Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza leo uwanja wa Uhuru kusherehekea miaka 48 ya uhuru. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davies Mwamunyange
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza leo katika uwanja wa Uhuru kusherehekea miaka 48 ya uhuru.

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya uhuru yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar leo.

Amiri Jeshi Mkuu akipokea saluti maalumu baada ya kuwasili Uwanja wa Uhuru
Amiri Jeshi Mkuu akikagua gwaride la heshima kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru
Seehemu ya umma uliojitokeza kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru leo

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamedi Shein (kulia) akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika. Kushoto ni Jaji Mkuu Augustino Ramadhani.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), wakitoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza katika maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Ndere kutoka
Uganda wakitumbuiza wakati wa sherehe za Uhuru leo
Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii
na Freddy Maro wa Ikulu










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hongereni kwa sherehe. Hakika mmependeza. Lakini Tanganyika si ilinanihii? Au?!

    ReplyDelete
  2. Naona leo hamna ma-snipers wanaokaaga juu ya paa.

    ReplyDelete
  3. Uhuru kwa wote sawa, je matunda kwa wote kweli?

    Miaka 48 ya uhuru watanganyika walio wengi wamefaidi nini?

    ReplyDelete
  4. miaka 48, jembe la mkono,watoto wanakaa chini darasani, umeme mgawo, maji safi ndoto, rushwa ufisadi, list ni ndefu. bora tungewaacha wakoloni watusadie kungoza angalau kwa miaka 10 yaani uhuru ingekuwa 1971.

    ReplyDelete
  5. Mungu ibariki Tanganyika na Tanzania kwa ujumla

    ReplyDelete
  6. Nchi yetu inapofikisha miaka 48, ni wakati mzuri wa kukaa chini na kutafakari safari yetu - tulikotoka, tulipo na tunakoelekea; pamoja na changamoto zinazotukabili kama Watanzania hasa wakati huu tunapopita katika utandawazi mkali.

    Pengine ni wakati wa kutafakari maneno haya ya Rais Kennedy "Ask not what your country can do for you-ask what you can do for your country!".

    ReplyDelete
  7. duh likwaride hapo lilishika kasi na hiyo ngoma kutoka uganda yaelekea ilikuwa kali kweli hadi wanapaa lol sherehe zilifana hope jana kulikuwa hakuna mgao wa maji wala umeme

    ReplyDelete
  8. Inamaana Nchi yetu haina vikundi vya ngoma kutumbuiza, mpaka tuagize kutoka uganda??

    ReplyDelete
  9. hivi hao wanaosema madhambi ya Rais wetu JK angekuwa Nyerere Baba yetu wangesema au ndi sifa za kulazimisha tuu!jk ataendelea kuwa Rais wetu kwa kipindi chote kulingana na katiba na mwenye wivu ajinyonge,ila ukweli ni kwamba anajitahidi sana isipokuwa wachache wanamuangusha ila atafanikisha vizuri katika kipindi chake chote!!!
    Mungu mbariki Rais wetu JK!!!

    ReplyDelete
  10. DEC 09 6;20 am BIG UP.

    ReplyDelete
  11. Nimejaribu kuangalia zile picha za sherehe miaka hiyo ya 61 na picha za jana sijaona mabadiliko yoyote.

    ReplyDelete
  12. kila mtu anajifunza tokana na makosa nadhani Rais wetu ivi sasa ameshayaona mengi na atayafanyia kazi aliyofanya makubwa wenye lawama nadhani nyie mno upofu tuu hamuoni nyuma mlikotoka au mmeyasahau Rais kikwete ni wetu sote tumpe ushirikiano mzuri

    ReplyDelete
  13. MIAKA 48 BADO OMBA OMBA WA KUTUPWA HATA KUJITEGEMEA HATUWEZI NA RUSHWA KILA SIKU.NASEMA NI AFADHALI MKOLONI ANGEKUWEPO LABDA TUNGEENDELEA ZAIDI NA KUWA NA NIDHAMU BORA MAANA INAONEKANA BILA YA KUSUKUMWA SUKUMWA NA KUCHAPWA VIBOKO SISI WEUSI HATUZINDUKI.KILA KIONGOZI ANAJINUFAISHA MWENYEWE NA FAMILIA YAKE.LEO WANAOPATA UMEME NI 10% TU YA WATANZANIA WOTE(UNAOKATIKAKATIKA), BARABARA HAKUNA,KAZI ZA SHIDA NA ZA KUPEANA WENYEWE NA FAMILIA ZAO...MPAKA LINI? HALAFU VIONGOZI WANAPIGA TU KELELE MSIKATE MITI NCHI INAKUWA JANGWA....WATU WATAISHIJE? WAAFRIKA TUMELAANIWA!

    ReplyDelete
  14. Inaumiza moyo sana kuona namna gani tunafanya mambo kwa MAZOEA. Nionapo hizi picha sioni hata cha maana cha kusheherekea, si kwamba natamani mkoloni angeendelea hapana, swala ni kwamba ni kwa sababu zipi tunaendelea kusheherekea uhuru?

    Hivi unapewa nafasi ya kutoa hotuba kwenye siku kama hii unazungumza nini?! Bado unamtaja mkoloni miaka 48 baadae? Tuna nini cha kuonesha kwa vizazi vijavyo?

    ReplyDelete
  15. mwanaume jicho...mwamunyange!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...