Stars United FC

Stars United FC ni timu inayoundwa na wachezaji wa kibongo kutoka state mbali mbali nchini Marekani, leo jumatano itaanza safari yake kuelekea Houston kwa mechi ya kutafuta kikosi kitakachoelekea Sweden Mwakani.

Mechi itachezwa jumamosi nov 28 na mchanganyiko wa timu ya Houston(Serengeti Boys) na Minnesota(Kili Stars) kwa pamoja wataunda timu moja,baada ya mechi yao kumalizika.

Stars United safari hii itamkosa kiungo wake mahiri Elvis Dotto kwa kukosa ruhusa na mwajiri wake na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Mudrick Majaliwa anekwenda nje ya nchi kwa majaribio na timu ya Fanja F.C.beki mahiri Adam Zimbwe naye hatasafiri na timu kwa sababu za kifamilia,mwingine ni Vicent Ndusilo na Sean Shaban nao hawatasafiri na timu kwa sababu za kifamilia na Seif Kadri Ndosa ambae bado ni majeruhi.

Stars United imeongeza nguvu ya wachezaji Muly na Rahim(Masachusetts),Edgar na Juma(Atl),na foward kali,Innocent Geofrey(Nc) wengine watakao ongozana na timu Hadji Helper(Atl), Evans Shangarai,Libe Mwang'ombe,Yahaya Kheri,Gilles,Lemy Mhando na Steav Majumbo(Dc),Ebra Nyangaly,Tifu(Ny),Fesal Njenje,Hamfrey Owen,Simon Marko na Denis Geofrey(Nc).

Stars United Wataingia Houston Alhamisi nov,26 na kufanya mazoezi mepesi kabla ya mpambano wao jumamosi,wachezaji wako katika hali nzuri ya mchezo na wenye ari kubwa ya ushindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. vimetumika vigezo gani kuichagua hiyo timu,mbona kuna watu wengi tu wanakanyaga ngozi kinoma hawapo?

    ReplyDelete
  2. Wana endelezeni libeneke. Huku UK ni upemba kinoma. Hamna lolote isipokua huyu Muunguja yule mpemba na yule ni Mbara.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  3. Hadji helper naona wewe uko everywhere.

    Mpira wa miguu wewe ni staa, baby powder wewe ni staa-umejaaliwa vipaji.

    Keep it up my braza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...