Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwa jimboni kwake leo ambako anatembelea kila kata kuwapongeza mabalozi kwa uchaguzi wa serikali ya vijiji na mitaa, ambako hamna chama cha upinzani kilichopata kiti hata kimoja na ni 100% CCM. Hapa ni kwenye kata ya lokisale.
Mh. Lowassa akiwasili kata ya Lokisale
Mh. Lowassa akisimikwa kata ya Lokisale na kiongozi wa wazee wa kimasai
mamia walijitokeza katika mkutano wa hadhara kupokea pongezi zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Huyo mzee wa mbele picha ya kwanza na ya pili anafanana sana na Mzee Ruben Kuney. I wonder kama ni yeye.

    Phatlorenzo-MN

    ReplyDelete
  2. Pongezi kwako Edo. Vuta subira lakini achana na Rostam wingu lake linachafua nyota yako mheshimiwa. 2015 tuko pamoja. 2010 usituvurugie mheshimiwa. Lakini 2015 u have our support.

    Phatlorenzo!! Sawa huyo ndiye mzee Kuney DC mstaafu wa Magu. Hao ni baadhi ya mtandao wa Edo.

    ReplyDelete
  3. vulalaaaaaa!
    2010 hiyo, kila mtu na mti wake.

    ReplyDelete
  4. mzee wa bunjuDecember 17, 2009

    kwa mila za kinyamwezi hapo lazma kungekuwa na kitendo cha kufupa lwanga( kumtemea mate ya baraka yaliyochanganyika na unga)sasa kwa ndugu zetu wamasai nadhani itakua ugolo( u can imagimne) ndo maana Mh. Edo kam unamawazo kwa kile kitakachotua mikononi mwake pude( rojo la ugolo) teheteheteh

    Mila zidumu

    Mzee wa bunju

    ReplyDelete
  5. Twazi penda mila zetu sn kuliko za wenzetu
    Tuzi tangaze milazetu duniani kote

    ReplyDelete
  6. NYOTA YA JAMAA NI KALI SANA WENYE NDOTO ZA KUTAKA KUMPOTEZA NI BORA WAKAFIKIRIA UPYA.

    HE IS GOING TO COME BACK FOR SURE!!

    ReplyDelete
  7. Mmmmh!! kumekucha, mwenye macho haambiwi ona.

    ReplyDelete
  8. BORA KUKOSA MALI LAKINI UWE NA FIKIRA MZURI. KWANI UNAWEZA KUTUMIA FIKIRA MZURI KUPATA MALI

    SASA KIBAYA ZAIDI UNAPOKUWA UNA FIKIRA MZURI UNAKUWA ZEZETA KABISA KWANI UNAKUWA HUNA UWEZO WA KUTAMBUA JEMA NA MBAYA.

    SIKU ZOTE UNAKUWA MSHIBIKI TU NA BENDERA FUATA UPEPO KWANI HUWEZI KUFIKIRIA MBALI ZAIDI YA UPEO WA MACHO YAKO.

    MAMBO YA USHABIKI WA SIMBA NA YANGA YA HATA YANGA IFUNGWE MABAO KUMI MARA KUMI NA SIMBA BADO NI SHABIKI WA YANGA DAMU DAMU YAMEPITWA NA WAKATI KATIKA DUNIA SASA.

    HAWA WANANCHI WANAJUA DHAMANI YA HELA ZILIZOPOTEA KWENYE DILI YA RICHMOND. JE NI SHULE, ZAHANATI, MADAWATI NK MANGAPI YANGEPATIKANA KWA HIZO FEDHA KUSAIDIA HAWA WANANCHI KUINUA MAISHA YAO?

    WATU WAFIKIRIE MAENDELEO ZAIDI.

    ReplyDelete
  9. Wa waaa Mr PRESIDENT TO be

    ReplyDelete
  10. EDO watanzania tunakukumbuka kwa uongozi makini na wenye misimamo. Ni wengi tunaokupenda Mr. president to be!

    Mdau Dange

    ReplyDelete
  11. ANON DEC 17, 02:30 NIMEKUSOMA.

    HIVI MATATIZO YA NCHI HII YAMEKWAMISHWA NA RICHMOND PEKEE AU UMEBEBA BANGO LA HISIA TU.

    USIMDHULUMU JAMAA.

    NAAMINI NI MAENDELEO ALIYOWAPELEKEA WATU WAKE NDIYO YANAFANYA WAMKUBALI.

    ReplyDelete
  12. there is no chance lowassa akawa president,hawa wapambe kijijini wanaosema wako pamoja na mwizi huyu na wengine wakidai mwizi huyu ni future president wanamatatizo ya kufikiri..ni bora akawa hapo hapo alipo jimboni kwake ili aseme na watu wa jimboni kwake na hao sidhani kama wana mihela mingi anayoweza kuwaibia..tena ana bahati sana kaiibia serikali ya tanzania ingekuwa ulaya angekuwa na kesi nzito ya kujibu pamoja na kufilisiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...