Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Batilda S. Burian leo ametembelea Kiwanda cha kurejeleza (recycle) chupa za plastiki cha Bakharesa kilichopo Chang’ombe jijini Dar.
Mh. Dkt. Batilda amesema amefarijika kuona kuwa sasa kuna Kiwanda cha kurejeleza chupa ambazo zilikuwa uchafu na kero katika Miji hususan jijini Dar
Mhe. Dkt. Batilda amepongeza Kampuni ya Bakhresa kwa ukusanyaji chupa na kuzirejeza. Amesema kuwa urejelezaji wa chupa hizi utasaidia katika kupambana na uchafuzi wa mazingira na kusaidia kuwapa kipato wauzaji wa chupa za plastiki zilizotumika.
Alisema chupa nyingi zinazoletwa ni chafu kwa hiyo zinahitaji kusafishwa katika mtambio maalum uliopo kiwandani ambapo bidhaa inayozalishwa huwa salam. Mhe. Dkt. Batilda amesema Serikali tutaendelea kuhimiza utengaji wa taka hivyo kuweza kurahisisha urejelezaji.
Mhe. Dkt. Batilda alisema kuwa Ofisi yake itahahakikisha kuwa vinaanzishwa vituo vya kukusanya chuo hizo na kuleta Kiwandani na watalipwa pesa zao.
Dr. Burian Mash Allah unapendezaga sana. Hongera sana Mheshimiwa, ni mfano wa kuigwa, Allah akuzidishie Ameen
ReplyDeleteUKUSANYAJI WA CHUPA UMELETA UCHAFUZI MWINGINE UNAOTOKANA NA WAKUSANYAJI KUTUPA HOVYO VIFUNIKO AMBAVYO INAONEKANA HAVIHITAJIKI KIWANDANI, NALO HILO LINAHITAJI UFUMBUZI.
ReplyDeleteMh. Waziri kapendeza Mashallah na wala humsikii katika kuropokaropoka na kujiingiza katika malumbano yasio ya msingi.
ReplyDelete(US Blogger)