JK akipokewa na Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere akitokea Trinidad na Tobago pamoja na Cuba ambapo alihudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Madola na kufanya ziara kikazi nchini Cuba na Jamaika. Katikati ni Bw. Jumaa meneja wa Emirates uwanjani hapo
JK akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea nchini Cuba na Visiwa vya Trinidad na Tobago ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Madola. Pembeni yake ni Makamu wa Rais Dr. Ali mohamed Shein.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Doh! JK naona Safari ya Latin Americans na Carebian tayari ameshaanza kuweka vunge,ANGEBAKIA KWA WIKI NYENGINE TU TUNGEMUONA NA RASTA KAMA MZEE BURNING,Nafikiri alikutana nae ndio maana amewacha tayari vunge ili aweke dreadlocks

    ReplyDelete
  2. JAMANI WATU MMEKUWA KAMA VILE MNAMSIKILIZA MUNGU AMBAYE HAULIZWI MASWALI YA KWA NINI YULE ULIMUUMBA VILE NA MIMI UMENIUMBA HIVI! HUYU NI MTU KAMA NYIE AND BEING ON TOP OF THE JOB IN THE COUNTRY NI AJIRA TU KAMA AJIRA ZINGINE AMEAJIRIWA NANYI CHANGAMKENI, MBONA HOFU HIVYO, HAIPENDEZI MWA JAMENI, OR THAT IS DISCIPLINE AT ITS BEST.

    ReplyDelete
  3. mheshimiwa kaja na jipya lipi?

    ReplyDelete
  4. i guess.. ndege ya mkuu imerudi kuweka wese tayari kwa safari ya copen hagen!

    ReplyDelete
  5. nasikia mheshimiwa ameshituka kuondoka nchi kwa wiki kadhaa amekuta mapinduzi ndani ya chama. hii ndio maana ya "chama cha mapinduzi" chochote kinaweza kutokea. mimi binafsi najua kiongozi kukosolewa ni jadi hasa nchi ikiwa inataka kufuata demokrasia. watu wote wanaosema kwa nguvu ni well wisher wa kikwete.wanananchi wasiposema outcome yake disaster no one need this....HII SIO CHUKI ni free speech.

    ReplyDelete
  6. kuna kitu nimenote.Mheshimiwa aliondoka na ndege ya serikali kale kadogo.alipotoka Jamaica kwenda Trinidad alikuwa nako.toka trinidad kwenda Cuba nikaona kapanda ndege ya abiria ya kawaida.sasa nashangaa karudi na emirates.Najiuliza kale kamefia njiani au la.pili kumbe inawezekana akapanda ndege za kawaida sometimes na kupunguza gharama.

    ReplyDelete
  7. Mbona umechelewa kuja Copenhagen kaka? Tunakusubiri

    ReplyDelete
  8. kazi kwelikweli...

    baba umerudi?nchi tunakuitaji ututatulie matatizo ya ufisadi,ujambazi,uhalamia mbugani,mikopo vyuo vikuu,sekondari za vodafasta,kutekwa watu na kudai pesa,mishahara ya walimu/wastaafu wa afrika mashariki nk nk

    ReplyDelete
  9. Michu,

    Kwa kuwarusha maswahiba zako kama kawaida yako!!

    Huyu Abubakari Jumaa kulikuwa na umuhimu gani kwa kumuandika,kwa ni yeye ni kati ya maofisa wa Serikali?

    Au ndio zile style za maejee, baba Jumaa....

    Niliona hata katika sherehe za TASOTA ulimrusha sana.

    Acha hizo, kuna vitu vya maana na havichafui hali ya hewa unaviweka kapuni!! Ujue kama kila kitu kina mwisho wake, hata hii globe itafikia mwisho.

    Ahsante,

    Mtanzania,
    tmajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. Mkapa aliona mbali kununua Gulf stream Jet. alijua Rais ajae amekula miguu ya kuku utotoni.

    ReplyDelete
  11. Rais kufanya safari za nje ni vema kabisa kwani zinampa nafasi ya kukutana na viongozi wa nchi nyingine na kuzungumza mambo mbalimbali ambao mengine ni muhimu kwa nchi. Kitu cha msingi hapa ni rais kuwa na muda wa kufanya kazi za ndani ya nchi na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo. Hivyo rais aende safari nje lakini asitumie muda mwingi sana nje ya nchi kwani yeye sio waziri wa mambo ya nje. Shughuli zingine amwamchie waziri wa mambo nje, pia makamu wa rais anaweze kwenda kwa niaba ya rais endapo rais anaona ni muhimu mtu wa ngazi ya juu ya uwaziri kuwakilisha nchi.

    Safari za makongomano sio lazima kwa rais kwenda, kwa sababu mazungumzo huko yanakuwa sana ya jumla jumla. Kama Copehagen Kikwete anakwenda kufanya nini, je makamu au waziri hawezi kwenda huko?

    ReplyDelete
  12. Suala la watu kutoa maoni yao kwa rais kuwa afanya maamuzi magumu nadhani ni maana zaidi kwani lina maanufa kwa watanzania wengi.

    Rais asiingie kwenye malumbano na kujibu hoja za wananchi ovyo na kuwaita watu wanaotoa dukuduku zao wehu.

    Kuongea ovyo kwa kiongozi wa juu wa chama ni kukusa maadali. Kwa waungana siku zote ustarabu ni
    kujibu hoja kwa kutumia hoja si watusi.

    Naompengeza Kikwete kwa kasema kuwa atapita kwa makini taarifa zilizopo na atajibu hizo hoja. Na hoja zingine ambazo havina tija kwa atazipuuza tu.

    ReplyDelete
  13. JK, Nikuambie kitu? Jana daladala ziligoma na tulishindwa kabisa kwenda makazini hakukuwa na usafiri na hatukuwa na hela hata ya kukodi kibajaji.

    Ndimi mwathirika wa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

    ReplyDelete
  14. Kaka Michuzi,
    Kuna tetesi kuwa Mheshimiwa alikuwa alifanya ka-Ziara Marekani nchi anayoipenda sana. Mbona kwenye taarifa yako sioni ukiwaeleza wananchi nchi zote alizotembelea.Alikuja na Emirates akitokea Dubai, Marekani...Kaka Michuzi hebu tueleze vizuri wanachi tuelewe.
    Na ke-ndege ketu kaliachwa wapiii?
    sisi ni walipa kodi nadhani ni vyema tukaelzwa mzunguko mzima wa Rais wetu.

    Sasa na huko Denmark..anaenda tena..Kufanya nini.? Si kuna makamu wa Rais, Waziri Mkuu...hawawezi kumwakilisha???

    ReplyDelete
  15. Thanks God, mtalii wetu amerudi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...