Kocha Marcio Maximo na Taifa Stars

Habari toka Cairo zinasema usiku wa kuamkia leo Ijumaa Taifa Stars iliyokuwa ikimenyana na Misri katika mechi ya kirafiki na kujikuta imekula bao 5-1.

Kwa zaidi cheki link hio chini na magoli ya waarabu,
ingawa goli letu hawakulionyesha.

http://www.youtube.com/watch?v=VVT-Sjsv7BM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. huyo kocha haondoke kwao kwani kashindwa kazi pia anachukua makipa wa bovu yeye ajifunzi kwa kina capello mwenzie anachukua wachezaji wabovu tu maximo hafai kwanza anashinda break point posta na mpira atafundisha saa ngapi .by Mdau.

    ReplyDelete
  2. nadhani timu ilikuwa haijaanaliwa. wakati wale kila siku wanakua mazoezi ya kule jangani. so tukubali tu matokeo. ila inashusha hadhi eeeeeeeeeeeeeh

    ReplyDelete
  3. Kwani wakionyesha hilo bao letu ndiyo tutakuwa hatujafungwa 5-1?

    ReplyDelete
  4. Hiyo clip inaonyesha jinsi gani kiwango chetu cha mpira kiko chini. Yaani wa misri wakifika golini kwetu tu ni bao duuuuh!! Kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  5. Acha kocha aendelee tu kuzikusanya akishiba ataondoka.....!

    ReplyDelete
  6. TANZANIA NAKO KUNA MPIRA? MWISHO SIMBA NA YANGA TU BASI. BAADA YA HAPO HAKUNA CHOCHOTE. VERY EASY GOALS.

    ReplyDelete
  7. Matokeo tumeyakubali. Hivi kule TFF hakuna kamati ya wataalam wa soka toka vilabu vya ligi kuu au vinginevyo wakatoa ushauri kwa timu ya taifa? Kweli football yetu ndogo lakini aina ya magoli tuliyofungwa inaonyesha timu ilichanganyikiwa, haikujipanga,walinzi hamna kitu. Anyway nashauri tujipange na tumshauri kocha yanayofaa, chuki na ubaguzi kwa wachezaji havisaidii taifa hili.

    ReplyDelete
  8. Tumechoka Na Habari Za Taifa Star Tuwekee Za Simba Au Liverpool Maana Tulimkataa Huyu Kocha Wakubwa Wakatulazimisha...TFF Basi Mngepigisha Kura Ya Maoni Kuhusu Huyu Kocha Hamkutaka Kisa Mnafanya Nae Biashara Brazil-Bongo Mnazani Hatujui

    ReplyDelete
  9. kwa kusema kweli afya za wachezaji wetu ni mgogoro! hawana misuli kabisa, ukilinganisha na hao Wamisri, ndio mana wakawa wanaingia na mipira kirahisi sana mpaka ndani ya 18. kama wachezaji hawana misuli ya kutosha ni ngumu sana kupata mafanikio katika mechi za kimataifa.waongeze lishe na mazoezi.

    ReplyDelete
  10. Hii ni kichekesho kweli!!!!
    Tazama goli la nne, yaani huyo mlinzi namba 5 mgongoni alivyo kwepa mpira wakati jamaa anajiandaa kufunga. Jamani huyu naye anachezea timu ya taifa? Sasa anafanya nini humo uwanjani?

    Kwa mchezo huu hata tukicheza na timu ya vijana under 21 ya Ghana au under 17 ya Nigeria au Bukinafaso bado tutapigwa bao nyingi sana.

    Yaani hata ukimbiaji wa wachezaji wetu bado ni sifuri,kujipanga hawawezi na sidhani kama wanafuata mafundisho ya kocha wao.
    I mean it is terrible, this is not soccer. Wanasoka wetu tafadhali, tazameni hata hii michuano ya under 17 huko Nigeria muone ni vipi soka inachezwa jamani.

    Brother Michu, naona niishie hapa maana sitaki kuonekana si mzalendo. Lakini ukweli ni kuwa wachezaji wetu hawajitumi kwa chochote, si mazoezi wala uwanjani kwenye mechi.

    Tumieni muda mnaoshinda bar kujifua na kutazama wenzenu wanachezaje jamani!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Kipa hana kosa lolote, hao mabeki ni balaa, wanakwepa mipira kudadeki walahi, sasa sijui wameenda kufanya nini uwanjani?

    Uzuri wa video tunaona kila kitu si mambo ya Charls Hilari, Lalalaaaaah mpira umepita sentimita chache kutoka golini kumbe ni wa kurusha.

