kona hadi chooni!!!!
ReplyDeleteHuyo aliyetoa maoni kwamba digrii zimekuwa njugu aache ulimbukeni na tabia chafu ya kupenda kuponda. Alitarajia hao wachache ndio wawe na digrii????????? Acheni ubinafsi, hata vyuo vikijengwa kila kijiji, hayo ndiyo maendeleo ambayo nchi inatakiwa ipate. Huu ulimbukeni na roho mbaya ya watu wachache kutaka kumiliki vitu, ndio yameifikisha nchi katika hali ya ufisadi. Hata akiponda, lakini Mama Kilango ndo hivyo keshaipata digrii. MWENYE WIVU AJINYONGE!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHayo mambo ya bongo bwana nchi za wenzetu vyuo kila kona kila mtu ana digree mpaka fundi cherehani wasomi kibao mpaka kazi hakuna.
ReplyDeleteSafi sana mdau namba 3. Mwenye wivu ajinyonge kama kidogo?
ReplyDeleteKila mtu apongezwe kwa hata kidogo alichopata au alichofanya. Bado tu linakukera suala lakuvaa joho watoto wa chekechea? Mbona tulishazungumza humu kijijini siku nyingi? Ungekata rufaa siku zile zile saizi umechelewa.
Kwa mtazamo wangu naona mtu kuvuka hatua moja kwenda nyingine ni maendeleo sina budi kumpongeza.
Wewe mdau namba moja mbona umejijibu wewe mwenyewe? Usifananishe magwanda ya polisi na au yakijeshi na sherehe. Hivi unapungukiwa nini?
Kila mtu akazane kivyake.
Blog ya jamii idumu.
Huyu mdau wa Tue Nov 03, 05:11:00 AM pumbaf kabisa we ungekua kijijini ungekua mchawi nakuambia huna tofauti na wale wanaologa wenzao eti kisa wanajenga nyumba na kuezeka na bati. Nikiangalia huo muda wa comment yako yaonesha ama unacomputer yako nyumbani umekurupuka alfajiri na kuccmment au upo ugenini kwenye mipaka ya watu so behave m2 na uache ushirikina wa maendeleo
ReplyDeleteMPENDE MSIPENDE DEGREE ZA SASA NI OVYOOO HATA WAHITIMU NI WEUPE UKILINGANISHA NA ZA MWAKA 47, THAI IS A FACT, HUWEZI KUMLINGANISHA MSOMI WA ZAMANI NA WA SASA KAMA WAPO VICHWA WA SASA NI WACHACHE SANA, I SAY SO BECAUSE I KNOW I AM A HUMAN RESOURCE MANAGER SOMEWHERE, MSOMI WA SASA HATA KWA LUGHA YETU YA TAIFA HAWEZI KUJIELEZA AU KUFANYA KITU DIRECT. SAY YOU WANNA SAY THAT IS IT. I DONT CARE CALL ME ALL NAMES YOU KNOW, I HAVE RIGHT TO AIR MY OPINIONS.
ReplyDelete