ankal akijiandaa kuanzaa trayo na timu ya Desperados FC ya mjini Bujumbura, Burundi leo. kulia ni kipa wa taifa wa Burundi na Azam FC ya Dar Vladimir Niyonkuru ambaye huwa anakula tizi na timu hii awapo mapumzikoni. anarudi Dar jumamosi kujiandaaa kumalizia ngwe ya ligi kuu. Na Desperados FC imeialika timu ya Sugar Rays ya Dar kuja hapa kukipiga karibuni
ankal akiwa na baadhi ya wachezaji wa Desperados kabla ya kuanza trayo.wa tatu toka kulia ni sam shelukindo namba mkagha wa timu hiyo
ankal akiingia kuanza trayo na Desperados FC. hadi tunaenda mitamboni majibu yalikuwa bado kutoka ingawa inasemekana pamoja na kutunguliwa bao 3 akiwa golini kama nyanda, ankal akila tizi la nguvu anaweza kutupiwa jicho na maximo...hahahhaaa
ankal na mwanamke wa Burundi wa mwenye beji ya FIFA Eline Biagoye ambaye huwa anakuja kula tizi ya urefa kila jumapili na Desperados FC. kwa mnaokumbuka huyu mama ndiye aliyechezesha mechi ya wanawake kati ya Tanzania na Cameroun neshno
Jumapili ni siku ambayo vijana kwa wazee hapa buja hukutanika kucheza michezo na kufanya mazoezi. mitaani utakuta makundi makubwa ya watu wakifanya jogging. jumamosi kuanzia alfajiri hadi saa tano huwa kila mmoja yuko mitaani kufanya usafi ama kazi ya jamii. ofisi na benki hufunguliwa baada ya hapo. ankal anadhani huu ni mfano wa kuigwa ambapo siku hizi toka jumamosi itengwe kuwa sio siku ya kazi hakuna anayejishughulisha na kazi za jamii

Ankal wafungwa lakini chenga wawala ati....!
ReplyDeletekifriji kinajiba hadi kwenye uzi wa bwawa he he heee bora ule tizi
ReplyDeleteankal unakumbuka au umesikia kuwa utamaduni wa kufanya kazi za kujitolea za kijamii ulikuwa umeanza kuwa na mashiko enzi za Mwalimu! Watu walikuwa na moyo wa kujitolea kwa sababu hapakuwepo na ufisadi wa waziwazi. Leo hii katika enzi za 'posho' utamwambia nani ajitolee kusafisha mtaa wake? Tumefika pahala ambapo hata mkutano wa nyumba kumikumi wa kujadili masuala ya mitaa yetu tunadai posho kwa sababu ndio utamaduni ambao tumeamua kuujenga. Hizi ni zama za posho, sahau kazi za kujitolea!!!!
ReplyDeleteWaburundi wanawake wanavipiga nakumbuka wakati nasoma Uganda walikuwa wanaweka game za wanawake huwa wanavipiga si mchezo.
ReplyDeleteAnkal,isije rejeta ikachemsha
ReplyDeleteFadhali ankal ukate kitambi hicho! Najua hapo rejeta lazima ilichemsha!
ReplyDeleteAnkal, waombe ambulance ikae uwanjani standby, just in case.
ReplyDeleteAnkal misupuuu, mbona uko ndani ya trousel? Au we ndo umezoea?
ReplyDelete