Golikipa wa wa Mtibwa Sugar, Shaban Hasn akiokoa mpira miguu mwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi katika mchezo wa ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar wikiendi. Simba walishinda bao 3-1.
Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassani Mgosi akiruka daruga la beki wa Mtibwa, Idrisa Rajabu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru wikiendi.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuinyuka Mtibwa Sugar mabao 3-1 timu ya Mtibwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. inapendaza! kazi nzuri sana Simba mwaka huu!!
    hapo ndo tofauti na ni mbinu zinazotakiwa kuigwa na kuenziwa na taifa zima, hakuna cha mchezaji mrefu au mnene watu wanaweza wapeni nafasi tu. ujumbe umefika!!

    ReplyDelete
  2. kwanini simba na phiri isiwe timu ya taifa?
    karibu nyumbani kaseja

    ReplyDelete
  3. JAMANI naomba kama mtu anayo website ya simba anipatie tafadhali

    ReplyDelete
  4. WATANZANIA TUAMKE TULIKO LALA, HUYU KOCHA WATAIFA NA TENGA WAKE NI WABOVU, KASEJA KAKOSA NINI AMBACHO TAIFA HALIWEZI KUMSAMEHE,WEWE UMEONA WAPI KATIKA DUNIA HII MCHEZAJI MZURI HACHUKULIWI TIMU YATAIFA , KAMA ANAMATATIZO BASI FAT NDIO WAKUSEMA SIO MAXIMO, KUMBUKA TENGA MAXIMO ANACHUKUA PESA ZA WALALA HOI HALAFU ATAONDOKA ,WEWE NDIO WENYE NGUVU HAPO SIO MAXIMO,HATA CAPPELO HAWEZI KMUACHA ROONEY INGAWA HANA NIDHAMU, MBONA RIO KAFUTA BANGI NA SASA NI VICE CAPTAIN WA ENGLAND, MTOTO AKINHIE KIGANJA HUKATI MKONO ILA HUUSAFISHA NAMAJI NA SABUNI,TENGA AMKA ULIKO LALA ACHA KUWA MZIGO WATAIFA

    ReplyDelete
  5. Soka siku hizi ni sayansi inayoambatana na mbinu, maarifa, na ujuzi. Tafauti kocha mbunifu na na wale makocha ambao hutegemea miujiza ndo hii! Hii ni type ya kina Morinho, Carlo A. ambao wakisimama mahali kazi zao lazima zionekane.
    Hongera wekundu

    ReplyDelete
  6. kikosi cha taifa hiki hapa

    1.kaseja

    2.nyoni

    3.jabu

    4.yondani

    5.swed

    6.banka

    7.ngasa

    8.chiji

    9.mgosi

    10.mrwanga

    11.kazimoto

    kocha mzirary mshauri juma mkamia

    ReplyDelete
  7. Anon Nov 16, 12.40 pm try this website - www.simbasportsclub.com

    ReplyDelete
  8. Mon Nov 16, 12:48:00 PM kama wewe ni mfuatiliaji wa mpira usingeandika hivyo. TFF hawana makosa kwani hata kwenye listi ya makocha waliyoipeleka kwa JK huyo maximo hakuwepo,, so huna point hapo huyu ni kocha aliyeletwa na serikali na ambaye anafull control na timu haingiliwi na mtu.Na TFF wanaheshimu maamuzi ya mkuu. Atakae mtoa maximo ni aliyemleta

    hongera TFF tunajua mmeitoa wapi FAT ya Ndolanga na mpira wa tz

    ReplyDelete
  9. SASA MBONA KIKWETE KAWAMBIA TFF AJIANDAE KUMLIPA MSHAHARA, NYINYI NDI WALEWALE TIMU HAINA MUELEKO, HATA NDALONGA ANGEPEWA MSADA NA SERKALI ANGEKUWA MZURI,TOKA MAXIMO AMECHUKUA TIMU KAFANYA NINI CHA MAANA,KAZI KUBWA ZENGWE TUU, MPIRA NI SAYANSI SIO MANENO MATUPU,WEWEW UNA JARIBU KUMTETEA TENGA LAKINI TENGA KABORONGA HANA JIPYA, MPAKA LEO HII MAREFA WANACHUKUA RUSWA DHAHIRI, ANA PENDELEA YANGA DHAHIRI, SASA TUTAFUTE KOCHA MWINGINE AMBAYE ATATUPELEKA MBALI , KWANI HAT FANALI YA CHALENJI HATUTAIONA MWAKA HUU

    ReplyDelete
  10. Wabongo kwa kuchanganya mambo? Simba na taifa stars wapi na wapi,tujadili simba -ambayo inatisha kwa rekodi mechi 11 point 33,naomba rekodi zaidi katika hii kwa Afrika,then dunia nzima.
    big up simba-na kaseja lazima arudi stars maximo atake asitake.

    ReplyDelete
  11. WEBSITE YETU WANA LUNYASI TAIFA KUBWA NI:
    www.simbasc.com

    AHSANTE WADAU

    ReplyDelete
  12. Kama MUNGU anasamehe why not u Maximo? Mogoro gani usieisha. Wekeni kikao myamalize 2nataka kuiyona Tz inaenda mbali. Maximo ni Kocha mzuri ila ana kigeugeu mda mwingine I cant stand him.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...