Kaka Habari za leo,
Naomba unisaidie kutoa tangazo kuna cheti cha Form Six kimeokotwa last week (Friday) cha MIRANDO RIDA AKINYI alisoma St. Anthony Secondary School amemalize 2006.
Anitafute kwa Namba 0713 25 26 77
Nitashukuru kwa msaada wako
Mdau
Naomba unisaidie kutoa tangazo kuna cheti cha Form Six kimeokotwa last week (Friday) cha MIRANDO RIDA AKINYI alisoma St. Anthony Secondary School amemalize 2006.
Anitafute kwa Namba 0713 25 26 77
Nitashukuru kwa msaada wako
Mdau
Umefanya jambo jema kabisa mdau. Nakupongeza kwa hilo!
ReplyDeleteHICHO NI CHAKO KITUMIE TU WALA USIWE NA SHAKA, HONGERA.
ReplyDeleteWatanzania tuwe na moyo huu, hasa VIBAKA na wezi wakubwa au wadogo na majambazi, I hope nao huwa wanasoma blogu ya jamii. Unapoiba au kuokota kitu cha maana kwa aliyepoteza na hakina maana yoyote kwako ni busara sana kukirudisha kwa namna yoyote ile ya siri au wazi. Kweli watu wanaiba au kuokota vyeti, ATM cards, vitambulisho, passport, nyaraka za kikazi na binafsi na hasa laptop zenye documents ambazo thamani yake ni zaidi ya ile laptop lakini wanaishia kuharibu au kuuza vinavyouzika kwa bei ya kutupa. Tuweni wastaarabu kama huyu jamaa ku-report kama umeokota au kuvitelekeza mahali pa wazi vile ulivyoiba lakini havina thamani wala maana kwako ila ni vya thamani sana kwa mwenyenavyo. Ikibidi wengine watakuwa tayari hata kuvilipia kwa sababu process ya kuvipata vingine ni ngumu na gharama sana. Sifundishi style mpya ya wizi kuiba vyeti na documents na kulazimisha wenyenavyo kuvilipia (style ya kidnapping) ili warudishiwe lakini nasema eleweni umuhimu na thamani ya vitu kama hivyo kwa waliopoteza na tafuteni namna salama za kuwarudishia. Ni suala la uungwana na ubinadamu tu.
ReplyDeleteMzee unachaji kiasi gani?
ReplyDeleteMungu akubariki ndugu yangu, sijawahi kuona jamani. Mimi niliadopt watoto wawili alokuwa ananisaidia kushughulia mambo ya pasi na nini wakati niko huku alitoka siku moja kwenda kuweka pesa bank ya Mnb kufika huko eti alisahau bahasha ya pasi za watoto hao kwenye kaunta hatua moja kurudi hakuzikuta, na kulikuwa hakuna pesa ni pass tu, tulitafta tukaweka matangazo nje ya bank hiyo kwani meneja alitukatalia kuweka matangazo ndani ya bank yake,. tulihaidi kutoa zawadi nono kwa mtu ambaye angeletupatia pass hizo but mpaka leo hakuna kitu mtu alozibeba au hata yule alozikota hataki kurudisha jamani. Watu wengine sijui wanatumwa tu kuharibu bahati za watu, mtu umekuta ni pass za watoto si unarudisha hata emagration unajifanya umeokota bahasha hiyo njiani jamani binadamu wengine jamani.
ReplyDeleteKWA USHAURI WANGU BLOG YA JAMII ITENGE KAJISEHEMU KA LOST AND FAUND,HAPO PEMBENI BADALA YA KUTAFUTA KWENYE KUMBUKUMBU,MDAU UBARIKIWE SANA HUO NDIO MOYO WATU HALISI WATANZANIA TOKA ENZI YA SHILINGI MIA CHAPA YAMMASAI.
ReplyDeleteI smell fishyyy!!! unalako jambo kama unataka kurudisha kirudishe baraza waliokitoa au shule aliyomaliza mkuu wa shule atajua cha kufanya. unless... unless... you are just looking for that particular individual for your own reasons. na vumbi lote la Dar I can't see anyone paying attention on a dusted piece of paper unless it looks like a dollar note.
ReplyDeletewatu wengine bwana mwenzao anatoa msaada wao wanaanza pumba zao ovyo sana hamkui?? hongera mdau god bless
ReplyDeleteMon Dec 14, 02:36:00 PM. You smell fishy kitu gani, labda huyo mtu hana mda wa kwenda baraza,akiweke kwenye bin?
ReplyDeleteHONGERA KWA MOYO HUO. KUWA NA HICHO CHETI HADI MWENYEWE AKUPIGIE SIMU. USIPELEKE BARAZA WALA POLIS. MFANO, RAFIKI YANGU ALIOKOTA POCHI INA $200.00 IKIWA NA CREDIT CARDS,VITAMBULISHO N.K KWENYE STORE. ALIULIZA WAHUSIKA WA STORE WAKASEMA WANAMFAHAMU MTU ALIYE POTEZA KWANI HUWA ANASHOP HAPA MARA KWA MARA. HAKUACHA POCHI STORE ALI ACHA NAMBA YA SIMU AKAWAAMBIA AKIJA MWAMBIENI ANIPIGIE NA MIMI NITAMKABIDHI.KWELI JAMAA AKAPOKEA SIMU IN 0NE DAY NA WAKAPANGA WAKUTANE AKAMKABIDHI.
