JK na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na warembo wa Miss East Africa na kamati nzima ya mashindano hayo mara baada ya chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu usiku kuamkia leo. Warembo hao kutoka mataifa saba kesho watachuana katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar na mshindi atapata gari aina ya Toyota Celica Sports yenye thamani ya dolla 24.000.
JK akipiga stori na warembo wa Miss East Afrika


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Mr.Presidenteee najua ni vizuri lakini jua Khali ya Wannanchi ni ngumu ,Ni Afadhali ya jana Pesa huku imekuwa tabu kuliko ,Siku hiz Elfu 10 km elfu 1000,Liangalie na hilo tuangalie sisi pia jamani maana Sikuhiz aliye nacho anacho asiyekuwa nacho basi....,Huku Mjini hiv sijui huko Vijijini kukokoje maana

    ReplyDelete
  2. Ni lini Jk ataita wataalam wa uchumi ikulu?

    tumeshaona taifa starts,Hashim Thabiti..tunahitaji wachumi nao wapewe nafasi ya kukutana naye na kujadili masuala muhimu zaidi!

    sifikiri kuona haowa kipiga picha na Jk.

    Obama juzi kaita MA CEO wa mabenjki yote makubwa na kuzungumza nao

    ReplyDelete
  3. presidar natumai utawakaribisha na vijana waliofanya vizuri kwenye masomo yao kutoka vyuo mbalimbali (graduates), secondary six and four then darasa la saba.
    si ndiyo mkuu????

    ReplyDelete
  4. Vizuri kaka michuzi kwa kumuonyesha Mh.JK akiwa na warembo Ikulu na basi kama angekuwa anafanya mapokezi kwa wanasayansi na wakulima maarufu hapo Ikulu hata mara moja kwa mwaka basi bongo tungekuwa mbali sana. Inabidi viongozi wetu wajifunze mambo yanayofanywa na viongozi wenzao nchi zilizoendelea. Mapokezi ya hawa madada yalitakiwa yafanywe na waziri wa michezo na utamaduni.

    ReplyDelete
  5. Soul searching!!!

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLELADecember 18, 2009

    Mr. President,
    NAOMBA PIA MWESHIMIWA RAIS UITE WATU KAMA HAWA HAPA CHINI.

    Peter Nalitolela,(Naipenda TZ)
    Yohanna Mashaka (jiniasi wa uchumi)
    US-Buloga (Fisadi, majigambo)
    Hildebrand Shayo (Mgunduzi)
    Al-Musoma ( Anakomenti kila kitu)
    Issa Michuzi ( anahabarisha TZ)
    Aisha Madinda (Mnenguaji)
    Shigongo (Udaku)
    T.I.D (anapenda Uchawi)
    Duly Sykes (mpenda misifa)
    Mwamvita Makamba (analisha mayatima)
    Baraka Chibiriti (WA cESSNIA)
    Mama Lishe wote( wanalisha Taifa)

    wahitmu wote wa darasa la 7 kutoka kigamboni shule ya msingi kwa maana wako pale karibu na kwako


    TAFADHALI MKUU KARIBISHA HAWA WATU ILI TANZANIA IENDELEE NA ULIMBWENDE NA WAHITIMU WOTE CHUO KIKUCC CHA MUZUMBE UNIVESITY YA KULE MOLOGOLO

    ReplyDelete
  7. atawakaribisha hao wengine kwa wakati muafaka sasa hivi amejisikia kuwakaribisha visura msimpangie mr pesident madaraka kwani nyinyi ndo mnaongoza nchi?ebo!! raisi anathamini saaana michezo na hii pia ni michezo

    ReplyDelete
  8. Tunatraji siku noja atawaita wakulima na wafugaji bora ikulu!

    ReplyDelete
  9. its agood thing mr president,congrats, tunasubiri na wengine tualikwe, ni kweli hutotufikia wote ila makundi yatatuwakilisha, tatizo linakuja kama u dnt belong anywhere ndio m aneno yanaaza, wachumi anakutana nao kila siku....watanzania tuwe watu wakuapprritiate.

    ReplyDelete
  10. ha ha haa uuuwiii huyu peter nalitotela ni balaa ati tid anapenda nini?? kwa kwa kwaaaa haki ya nani wewe umepinda sana yani nimecheka sana mkuu wa nanihiii tunaomba ufanye mpango wa kutuwekea picha ya huyu peter nalitolela tumuone tu kama anaendana na vituko vyake manake comment zake zinatuachaga hoi bin taabani

    ReplyDelete
  11. next miss utalii ha ha ha ha ah

    ReplyDelete
  12. Du! sina la kusema yetu macho -- -- -- -- --.???

    ReplyDelete
  13. Bwana Michuzi! Sasa huyo mwezetu alikuwa anapiga picha au anatembeza sera... Haogopi hata mbele ya Presidar na Fastilad yeye kapotea ghafla. Anafanana na Mhe. fulani Waziri wa Mambo ya N.... je ni yeye? Kwanza kazi babu...

    ReplyDelete
  14. HAWA WALIAKWA NA MAMA SALMA TU. JK KWA SABABU IKULU NI HOME BASI LAZIMA ASALIMIE WAGENI WA MAMA.

    ReplyDelete
  15. wewe mtoaji mada anon 05:45am tafuta la kusema umiss sio michezo hiyo sijawahi kuskia

    ReplyDelete
  16. dah yaani nilipoona picha hii nimekumbuka story ya jarida la zamani sana la sani..kuna picha inamuonyesha mheshimiwa flani mstaarabu anasalimiana na ndumila kuwili wakiwa wamekumbatiana halafu kwa mbaaali kuna picha ya muungwana mmoja anasikitika huku akijisemea ''mama yangu weeee kakumbatiana na ndumila! keshaibiwa''..sasa hawa warembo wanakumbatiana na huyo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa sijui kama watapona...

    ReplyDelete
  17. Leo ni leo asiye na mwana abebe jiwe....wale waitrea wapo wapi, wale ndiyo walitakiwa wawe fore-front ili wauze onesho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...