Hizo ni posters za filamu mpya za Steve Kanumba zitakazotoka hivi karibuni. Ya kwanza itakuwa 'Saturday Morning' (chini) itakayotoka Jumatatu ijayo na kufuatiwa na 'Hero of the Church' ambayo imechezwa na wasanii kutoka Nigeria, Uganda na Tanzania


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. balghaatul mehboobhDecember 15, 2009

    eeh saturday morning tena? kumbe siku hizi kashajua kingereza huyu mjomba

    ReplyDelete
  2. wewe mwenye jina lisiloeleweka kama mzizi nani kakwambia kanumba hajui kingereza acheni uzushi wetu fanyeni kazi zenu nanyi zionekane c kuchonga tu

    ReplyDelete
  3. mi nnachotaka kujua ni kwa nini filamu zetu nyingi zina majina ya kiingereza, hasa siku za hivi karibuni? kama kuna mtu ana jibu anisaidie tafadhali.

    ReplyDelete
  4. Bandagalang'onyoDecember 15, 2009

    Poa saana Kanumba,upo juu,mimi ninakukubali na ni mpenzi wa filamu zako,kaza buti mwanangu,wanga wengi,wao wanaojua ki english mbona hatuoni kazi zao?wabongo hatupendi kuona maendeleo ya wenzetu,ndio maana tunakufa maskini.

    ReplyDelete
  5. Jamani kwanini wanapenda kutumia majina ya kiingereza? mbona inapendeza zaidi wakiipa majina ya kiswahili sababu naamini hiyo movie lugha inayotumika ni kiswahili.

    ReplyDelete
  6. Nashangaa na movi za kibong kila wiki zinatoka kibao ndo maan ubora sifuri smahani hizi sio movie bali ni maigizo yasio na kichwa wala miguu . kalagabaho hebu tiwe sereius kidogo tu na nina imani tunaweza

    ReplyDelete
  7. Kanumba hongera na ukaze buti kusikiliza maoni ya wateja wako.

    Unaona hata 'posters' tu zinakuonyesha utofauti. Yaani ya kwako kabisa (chini) ni poor in design & quality kuliko ya juu! Kibaya chajichembeza!
    Si lazima ujiweke kwenye ma 'posters' kila wakati.

    ReplyDelete
  8. kama ilivyo Nigeria kila filamu ya kibongo inayohusiana na dini utaona wanamuelezea Padri, Mchungaji au Kasisi kulikoni? mbona sizioni zinazomhusisha Shehe na Msaafu au hairuhusiwi? sometime waislam watakua wanatengwa manake nao wanahitaji mafunzo kupitia filamu jamani

    ReplyDelete
  9. kama ilivyo Nigeria kila filamu ya kibongo inayohusiana na dini utaona wanamuelezea Padri, Mchungaji au Kasisi kulikoni? mbona sizioni zinazomhusisha Shehe na Msaafu au hairuhusiwi? sometime waislam watakua wanatengwa manake nao wanahitaji mafunzo kupitia filamu jamani

    ReplyDelete
  10. MAJUTO WA BOX USWIDIDecember 15, 2009

    MIMI BINASFI SIZUNGUMZII KANUMBA KUJUA AU KUTOKUJUA KIINGLISH HILO NI SUALA LA KITAIFA' NA HABARI ZAIDI JUU YA HAO KINA KANUMBA WALIOMO SERIKALINI MTAISIKIA PUNDESIPUNDE,MIMI NAZUNGU MZIA SUALA LA WASANII WA TZ KUPENDA KUANDIKA VICHWA VYA HABARI(HEDING) VYA FILAMU ZAO KWA LUGHA YA KIINGEREZA HALI YA KUWA WANAELEWA FILAMU HUUZWA KWA KUTAZAMA NA KULIELEWA COVER NA ISITOSHE WATEJA WAO WAKUBWA NI WATU WASIO NA ELIMU NA WASIO NA KAZI.JARIBUNI KUBADILIKA ANDIKENI VICHWA VYA HABARI KWA LUGHA YA WATEJA WENU - mdau majuto-uswidi

