mfadhili mkuu wa yanga Yusuf Manji (kulia) akiwa na aliyekuwa rais wa klabu hiyo ya jangwani Francis Kifukwe. Inasemekana Manji amejivua kuwa mfadhili wa yanga na pia amegoma kugombea nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi mkuu ujao. kwa upande wa ufadhili amesemekana kudai kuwa yanga sasa ni imara na yenye uwezo wa kujiendesha bila kutegemea mfadhili baada ya juhudi zake kuzaa uwezo huo, na kwa upande wa uenyekiti amesema hawezi kuwa na muda wa kufanya kazi za wadhifa huo kwani ana shughuli nyingi.
WAKATI HUO HUO YANGA INACHEZA NA SOFAPAKA YA KENYA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA TUSKER CUP NESHNO YA ZAMANI KATIKA MCHEZO UNAOTARAJIWA WA VUTA NIKUVUTE. KAMA KAWA GLOBU YA JAMII ITAKUWA MACHO KUWALETEA KINACHOJIRI. KAA CHONJO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Manji ningepata contacts zako, ungeona mbingu zote. Hujui unachokikosa, khalaghabao.

    ReplyDelete
  2. Huyu hakuwa na nia ya kuendeleza mpira tangu mwanzo...nia yake ilikuwa ni kushindana na Mengi na kujitafutia umaarufu...hana lolote.

    ReplyDelete
  3. nimeona comnt yako ntakupata vipi wapi

    ReplyDelete
  4. Kama kweli uko serious unataka kuona mbingu zote, utatafuta tu namna ya kunipata.

    Bahati mbaya siwezi mwaga contacts zangu hadharani vile naogopa hadi akina 'kajambanani' watanitafuta.

    Vinginevyo, wacha ukose bahati.

    ReplyDelete
  5. haki ya nani humu ndani kuna watu wamepinda ha ha haaa acha tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...