Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa maji waliopo katika Mkutano wa mwaka wa utekelzaji wa programu ya maji vijijini unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumatatu katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha AICC jijini Arusha
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya akiwa na Mkurugenzi Muendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC Bwana Elishilia Kaaya(shoto) na maofisa wengine wakati akisindikizwa kuondoka katika kituo hicho baada kufungua rasmi Mkutano wa mwaka wa utekelezaji wa programu ya maji vijijini unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumatatu jijini Arusha.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji azindua mkutano wa Utekelezaji wa programu ya maji vijijijini

Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya amesema lengo la kitaifa kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ni asilimia 65 ifikapo mwaka 2010.

Amesema hilo ni lengo la Milenia ,lengo namba saba ambalo ni lengo la kidunia kwamba ifikapo mwaka 2015 idadi iwe imepungua kwa nusu.

Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya amesema hayo katika Mkutano wa siku mbili wa mwaka wa utekelezaji wa programu ya maji vijijini unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Desemba 14 na 15, 2009 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha AICC jijini Arusha.

Pia ameongeza kuwa tafsiri ya kitaifa ya lengo la milenia ni asilimia 74 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwaka 2015, na kwamba lengo kuu ni kwamba ifikapo mwaka 2020 kila mtanzania awe anaweza kupata maji safi katika umbali usiozidi mita 400 na iwe ni haki kwa Mtanzania kupata angalau lita 25 za maji kwa siku.

Amesema hadi kufikia mwaka 2008 asilimia 58.3 ya wananchi waishio vijijini waliweza kufikiwa na huduma ya maji na kuongeza kuwa juhudi za serikali katika kuyafikia malengo hayo zinafanyika katika utekelezaji wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. kaka michuzi tafadhali tupe habari kuhusu maziwa feki ya watoto yaliyokamatwa na tfda jamani mbona hawa wachina watuua

    ReplyDelete
  2. hongera prof mwandosya uko juu..

    ReplyDelete
  3. huyu waziri ilibidi awepo kule copen lakini nani anawakilisha mambo ya mabadiliko ya hewa nchi?

    au maji hayahusiki na climate change?

    kweli bado tupo kizani si ajabu ukakuta waziri wa miundo mbinu na jeshi ndhio kaenda copenhagen

    ReplyDelete
  4. porojo tu miaka nenda rudi tuna shughulikia maji vijijini

    tanzania ndo nchi yenye vyanzo vingi vya maji na vya kudumu kuliko nchi yoyote ile duniani
    kama lake victoria,nyansa,tanganyika na mito lukuki.
    angalieni ramani mjionee.
    lakini maji ni tatizo, je tungeishi jangwani ingekuwaje?

    ReplyDelete
  5. Mwandosya for president or Vice President? what is your next move? I don't understand what is going on for this PR stunt!?

    Lets wait and see.

    ReplyDelete
  6. mwakani huu mkutano ufanyike kwenye kijiji tena kile chenye shida ya maji

    ReplyDelete
  7. annon bennet umesema sawa...

    per diems izo

    ReplyDelete
  8. Nani mwakilishi wa wananchi kwenye mkutano huu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...