Aliyekuwa mwanamuziki wa bendi kadhaa za muziki nchini ikiwemo TOT,Double M Sound na nyinginezo Rashid Mwenzingo wikiendi hii aliwasilimia kisanii wanamuziki wa bendi ya K-mondo sound waliokuwa wakitumbuiza katika ukumbi wa Triz Motel uliopo Mbezi jijini Dar.
Mwenzingo aliingia ukumbini hapo kwa lengo la kuangalia shoo hiyo kama
washabiki wengine wa K-mondo lakini alijikuta anapanda jukwaani baada ya
kukunwa na moja ya vibao vilivyopigwa na bendi hiyo ambavyo vingine
aliwahi kuviimba katika bendi alizowahi kufanyia kazi.
Mwenzingo ambae kwa sasa anaimba katika bendi ya Msondo alipanda jukwaani hapo na kuimba sambamba wana Kmondo kama ishara ya salam kwa wasanii wenzake wa bendi hiyo. “Kama ilivyo kawaida yetu wasanii huwa tunasalimiana kisanii”alisema.
Bendi ya K-mondo ambayo hufanya maonyesho katika ukumbi huo wa Triz uliopo Mbezi kila siku ya Ijumaa inaongozwa na Richard Mangustino sambamba na wanamuziki wengine akiwemo Vumi, Mhina Panduka a.k.a Toto Tundu na wengineo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...