mfadhili mkuu wa yanga Yusuf Manji (kulia) akiwa na aliyekuwa rais wa klabu hiyo ya jangwani Francis Kifukwe. Inasemekana Manji amejivua kuwa mfadhili wa yanga na pia amegoma kugombea nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi mkuu ujao. kwa upande wa ufadhili amesemekana kudai kuwa yanga sasa ni imara na yenye uwezo wa kujiendesha bila kutegemea mfadhili baada ya juhudi zake kuzaa uwezo huo, na kwa upande wa uenyekiti amesema hawezi kuwa na muda wa kufanya kazi za wadhifa huo kwani ana shughuli nyingi.WAKATI HUO HUO YANGA INACHEZA NA SOFAPAKA YA KENYA KWENYE FAINALI YA KOMBE LA TUSKER CUP NESHNO YA ZAMANI KATIKA MCHEZO UNAOTARAJIWA WA VUTA NIKUVUTE. KAMA KAWA GLOBU YA JAMII ITAKUWA MACHO KUWALETEA KINACHOJIRI. KAA CHONJO.


Manji ningepata contacts zako, ungeona mbingu zote. Hujui unachokikosa, khalaghabao.
ReplyDeleteHuyu hakuwa na nia ya kuendeleza mpira tangu mwanzo...nia yake ilikuwa ni kushindana na Mengi na kujitafutia umaarufu...hana lolote.
ReplyDeletenimeona comnt yako ntakupata vipi wapi
ReplyDeleteKama kweli uko serious unataka kuona mbingu zote, utatafuta tu namna ya kunipata.
ReplyDeleteBahati mbaya siwezi mwaga contacts zangu hadharani vile naogopa hadi akina 'kajambanani' watanitafuta.
Vinginevyo, wacha ukose bahati.
haki ya nani humu ndani kuna watu wamepinda ha ha haaa acha tu
ReplyDelete