Miss East Africa Rwanda, Cynthia Akazuba akitabasamu baada ya kuvikwa taji
Fimbo tatu za Rwanda: Miss East Africa Rwanda, Cynthia Akazuba (aliyeketi) akiwa na mshindi wa pili, Annete Mahoro na mshindi wa tatu, Sabrina Kangezi mara baada ya kutawazwa

Ampendeza: Miss East Africa Rwanda, Cynthia Akazuba akitabasamu baada ya kuvikwa taji MISS Kigali, Cynthia Akazuba usiku wa kuamkia leo aliibuka mshindi katika shindano la kumsaka Miss East Africa Rwanda baada ya kuwashinda warembo wengine 11.

Katika shindano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Serena mjini hapa, Cynthia alizawadiwa faranga milioni moja karibu sh milioni tatu za kitanzania.

Kwa ushindi huo sasa Cynthia ataiwakilisha Rwanda katika fainali za Miss East Africa zitakazofanyika Desemba 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Mrembo Annete Mahoro alishika nafasi ya pili akiondoka na faranga 500,000 sawa na karibu milioni moja na nusu ya Tanzania. Annete pia ataiwakilisha Rwanda kwenye fainali za Miss East Africa.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Sabrina Kaganza wakati Viviane Umulisa na Ritha Uwera walishika nafasi ya nne nay a tano. Majaji wa shindano hilo Rena Callist, Petter Mwendapole (Tanzania), Lauren Makuza na Evelyne Umurerwa (Rwanda) na Inamahoro Chantal (Burundi) walimchagua mrembo Uwera Magreth kuwa Miss Photogenic na vazi zuri la ubunifu ambapo alipata ofa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania pamoja na kuishi kambini na warembo wengine wa Miss East Africa.

Shindano hilo lilipambwa na wasanii mbalimbali wa Rwanda lakini muigizaji Ntarindwa Diogene alionekana kukongoka nyoyo za mashabiki waliohudhuria onyesho hilo. Pia mwanamuziki Meddy alichangamsha onyesho hilo.

Warembo wote 12 walipita jukwaani na mavazi ya ubunifu, jioni vazi la asili kabla ya kuchujwa na kubaki watano ambao waliulizwa maswali mbalimbali kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na maisha yao binafsi.

Kambi ya Miss East Africa itakuwa Kunduchi Beach Hoteli na itaanza Desemba 1 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wako bomba ile mbaya

    ReplyDelete
  2. Sas ngoja Wahutu wakanawe mapanga yao, kwa mchezo huu MUHUTU kamwe hatowini.

    ReplyDelete
  3. NILIPOZIONA PICHA ZA WANYARWANDA HAO WIKI ILIYOPITA NILISEMA WATANZANIA HATUNA CHETU, MMEYAONA HAYO SASA,

    ReplyDelete
  4. We anonymous was Uhutu, Ututsi, acha hizo! Yaani wanowe mapanga? kwahiyo kila anayekuzidi uzuri, utajiri na fursa ni kumwua au inabidi ufanye juhudi ushindane nae, wivu wa Kimaendeleo? Kwa taarifa yako, mwaka 1994 wahutu walikimbia baada ya kuwaua majirani zao watutsi lakini matatizo yao hayajaisha kwasababu waliwaua majirani zao!
    Let's promote beauty, ujirani mwema na utu, sio ukabila.
    Na hata hivyo Miss France 2000 Sonia Holland na Miss Switzerland Lilianne Murenzi wana asili ya AFRICA, with beauty, they dont look at tribe!

    ReplyDelete
  5. hawa mbona sio wakali, watanzania tunawasichana bomba zaidi na mwaka huu hilo taji tutalichukuwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...