TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), leo ilimfikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mkuu wa idara ya Ulinzi katika Shule za St.Marys, kwa tuhuma za kudai rushwa ya Ngono.

Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Omari Kingwele, Mwanasheria kutoka katika Taasisi hiyo Sophia Gura, alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Eustace Mrefu mkazi wa jiji la Dar es salaam.

Akimsomea shitaka linalomkabili katika kesi hiyo, Gura alidai mahakamani hapo kuwa Mrefu alitenda kosa hilo Aprili 28, 2008 kwenye nyumba ya kulala wageni ya Chem Chem iliyoko maeneo ya Tabata Dar es salaam, ambapo anadaiwa kudai rushwa hiyo kwa Celina Peter.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kudai rushwa hiyo kwa msichana huyo, kwa kumhadaa kuwa angemtafutia kazi katika shule hizo au katika ofisi zingine, kwani msichana huyo alimuomba amsaidie kwa hilo.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo alirudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini wawili waliotakiwa kumdamini kwa kusahini hati ya dhamana yenye thamani ya Shilingi laki 5 kila mmoja.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januri 14 mwaka huu, itakapofika mahakamani hapo kwaajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Duu kesi hiyo imeahirishwa hadi January 14 mwaka huu...?, Mambo ya mwaka mpya...Good luck, GGMC

    ReplyDelete
  2. Sisi taka takukuru peleka hiyo fisadi ya Richmond pale mahakama. Hiyo mlinzi nataka ngono chapa fimbo tu namalisana nayeye!!

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa wa Tukukuru ni wajinga, wanaacha kushughulikia mafisadi wanaotaifisha nchi, wao wanfuatilia changu doa!!! to hell tukukuru

    ReplyDelete
  4. Mh! Ina maana watu wanaona hilo si kosa kubwa? Na haki kwa watu wanaonyimwa kazi au huduma fulani kwa kuwa hawajakubali hio kutoa hio rushwa ya ngono itatoka wapi?

    ReplyDelete
  5. Hawa takukuru wamwachie huyo mlinzi si walikubaliana wakapeana ngono sasa wao wanaingilia nini,ni aibu sana kwa chombo cha serikali kama hicho badala ya kushughulikia mambo muhimu kama RICHMOND kwa ajili ya maslai ya taifa wanaenda kukimbizana na walinzi kwenye magest.

    ReplyDelete
  6. Hivi watu mnajua maana ya kutaifisha kweli? Kutaifisha ni kufanya kitu kuwa mali ya taifa na si kujilimbikizia au kuiba mali ya taifa kama wengi tunavyofikiria.

    ReplyDelete
  7. HII KALI DU! BONGO KUNA MAMBO!

    SASA SIJUI HII KESI ITAENDESHWA JE.

    ANYWAY IS A VERY INTERESTING CASE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...