Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni akinadi saa yenye picha ya Spika katika tamasha la injili na Kusaidia walemavu jana katika uwanja wa CCM Kirumba. ambapo Jumla ya Tsh 49, 9850 zilipatikana baada ya wananchi kujichangisha kwa lengo la kumnunulia Spika Saa hiyo na fedha kutumika kusaidia walemavu mkoani Mwanza. Spika alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo.

Mhe. Chegeni akikusanya michango kwa ajili ya kununulia saa yenye picha ya Spika. Chini waimbaji wa injili wakimkabidhi Mh. Spika saa hiyo

Rose Mhando na kundi lake wakitumbuiza kwenye tamasha hilo
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akipokea tuzo kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania ikiwa ni kutambua mchango wa Spika katika kuliongoza Bunge la Tanzania kwa ujasiri mkubwa haki na uadilifu chini ya kauli mbiu “kasi na viwango”. Spika alipewa tuzo hiyo jana mjini mwanza mara baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la injili na kusaidia walemavu katika uwanja wa CCM kirumba – Mwanza. Toka kushoto ni John Shabani, afisa habari wa Christian Promoters ambaye ndio wadhamini wa tamasha hilo na Bi Stella Joel, Mwimbaji wa nyimbo za Injili.

Spika Akifurahia tuzo yake

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akikabidhi Fulana, kofia na mafuta maalumu kwa ajili ya walemavu wa Ngozi, Miamvuli, na vyakula katika hafla iliyofanyika wakati tamasha la injili na kusaidia walemavu katika uwanja wa CCM kirumba – Mwanza. Spika alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AMEEEEEN! Hizo ndo shughuli zitakiwazo kwa saaana. Ila nina wasiwasi na hiyo michango km itawafikia walengwa! maana Bongo wajanja wengi huziweka mifukoni badala ya walengwa. Mungu awabariki mliondaa, kuhudhuria na kuchangia onyesho hilo.

    ReplyDelete
  2. HONGERENI ILLA, KWA SASA NAONA IMEKUWA KWA SAANNA, NADHANI UCHAGUZI UKO MACHONI KILLA MBUNGE ANALIA KIVYAKE TUNAONA SASA NJIA ZA KUJIPIGIA DEBE KWA MBINU MPYAx2 ZA KILA AINA KWA WABUNGE WOOTTE

    ReplyDelete
  3. Nyie wasanii wa \injili muogopeni Mungu! Wewe John Shabani umechukua hela za watu Dar hujaonekana kumbe upo Mwanza!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Mhe chegeni uko juu,mungu atakusaidia

    ReplyDelete
  5. rubbish!!!

    siku hizi mgeni rasmi anapewa zawadi? hao ni kweli wanamtukuza Mungu au wanapigia mwanadmu kampeni, tena asiyefaa!!
    hakika moto wa kifuu cha nazi unawasubiri.......

    ReplyDelete
  6. wadau samahani mimi niko ulaya na mambo mengi ya tz yananipita sababu ya box,kwani spika wa bunge bado mzee sitta sio mama sijui anna abdalaha au anna makinda???au ni spika mstaafu???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...