    Maximo aanze na timu ya vijana chini ya miaka 12, hawa hawafundishiki hata kidogo, tunapoteza muda na fedha tu hapa.

    ReplyDelete
  12. Tazama tena goli la pili, wakati jamaa anajiandaa kupiga beki namba 2 mgongoni anakwepa mpira, tena anatazama pembeni badala ya kuangalia mpira unakoelekea. Goli la tatu ni yale yale beki kakwepa mpira, kipa afanye nini? Kwanza ndo umemziba hata kuona hawezi. Jamani Tuatafuteni timu upya hawa hawawezi, tuamue kuanza na vijana chini ya miaka 12, baada ya miaka mitatu tutakuwa na timu bora ya vijana na Taifa.

    ReplyDelete
  13. YAANI NAHISI HATA HILO GOLI HAKUNA ,WACHEZAJI GANI WANACHEZA KAMA VILEMA??YAANI UKIANGALIA INAUDHI KABISAA WANAONEKANA HATA UWEZO WA KUSIMAMA TU NA MTU WA TIMU PINZANIA HAWANA,HUU MCHEZO WA BENDERAFUATA UPEPO SIJUI UTAISHA LINI.
    SIJAONA KITU CHOCHOTE ALICHOBADILISHA HUYU MAXIMO,YAANI UNAWEZA KUJISAHAU NA KUTAKA KUINGIA UKASAIDIE,YAANI KOCHA NA WACHEZAJI WAKE HAWANA AKILI YA KUCHEZA MPIRA KABISAAA..........
    KUMBUKA KILICHO UWA TIMU KABISA NI MBINU ZA OFFSIDE/OFFSIDE TRICKS MARANYINGI SIO ZAKUZITUMIA KWA WATUWALIONA SPEED.DEEZ

    ReplyDelete
  14. Adolph RugeraNovember 06, 2009

    Maximo kazi imemshinda,lazima ang'oke hana jipya,hivi kwanini tusibadilike? Mbona Kevin Keegan pamoja na kupendwa na waingereza wenzake,timu ilipovurunda walimtimua? Hana jipya,its time for him to leave,no way out.

    ReplyDelete
  15. mPIRA ULIKUWA AIBU KUUANGALIA MAAN KIPINDI CHA KWANZA JAMAA WALITUNYANYASA KAMA SISI YOSSO VILE.
    kWA UJUMLA HATUNA MPIRA....

    ReplyDelete
  16. Hapa goli letu linaonekana;
    http://www.youtube.com/watch?v=i5ecMNh51KM&NR=1
    siri ya magoli ujasiri wa kushuti na kulenga.

    ReplyDelete
  17. KWA BAHATI MBAYA MKUU WA WILAYA MAONI NILIYOKUTUMIA KUPITIA E MAIL YAKO BINAFSI HUKUYAWEKA HEWANI.
    NIMEUTAZAMA MTANANGE JANA USIKU, VIJANA WETU BADO NI MCHEKEA VIBAYA MNO.
    HAWANA LISHE, HAWAWEZI KUMILIKI MPIRA WALA HAWANA UJUZI WA KUSOMA MOVEMENT ZA MPINZANI.
    WAMENITIA SIMANZI MNO INGAWA ILIKUWA FRENDI GEMU.
    INABIDI KUWE NA MKAKATI WA KWELI, HASA KWA VIONGOZI. VIONGOZI WAPELEKWE NJE KUSOMA NAMNA YA KUIANDAA TIMU.
    SIAMINI VIJANA HAWA KAMA WANA LISHE YA KUTOSHA.
    WACHEZAJI WANAOKOTWA OKOTWA TU NA WALA HAKUNA MAANDALIZI JUU YA CHAKULA GANI WALE, WALALE SAA NGAPI, WAISHI MAISHA YA AINA GANI, WAFANYE MAZOEZI KIASI GANI.
    MIMI NAKUMBUKA NILIPOCHEZA LIGI HUKO NYUMBANI, HATUKUWA NA MPANGILIO WA CHAKULA WALA HATUKUPANGIWA NYAKATI ZA KUPUMZIKA NA KULALA.
    KAMA KWELI TUNATAKA SOKA LETU LIKUE, TUFANYE MAANDALIZI YA MAANA.
    WADAU KAMA SHEIKH LIKI ABDALLAH NA MHESHIMIWA MICHUZI NA WENGINEO WAPEWE NAFASI YA KUTOA USHAURI, WANA UTAALAMU FULANI.
    TUSIENDEKEZE TENA KUJENGA MATAWI YA LIVERPOOL, MAN U, CHELSEA, JUHUDI ZETU TUZIELEKEZE KATIKA SOKA LETU LA NYUMBANI, MAANA HAWA WANGEREZA HATUNUFAIKI NAO KWA CHOCHOTE TUNAPOWASHABIKIA, WALA HATA HAWATUTAMBUI. SIMAANISHI TUSIENDELEZE MARADHI YA KUPENDA TIMU ZA KIZUNGU, MAANA NDOO TUSHALEMAA TENA, LAKINI KWANZA TUPENDE CHETU.
    MDHARAU KWAO MTWANA.
    NAAMINI TUNAO VIJANA, KAMA WAKIANDALIWA, WANAWEZA KABISA KUTAMBA KATIKA SOKA LA AFRIKA HATA LA DUNIA, KAMA WAGHANA NA WAMISRI NA WENGINEO WANAVYOFANYA.
    WADAU WASIWE TU NA FIKRA ZA KUPONDA, BALI WAWE WAZALENDO.
    KAMA HUNA UZALENDO BORA ZIBA MDOMO WAACHIE WAFURUKUTWA KAMA MIMI WASEME.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  18. hao egypt nao wachovu,wametualika sisi vibonde ili wawatishe ALGERIA,katika mechi yao ya mwisho ya qualification za world cup tareh 15 november.ila wameula wa chuya mwendo ni ule ule watazikwa tuu,mechi ya mwanzo walifulia 3-1