    ReplyDelete
  11. hizi movie dizain za kinigeria ambazo zinakuwa na mambo ya kanisa kanisa si nzuri na to be honest kanumba hizi movie hazitakufikisha kokote wenzetu wasouth africa wanaact mambo ambayo yanakubalika kila kona a dunia ndio maana unaona wanapata sana mikataba holywood au hata wasani wa holywood wanapenda kuchukua story za movie kama skin,totsi,hotel rwanda n.k
    mimi ni mkristo na sizipingi hizi sinema kama utatoa movie moja basi nikupe story moja kuna mama wa kinaijeria actress maarufu sana ana movie yake ambayo eti inazungumzia uchawi wa watoto ile movie huwezi amini kwa kuwa ni ya dini na huyo mama ni mchungaji watu wakaanza kuuwa watoto eti wanawatuhumu kuwa ni wachawi wengine wanamwagiwa acid ,yaani mateso ambayo unashangaa,kuna wazungu walikuwa huko nigeria basiwakashangaa mbona mtaani watoto wengi na wengine wanamakovu wa kutisha kufatilia wakagundua ni noliwood basi kama unavyojua western media wamenyaka ni scandal kila siku madocumentary na huku ulaya wanajua africa ni moja basi aibu aibu ,kanumba naomba upate elimu zaidi sio kukurupuka tu kufyatua mamovie.sorry watu kama nimeboa

    ReplyDelete
  12. nafikiri swala la kuzipa filamu jina la kiinglishi ni target ya kuwapata wateja nje ya nchi. mfano nasikia cd nyingi sana zinauzwa nchi jirani congo,burundi,rwanda etc ambao kiswahili chao kina mipaka
    USHAURI: kasha liwe na majina yote mawili kiinglishi na kiswahili au kifaransa pia ili wengi waelewe

    singapore

    ReplyDelete
  13. si mnaona movie yenyewe kacheza na wanigeria? nyie vipi? kama Nigeria wanacheza mambo ya kdini dini basi ndio wenyewe waliopo kwenye movie hii na unazani watacheza nini kingine? Watanzania pia si mambo msiige? Kila movie ni kinigeria nigeria watunge cha kwao hola! sifuri. Movie nyingi ni za watu wanalia / wanashida/ vitu kama hivyo. sijaona movie ya mafanikio hata siku moja. inamaana sisi ni shida shida shida tuuuuuu. Gosh

    ReplyDelete
  14. JIANG UPO SAHIHI, KWANINI WANAPENDA MAJINA YA KIINGEREZA NA HAWAKIJUI HALAFU NDANI UNAKUTA USWAHILI UMEJAA

    KWANININ WASIITANGAZE ZAIDI LUGHA YETU???????????
    YAANI WANANIBOAAAAAA HADI NALIA

    ReplyDelete
  15. jamani LOVELY GAMBLE inatoka lini? Mlituambia December, na december ndo hii hapa inayoyoma, hamna kitu, kulikoni?

    ReplyDelete
  16. kuna bibie anataka kujua kwanini?
    filamu zetu zinamajina ya kingereza,
    JIBU LAKO: Tunajaribu kuzifanya ziwe za kimataifa katika kulenga soko la kimataifa,sijui kama unazo taarifa kuwa move za kinajeria zinateka soko japokuwa kingereza chao ni Broken lakini wanauza nje,katika masoko ya kienyeji na kutishia soko la kimataifa,inasemakana move za kinajeria zinakaribia soko la Bollywood(Indian Move).
    tunajaribu kuwapa nguyu akina kanumba.
    wadau
    FFU

