Kwako Issa michuzi

Naomba uniwasilishie ombi hili kwa wadau wabongom popote duniani.
Naomba kujua maneno ya kilingala yanayoimbwa katika wimbo wa kiongo ulioimbwa na Maquis du Zaire.
Wanasema ' nasengi yo nyoso bolingo ...............................mama.
sina ubaya na wewe samahani mama kiongo'

Hapo kwenye dash dash ndipo nataka kujua wanasema nini.

Mimi na bendi yetu ya muziki wa dansi hapa London tunataka kuanza kuuimba wimbo huu katika show zetu.

Msaada wenu ni muhimu sana kwetu.
Mdau Asa
London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. ndenge zali kosala na baneko nagai papaa

    ReplyDelete
  2. Nyie mnaotaka kuuimba huo wimbo mnayo haki miliki au mnataka kujiimbia tu kwa kujiona mnaweza kuimba? Au kwa kuwa mdau mmoja kafungwa? Mkiwaomba haki ya kuutumia hata huo mstari watawaelekeza unaimbwaje. Heshimuni jasho la watu jamani.

    ReplyDelete
  3. We ukiona vipi Tunga tu maneno yako ukipenda unaweza kuita Remix!!!

    ReplyDelete
  4. siufahamu wimbo huu lakini ni rahisi kupata maneno ya nyimbo za kikongo/kilingala kwa kusikiliza kipande hicho kwa kurudia rudia. kwa kuwa nia hasa ni kuburudisha (pengine sio kuelewa maana) ukisikiliza kwa kurudiarudia hapo sehemu huku ukiwa na kalamu na karatasi utayapata maneno au hata silabi zinazofanana ama kukaribiana. huwa nafanya hivyo nikiupenda wimbo wa kikongo, ingawaje mie sio mwanamuziki. kilingala kina silabi rahisi kama kiswahili tu. kwa wewe mwanamuziki hii itakuwa rahisi sana. 'mapapa likoloo' (mikono juu- sijui kweli au fix)

    ukitaka mistari ya double-double ya nyiboma nibonyeze tu.

    ReplyDelete
  5. Acha ujinga wewe, ukiona mambo hayaendi weka maneno yoyote ya kimatumbi, wataona sawa tu

    nyokoinyo

    ReplyDelete
  6. Nenda Club Afrique East London kuna wacongo wengi waliokuwa Bongo utapewa tasfsiri hapo hapo London Uingereza.

    ReplyDelete
  7. ..kuuliza si..hivi nini tofauti ya 'haki miliki' na 'hati miliki' (kama ipo..)

    ReplyDelete
  8. Kusema ukweli jamaa anahitaji msaada wenu, basi badala ya kuleta blah blah kwanini msimsaidie tu??

    ReplyDelete
  9. WASILIANA NA BENDI

    watafute kwenye net, ila huko london kweli huwezi kukutana na mzaire akakwambia ni nini

    or tafuta lyrics kama zimo online

    mbona unataka kupoteza muda wako, nedna kwenye baa zao ongea vizuri ulizia na labda watakupa na maneno yenyewe yanavyoandikwa na kurekebisha kama una kosa katika uliyaandika wewe hapa

    Or tafuta bendi

    Mambo haya yanaitaji skills ndugu yangu. develop your skills

    ReplyDelete
  10. Maneno ni haya;
    NASENGI YO NZOKA BOLINGO KAKE OBETI NGA LIMBISA MAMA

    ReplyDelete
  11. weee kipusa...weka maneno yako tuu hapo.... kama vile ... coco madimbaa bileku ya mpasii.oooooh...si inatisha unataka nini tena nikupe...niutmie email yako nikupe maneno ya kuweka hapo....

    ReplyDelete
  12. simpo! tafuta mkongo uk msikilizishe atakuambia hawa wanaozungumzia hati miliki blah blah wasikukatishe tamaa, tunaimba nyimbo kanisani zilizotungwa na watu wengine mbona hatuulizwi hati miliki rubbish kwani unatengenezea album si burudani tu?

