Wananjenje wakiwa na gwiji la muziki Mohamed Ilyas toka zenji kwenye mnuso usiku wa kuamkia leo. Mohamed Ilyas anayetumbuiza na kundi lake la Twinkling Stars kaiambia Globu ya Jamii kwamba hivi sana anaendesha shule ya muziki kwa wanawake huko Unguja na hivi sasa ana wanafunzi takriban 27 wanaojifunza kupiga ala mbalimbali na kuimba pamoja na kutunga mashairi
Mohamed Ilyas akipiga violin wakati kundi lake lilipotumbuiza
kwenye huo mnuso usiku wa kuamkia leo jijini Dar Mohamed Ilyas akipiga filimbi akiwa na wenzie. Mkongwe huyu ni mmojawapo wa magwiji wachache wa muziki waliosalia na inafaa kuwaenzi na kuwapa heshima inayostahili kwani wamebaki wachache mno kama lulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mohammed Ilyas gwiji la muziki nazifagilia sana nyimbo zake.

    ReplyDelete
  2. Ninampongeza Mzee Mohamed Ilyas kwa kanzi nzuri anayoifanya. Pia nimefurahi kuwaona Kitime, Babu Njenje na Juma Waziri-Kinyaunyau, Kachiri! Ninawasifu kwa kudumisha viwango vya kazi... Ila tunaamini jinsi mnavyozidi kuwa na busara mmeshaanza kuwandaa vijana wa kurithi mipini yenu na vipaaza sauti!

    ReplyDelete
  3. nimefurahi sana leo kutupa habari za mohd ilyas na ningependa ukatuwekea hata nyimbo zake kwenye galaxy music maana ni wapenzi wa hivyo vitu.

    ReplyDelete
  4. tunaomba utuweke hivyo vitu vya mohd ilyas kwenye mk galaxy hivyo ni vitu wadimu

    ReplyDelete
  5. hii ni namna ya kuwaenzi wazee wetu inapendeza sana! pia nilikuwa naomba kuuliza kama nina tatizo na nataka msaada kutoka kwa michuzi nafanyaje? jamani nimehangaika sana nisaidie ili niweze kuomba msaada. nashukuru in advance.

    ReplyDelete
  6. Nadhani suala sio kuwaenzi watu kwakuwa wamebaki wachache. Utamuenzi jambazi kwakuwa amebaki peke yake? Hoja ya msingi ni kuwaenzi wale wote ambao wana mchango wa kipekee katika jamii yetu. Huyu naye, kama mmojawapo wa watu wa aina hiyo basi anastahili. Huenda ningeshauri kuangalia ni akina nani hao ambao mchago wao, au vipaji vyao katika jamii yetu ni vya kipekee. Kisha basi, kuwaenzi, kuwatuza, na kuhifadhi kazi zao kwa ajili ya vizazi vijavyo

    ReplyDelete
  7. Vitu vya Mzee wetu Mohammed Ilyas unaweza ukavionja hapa ikisha ukaenda nunua sokoni.

    http://www.myspace.com/mohamedilyas

    Mdau Holland

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...