    ReplyDelete
  17. Kanumba fanya kazi, wachana na critics waliofilisika hoja.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  18. Kanumba mi shabiki wako na ninakukubali sana tu. Kiinglish isiwe issue kwani hata huko maofisini wamejaa kibao na midigrii yao lakini umombo haupandi, achana nao. Kwa upande mwingine, mi naomba nikushauri kuhusu mavazi. Kiukweli sipendezwi na yale mavazi yako ya majoho majoho na mikofia dizaini, hazikutoi wangu. Achana na mavazi hayo, make yanakufanya uonekane mzee. Vaa kikawaida mtu wangu. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  19. sasa kama tunatarget soko la nje mbona humo ndani ni kiswahili, so huyo asiyejua kiswahili ananunua jina la muvi tu? maana ataelewa nini akiangalia wakati ndani ni kiswahili...kuweka majina ya kizungu haileti maana!
    M Net wanaonyesha muvi za kibongo, hizihizi za kina kanumba zikiwa na sub-titles, haki ya nani tena kama hujui kiswahili hutaielewa muvi as hizo sub-titles za kiingereza ni vitu vya ajabu...yani ni aibu...
    Kuwakopi wanaigeria kwenye film industry wala hatuendi mbele...tunatwanga maji kwenye kinu tu, maana wao wenyewe hawajamaster, sisi tukiiga ni uozo zaidi!

    ReplyDelete
  20. ww unayejiita ffu unaota mchanamchana,kiingereza cha nigeria sio broken kama unavyodai wewe,kiingereza chao kiko juu sana kuliko cha kwetu pili elewa kuwa kiingereza juu ya kasha uswahili ndani ya movie yenyewe havitasaidia kusonga mbele bali kurudi nyuma kwani huo ni wizi fulani

    ReplyDelete
  21. MIMI KUHUSU LUGHA SIONI TATIZO SANA HATA WAKITUMIA KIKURYA BADO POA TU.

    MOVIE ZA KIHINDI ZILIWEZA KUUTEKA ULIMWENGU WA FILAMU KWA KUTUMIA LUGHA YAO YA KIHINDI. NADHANI KITU CHA MSINGI NI HADITHI YENYEWE NA MAFUNZO YALIYOMO.

    HADITHI ZISIWE ZA KUIGA TAMADUNI NYINGINE ZA NJE ZIWE ZA KITANZANIA AU KIAFRIKA ZAIDI NA KUSINDIKIZWA NA MELODY NZURI NZURI.

    PICHA NYINGI ZA KIHINDI KWA MFANO WATU WAMEKUWA WAKIVUTIWA SANA, MBALI NA HADITHI YENYEWE, NA MUZIKI NA UCHEZAJI WAO.

    BIG UP! TARATIBU MTAFIKA.

    ReplyDelete
  22. Asante FFU kwa majibu yako, ila kumbuka na kuweka akilini kuwa kiingereza cha nigeria ni kizuri na kipo juu sema kinachokuchanganya wewe ni ile lafudhi yao lakini msamiati upo mahala pake; sasa utatekaje soko la kimataifa kwa lugha ya kiswahili ambayo haijaenea kokote?

    ReplyDelete
  23. yani mimi hapa ndo uwa nachoka kabisaaaaaa....

    lugha za ukoloni bwana???...aya

    filamu tunazipenda kanumba ila,ilo TATIZO la kiinglish ktk cover ilhali ndani kiswahili

    wapi na wapi!!!

    ReplyDelete
  24. weee annon apo juu

    umweke shekhe apo yani uwaigize waislamu,,unajitaka au???

    maana uo moto wake chezeya ni fulu maugomvi/visasi adi kiyama

    hhahahaaaaa

    ReplyDelete
  25. mie sikumuona huyo kanumba alivyoingia kny BIG BROTHER HOUSE...SOUTH AFRICA...ila kwa jinsi watu walivyokuwa wanaelezea mambo aliyoyafanya...nimebaki...nafuraha sana kila nikikumbuka vituko vyake nacheka sana....

    ilikuwa mwezi wa ramadhan,na yeye alikuwa amefunga!wenzake walipomuuliza kwa nini hali chakula.akajibu namnukuu...' AM CLOSING!!!!I WILL OPEN IN THE EVENING!!..(manake amefunga!atafungulia jioni)HAHHAHAHAHAHHAHAHAAHHAHAHAHAHHAHAHAHAHAHAHHAHAHAHHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHHAHAHAHHAHAHAHAHHAHAHAHAHHAHAHHHAHAHAH..yaani mwenzenu kila nikikumbuka nacheka sana HAHAHHAHHAHAHAHHAHAHAHAHHAHHAHAHAHAHHHAHAHAHHAHAHHAHAHAHHAHA!
    ney-bham.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...