    ReplyDelete
  13. kwa lazima muimbe wimbo huo tu,kama nyie ni wanamziki wa kweli si mngejituma kutunga nyimbo zenu,badala ya kuwa watumwa wa kuiga wakongo,huu ushamba ushamba utawaisha lini?mbona zipo nyimbo nyingi za kale za kiswahili kwa nini?msizitaangaze? kuliko huu ujinga mambo leo.Sasa huko London.Ukerewa nyie ndio mabalozi wa kongo au? ndio tawi la Maquiz.
    kama mabox ya kubeba yamekwisha rudi nyumbani

    ReplyDelete
  14. Heshimuni kazi za wenzenu. Kama hamuwezi tunga nyimbo zenu na mnataka kutumia za wenzenu, watafuteni hao maquiz du zaire, waombeni haki ya kutumia wimbo huo na watawapa mashairi yote. HILO TU NINAWAOMBA.
    Bwana Michuzi naomba tusifagilie wizi. Hii haijakaa sawa baba. Halafu hawa jamaa wapo mamtoni na wanajua kuwa huwezi tumia sanaa ya mtu bila ruksa yake.

    ReplyDelete
  15. wabongo bwana mkiulizwa hiki mna jibu hiki UJINGAA... jibu swali kama hujui nyamaza si UMUCH KNOW MWINGI kuleta blah blah tu. swaine!

    Papaa Stan
    Moshi. Tanzania

    ReplyDelete
  16. Aisee Malumbo habari za kazi?mimi sijambo na tegemea na wewe pia,naomba niwasadie Jamaa wa London wameomba msaada
    wa maneno (words) ya Kilingala katika Nyimbo ya KIONGO kupitia blog ya Michuzi,naomba uwakilishe msaada wangu kwao...

    Orch. Maquis du Zaire Nyimbo "KIONGO" neno ya Kilingala ni;

    NASENGI YO NZOKA BOLINGO KAKE OBETI NGA LIMBISA MAMA

    /Wako Maestro Vumbi Dekula

    ReplyDelete
  17. Mimi sijausikia huo wimbo ila maneno uliyotoa tafsiri yake ni kama ifuatavyo:
    NASENGI- NAOMBA
    NYOSO- YOTE
    BOLINGO-MAPENZI.
    natumaini itakusaidia.

    ReplyDelete
  18. kuiga iga mpaka lini. tunga maneno yenu. kwanza hizo haki miliki UK hakuna. nadhani haka kabendi kwishineni kabisa kama kanashindwa kutunga nyimbo.

    najua mnataka kuburudisha wabeba maboksi. lakini tungeni zenu. mnatia kinyau nyau humu

    ReplyDelete
  19. Kweli wabongo much Know....na ndo mana adi viongozi wetu wamejaa blah blah
    Mtu kauliza swali,kama una jibu msaidie kama hauna don't waste your time.

    ReplyDelete
  20. Bwana Michuzi,
    Asante sana kwa kunisaidia ku-post langu la kutaka kujua maneno yaliyoimbwa ktk wimbo huo wa kiongo. nawashukuru sana wadau wote waliochangia mawazo yao ya maana. hasa anony. 12.45 na anony01.54. sisi ktk bendi yetu tunaandika pia nyimbo zetu, na siyo kama anony's wengine walivyodhani. ila ktk fani lazima ujaribu kukubali na kuwaenzi wanamuziki wengine walioonyesha vipaji vyao katika sanaa fulani. na wana maquis ni mojawapo ya bendi zinazostaili kuenziwa. kiuandishi wa muziki na upangiliaji walikuwa moto wa kuotea mbali. sina mengi ila bendi yetu inaitwa 'THE GALAXY BAND' tunapiga kila Jumamosi WEST GREEN TAVERN- Tottenham na jumapili LIVE AND LET LIVE in Forest Gate.

    ReplyDelete
  21. kabla sijasoma wadau ebu nicheke
    hahahahahaaaaaa kwi kwi kwi hahaaa

    maana apa leo kazi wal'lai hii blogu idumu milele mchuzi unatupaga raha weweee??

    sasa uyu kawaza nini?hhaaaa

    ReplyDelete
  22. kaaazi kweli kweli...njaa izi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...