    ReplyDelete
  19. Nimechoka na uzalendo wa kijinga. Mijitu iliopo TFF ni ziro jamani tukubaliane. Hawana mpya na kiukweli hata tukiwaondoa nani atajaza nafasi hizo?? Uchaguzi wa timu ni upendeleo na una angalia sana siasa. Nilisema sana kwamba mpira hatuuwezi kwanini tunajilazimisha?? Hata tukileta kocha toka mbinguni akili zenyewe za kukojoa kwenye masinki haya ukipewa maeelezo utelewa vipi na kichwani ni ziro?? Upeo mdogo,uwezo mdogo,nk

    Sasa hata kama TFF mshapata panga jamani tuchague mechi tunazolingana nazo kiuwezo ku build confidence si kwenda jizalilisha. Hii mijamaa iliwatoa nishai Cameroon kama wamesimama kwenye fainali ndio tutawaweza sisi?? Kama mnaelewa kiarabu tunavyozalilika ni Aibu tupu.

    ReplyDelete
  20. goli letu limefungwa na kigi makassi...ila magoli tuliyofungwa ni makosa ya mabeki na kipa pia kachangia...maximo has no option but to recall kaseja back to the team whether he likes or not hiz the best goalie we've had inthe past 6 yearz

    ReplyDelete
  21. kocha han tatizo...ni wachezaji hao...kuvamia mavyakula...wamenda misri..wamevamia biryan..hawajiwezi....

    ReplyDelete
  22. Watanzania 2vuteni subira kufungwa 5-1 aimanishi timu ye2 ni mbaya.Najua wengi 2nataka timu ye2 iwe kama Ghana au Ivory Coast ukweli ni kwamba mda we2 ni bado. 2natakiwa 2jicheze kwa bidii na juhudi zote, pia kosa le2 kubwa 2naogopa majina wao ni wa2 kama sisi na wanacheza mpira mmoja. La mwisho ni kufungwa twafungwa lakini chenga twawala...Mtawala

    ReplyDelete
  23. 2shachoka kusubiri timu ye2 itafanya vizuri mwaka gani na sisi 2jisifie 2kiwa na mataifa mengine? Kila mwaka timu ye2 inapikwa 2 itaiva lini? Huu ni wakati wakusema basi. Wachezaji nao inabidi muji2me sio 2namlaumu kocha, ndio kocha anafundisha lakini majukumu yote yapo kwa wachezaji au munaogopa majina? 2fanyeni biidi 2014 twende brazil 2kaiwakilishe nchi na africa kwa ujumla

    ReplyDelete
  24. Du, kwa wenye kumbukumbu ya mpira, wamisri walishatufunga goli 5-0 miaka ile ya kina stephen nemes na mohammed hussein (sina uhakika kama walicheza mechi ile lakini). Nadhani tumejijengea kisaikolojia kuwaogopa hawa watu. Kingine, kuna kitu ambacho siwezi kuelezea, hawa wachezaji wana morali zaidi wakichezea vilabu vyao kuliko timu ya taifa, imekuwa hivyo miaka mingi sana, sijui ni kwa sababu gani. Badu tu kichwa cha mwendawazimu.

