



Taasisi ya Mikopo ya Easy Finance, imetoa mchango wa Shilingi Milioni 12.5 kukisaidia Chama cha Soka cha Zanzibar, ZFA, kufanikisha mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kurindima huko Zanzibar hivi karibuni.
Hafla fupi ya makabidhiano, imefanyika jana mjini Zanzibar ambapo Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Juma Shamhuna alipokea hundi hiyo kwa niaba ya ZFA, na kuipongeza Easy Finance kufafadhili Kombe la Mapinduzi, pia alitoa wito kwa wafadhili wengi zaidi kuzidi kujitokeza kufadhili michezo visiwani humo.
Akikabidhi hundi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Easy Finance, Isaack Kasanga, amesema Easy Finance, imetoa mchango huo kwa ZFA, ili kuonyesha inathamini juhudi za ZFA, kuboresha mchezo wa soka Visiwani Zanzibar.
Bwana Kasanga amesema pia mchango huo ni namna ya kurudisha fadhila kwa jamii wa Wazanzibari kwa jinsi wanavyoiunga mkono taasisi ya Easy Finance ambayo inalo tawi wisiwani Zanzibar.
Hii ni mara ya pili kwa Easy Finance kufadhili michezo Zanzibar ambapo mara ya kwanza, ilitoa ufadhili wa shilling milioni 5 katikati ya mwaka huu.
Easy Finance, ni taasisi ya mikopo inayotoa mikopo ndani ya muda mfupi na masharti rahisi, ina makao makuu mjini Dar es Salaam na matawi Zanzibar , Mwanza na Mbeya litafunguliwa hivi karibuni
...his name is Mahmoud (rather than Mohamed) Thabit Kombo, unless he has changed it in the last few days.
ReplyDeleteKama pesa hizi zingekuwa zinasaidia elimu ingekuwa kitu kizuri sana.Shule nyingi hazina madawati wakati tunasika makampuni yanatoa mamilioni kwenye soka.
ReplyDeleteZENJI RAHA SANA,UKIWA NA 5000 POUND UNAKUTANA NA MAWAZIRI NA MAKAMERA,HEBU JULY NIENDE NA MIMI NIKASAIDIE JAPO SHULE SIO.
ReplyDeleteJamani safari moja huzaa nyengine, hapa jamaa wanaanzia tu na si km hawajui kwamba zanzibar tuna uhaba wa vitendea kazi kwa idara ya elimu, nawapongenza kwa mchango wenu ili kukuza mashindano yetu ili kuyaenzi Mapinduzi.....
ReplyDeleteJunior Hyderabad.
Jamani huu ukumbi gani yaani huyu waziri was nini sijui amelowana na jasho utafikiri hapo ni Gym. A/C ipo wapi?
ReplyDeleteJamani why mtu anaenda kukutana na Waziri, tena ktk shughuli za kikazi, halafu anavaa T-shirt? Na huyu naibu waziri vp? au walikuwa ktk sports day ya Easy finance? maana nisije nikawa nashangaa kumbe ni sports day
ReplyDeleteHuyo ni Mahmoud Thabit Kombo tuliyesoma nae Arusha School au? lazima nirudi bongo [Tambararez].
ReplyDeleteJamani kule kwetu visiwani, kiongozi huwa karibu na wananchi so we respect them as normal person si unaona hta naibu waziri hana suti? Hakuna kujikweza kule sote ni maskini ww vp? Kuhusu kurowa jasho naibu waziri hamjui km hakuna umeme kule kwa siku kadhaa.
ReplyDeleteJunior Hyderabad.
Huyu bwana anatoa mchango, angevaa hata kaptula ni sawa tu, anayepokea mchango ndio lazima aje amevaa suti, kuheshimu shughuli..... ni jeuri ya pesa
ReplyDeleteMbona nilisikia Zanzibar wamegundua mafuta na wameanza kuyachimba imekuaje tena?
ReplyDelete