Jumamosi Tarehe 28/11/2009 BigRight Promotions imeandaa pambano la ngumi za kulipwa katika ukumbi wa UMOJA CLUB ulipo mwananyamala Mapinduzi,

Kwa lengo la kuhamasisha wanamichezo kupenda kujitolea kupimwa afya zao,kwani kuna baadhi huwa wanafeli wanapowakilisha nchi katika michezo ya kimataifa,kwa kutokujua afya zao vizuri, kama zoezi hili litakuwa linakwenda vizuri, BigRight Promotions inategemea kuingia mkataba na UMOJA CLUB kwa usimamizi wa AMREF wa kuandaa mapambano na burudani kila mwezi kwa ajili ya uhamasishaji upimaji na uendelezaji vipaji na michezo nchini.kuanzia januar 2010.
Katika mpambano huo inatarajiwa kuwapiganisha mabondia wakongwe ambao bado wapo fiti kimichezo na mabondia chipukizi ambao ni wakali na wapo katika hari ya ushindani,

Mabondia wanaotegemewa kucheza ni kama ifuatavyo;

(Win-draw-loss)

cruiserweight RAMADHANI KIDO(5-0-1) Vs KAMINJA RAMADHANI(9-1-4). 8round

light middle weight Lucas Benard(3-1-0) Vs Mbwana ally (van dame)(3-2-5). 6round

light middle weight Ibrahim `BigRight`kamwe(9-1-1) Vs Paul msela(12-2-7).4round

Light welter weight Jafary Majia(mr Nice)(4-0-2) Vs Ibrahim Amedeus(Star boy)(6-1-3). 4round

Light weight Musa sunga (Sunga boy)(1-0-0) vs Josefat john.(3-0-0) 4round

Fly weight Becka Mackenzie(mdachi)(3-1-1) Vs Shaban Madilu.(7-3-8) 4round

Bantam weight Rajab Shaban(kibosho)(0-1-0) vs Athman Hassan.(2-0-0) 4round

light fly weight Sadat Miyeyusho(6-3-4) Vs Ali Hassan(5-2-2) 4round

Said chaku(chaku master)(14-5-12) v/s Daudi Mhunzi(11-4-9) 6round


Mapambano haya ni ya uhamasishaji upimaji UKIMWI na afya za mabondia kiujumla.pia washindi watapata nafasi ya kucheza katika mapambano yafuatayo aidha ubingwa au kadi ya kugombania ubingwa,Pia kutakuwa na burudani za wacheza rusha roho,maigizo,na muziki wa kizazi kipya ukiongozwa na sista P na waimbaji tofautitofauti

Zoezi zima la upimaji linatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa tarehe 27/11/2009 saa nne asubuhi hapohapo Umoja club

MAHALI ULIPO UKUMBI WA UMOJA CLUB.

AMREF (BASKETBALL COURT),

MWANANYAMALA MAPINDUZI – KINONDONI D.S.M

SIO MBALI NA UWANJA WA MPIRA WA MWANANYAMALA`B` - LAKE RANGERS

UKIPANDA BASI UNASHUKA MWANANYAMALA MAGENGENI (SOKONI) AU MWANANYAMALA HOSPITAL



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...