    ReplyDelete
  25. Sina mengi ya kusema kwa kuwa nina hasira!! Kwa ufupi kosa kubwa si la kocha ila ni wachezaji. Sidhani kama ni kazi ya kocha kufudhisha tackles!! Ingawa kocha nae yupo responsible kwa kuchagua wachezaji ambao hata ku tacke hawawezi. Uliona wapi mshambuliaji anamtackle beki baada ya beki kumtackle yeye? Hivyo si dhani ni vitu ambavyo kocha napaswa kufundisha ila ni biddi maalum ya mchezaji mwenyewe. Hakiyamungu wanacheza kama watoto wa shule?? Mnawatoa wapi hawa?? Hii ni aibu! Jamani jamani jamani taifa linakwenda wapi hili?? Hivi tutakaa tunajidanganya mpaka lini?? Hivi mnadhani hao Ghana wamefika hapo kimasihara?? Walichapwa watu, walifukuzwa watu vibarua mpaka leo hii unaona mambo yanakwenda fresh. Lawama si za kocha peke yake bali uongozi wote wa TFF kwa ujumla. Ni nani aliyekubali mwaliko wakati anajua timu imesamabaratika? Katibu nae awajibike!! Kocha kwa nini ukampanga Kipa Mustafa Bartez ambaye ni kipa namba mbili wakati kuna kipa namba moja Shabani Dihile katika msafara?? Hivi wewe ulidahani unacheza na Honduras kule kwenu kwa taarifa yako watu hawauzi sura katika soka ya Africa, ukileta ubrazili wako utapigwa 10!! Nyie wabrazili ndio maana hamna rekodi nzuri ya usoka nje ya Brazili kwa kuwa mna kiburi mnadhani mpira unachezwa Brazili tuu!! eeeenhe sasa umekiona cha mtema kuni tano dah!! Noma!! Na unabahati ukupigwa 10!! Hebu baba fungasha virago urudi kwenu!! tafadhali bab hatutaki matatizo!! We are giving you only 20 days to resign if you don't you will see what come after!! Thanx!!

    ReplyDelete
  26. Mimi nashauri watu kabla ya kuchangia watazame kwanza mchezo wenyewe. Kuna jamaa hapo juu anasema eti kilichotuua ni kucheza offside trick!! Jamani, umeona wapi kwenye hayo magoli mtu kacheza offside trick, au kwa kuwa tu umesikia kwa mtu "offside trick" basi lazima uongee?

    Kocha hana kosa lolote lile, sijawahi kuona kocha anafundisha kukwepa mipira hata siku moja. Kipa hana kosa lolote na magoli yote hata angelikuwa kipa gani angefungwa tu, mabeki wamemzingua na kuziba afanye nini?

    Wachezaji wanakimbia kimbia tu hawachukui positions zozote, wanafuata tu mpira. Inamaana hawa wachezaji wetu wa timu ya taifa hawana TV kwao kutazama hata mechi za wenzetu waone wanajipangaje?

    Hata akija Yesu au Mohamad mtume kufundisha timu ya BOngo, wachezaji vilema wa maungo, viziwi hawasikii, kiburi mtindo mmoja mbaya zaidi wanaingia mazoezi washa vuta msuba. Hata ufundishe namna gani, mafundisho yako yote yanaishia juu ya msuba (Bangi), bangi ikiisha tu kichwani na yote ulosema, kuonesha yanaondoka. Unarudi back to square 1.

    UTUMBO UTUMBO

    ReplyDelete
  27. tatizo la bongo ni kuchanganya soka na siasa,yan watu wanadhamini sana mpira au mechi ya simba na yanga na kuona timu ya taifa ni kama timu ya mzaha tu..ukiangalia wachezaj wanavyojituma kwenye mechi ya simba na yanga na ukilinganisha wanapokuwa na timu yao ya taifa utaona ni tofauti kabsa!!!kifup mpira wa bongo ni simba na yanga mengineyo ni porojo!!!aibu tupu !!!

    ReplyDelete
  28. MAXIMO hatufai kabisa, hataki ushauri, anatuharibia timu yetu, hata akikaa miaka kumi hatutoenda mbali, huu ni mwaka wa nne bado anasema anajenga timu. wachezaji tunao wazuri wenye vipaji,hawachagui, madai yake anachagua vijana, MAXIMO anachagua makipa ambao hata katika Klabu zao wanawekwa makipa wa akiba. MAXIMO akimrudisha Kaseja, Haruna Moshi na Athumani Iddi timu yetu itafanya maajabu, vinginevyo tutaendelea kufungwa tu, hata kombe la EA Challenge tutatolewa tu sisi hatuna tofauti na Zambia, DR Congo, Senegal

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...