hapa si pengine ila ni mgahawa maarufu wa liverpool restaurant iliyopo mombo ambapo mabasi karibia yote ya dar-arusha-dar na kwengineko kwenye njia hiyo kuu ya kaskazini hupiga breki ili abiria wapate dina la mchana.
kwa vile konda anakupa dakika 15 tu ya kujipatia mlo inabidi ufanye fasta kuagiza na kula kwani kadamnasi huwa kubwa na kila mtu hataki kuachwa
ndani ya anfield ya mombo
pia kuna Babu Nyonda ambaye anakupatia huduma ya kutangaza basi gani liko tayari kuondoka na abiria kama hajamaliza abebe anachokula ili aondoke la sivyo ataachwa...
pamoja na kwikwi msimu huu angalau anfield ya mombo inampa anko sababu ya kuishi kwa matumaini





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. yaani mkuu umeenda kwa ndege unarudi kwa basi,bora ungeanza na basi halafu umalizie na mwewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...