ReplyDeleteKWA HIYO: UKIOKOTA KITU KAMA UNAMOYO WAKURUDISHA, PLEASE MAKE SURE UNAMKABIDHI MLENGWA NA SIO KUMPA POLIS AU BARAZA LA MITIHANI. TUWE NA MOYO HUU WABONGO.
Tuwe na moyo kama huo Jamani watanzania hakuna kitu kinakatisha tamaa kama kupoteza vyeti vya elimu ,ni moja ya kipindi kigumu sana waliopotelewa huwa wanapitia...
ReplyDeletejamani maneno mabovu si mahala pake hapa hivyo tubadilike pia.
kaka kama unaweza nenda baraza najua lazima huyo jamaa alitoa taarifa zaidi pale pia unaweza pata number zake kwa haraka zaidi.mungu akubariki sana ndugu....
Naamini Mungu atakubariki sana. Kwani ni wachache sana wenye moyo kama wa kwako. Na mijitu mingine sijui ina tabia za aina gani? Badala yakutoa mawazo mazuri, yanataoa pumba tu. Yawezekana Anony Monday Dec14 @ 2:53PM ni jambazi. Make mtu mwenye akili timamu huwezi kutoa wazo kama ili. Lakini Mungu atambariki hyu kaka ama dada. Wote tuwe na moyo kama huu.
ReplyDeleteNi mimi jamani asante sana,naomba uniletee nyumbani kwetu tafadhali naishi sinza karibu na mlimani city ukifika kituoni nitakuona,njoo kesho saa 5 asubuhi shukia kituo cha getini nitakuwa pale nakusubiri nitakuwa nimevaa min-skirt nyeusi na top ya kijani tafadhali jitahid sana...
ReplyDeleteJamani ulietoa tangazo Mungu akubariki saana achana na hao wabeba mabox wanaokukatisha tamaa hawajui kwa hilo ulilofanya Mungu anakufungulia milango ya mafanikio. Mimi nimewahi kuokota vitu vya thamani saana natafuta documents yenye mawasiliano namtafuta mtu na anakuja kupokea mzigo wake na siku zoote wananiombea kuwa mungu akubariki na kweli imenisaidia saana,siku moja nilipoteza vyeti vyangu vyoote originals nilikuwa naenda kutoa copy nikasahau katika daladala maeneo ya magomeni na hapo vilikuwa vinahitajika ubalozi wa marekani baada ya siku mbili,nilichanganyikiwa mtu binti aliyeviokota alitaka kuvitupa mjombake akafungua bahasha akakuta ni vyeti akasema huyu mtu atakuwa analia na kweli nilichanganyikiwa nikaona mwisho wa ndoto zangu umekwisha, alichukua licence yangu ya nursing inapicha wakaipeleka gazeti la Alasiri ikapigwa picha na kubandikwa ukurasa wa mbele kuwa dada huyu kapoteza nyaraka zake za muhimu afike ofisi ya alasiri apewe mawasiliano na mtu aliyeviokota, nilifurahi saana nakaamini wale watu niliokuwa nikiokota documents zao nakuwatafuta na kuwapa maombi yao yamefanya kazi. Hivyo wewe uliyetoa tangazo hili Mungu atakujibu kwa njia nyingine na maisha yako yatakuwa na mafanikio. Ubarikiwe saana
ReplyDeleteSawa matangazo kama hayo ya mtu kupoteza kitu ni mazuri sana kwa nchi zilizoendelea,lakin nchi kama TZ ukikuta huyo mtu aliyepoteza hicho cheti alipoteza na kiasi kikubwa cha hela au ni albino ambaye alipotea kabisa,mzee lazima uisaidie polisi na TZ ukiambiwa unaisaidia polisi utaona rangi zote.Sawa utajitetea uliokota lakin mpaka ije kueleweka umeokota kweli kijasho kitakutoka practically ndio iko hivyo.Ndio maana watu wengi wanaokota vitu lakin wanapata woga wa kujitangaza na kuanika namba zao za simu.
ReplyDeleteSIKU HIZI CHETI HICHO KITAMSAIDIA NINI? HUYO JAMAA NAMFAHAMU YUKO HAPA KIWANJA MWAKA HUU KAMALIZA FIRST DEGREE NEXT YEAR ANAANZA MASTERS SI DHANI KAMA ATAKIITAJI SANA
ReplyDeleteANKAL, KWA NINI WATU WANAOTOA PUMBA USIWATIE KAPUNI? AU HUWA HUSOMI MAONI KABLA YA KUPOST. HAWA JAMAA WANAO ONGEA PUMBA WEKA KAPUNI NA WAPE NAFASI WANAO CHANGIA HOJA ZA MSINGI. TENDA WEMA NENDA ZAKO, KWAMBA MUNGU KAFANYA VYETI VYAKO VIPATIKANE KWA AJILI ULIRUDISHA VYA WATU, THAT'S NOT TRUE. IT IS COINCIDENCE. UKIOKOTA TENDA WEMA THEN KEEP ON MOVING.
ReplyDelete