Shule ya Msingi Rwamlimi iliyopo Musoma Mjini inasikitika kutangaza kifo cha Mwalimu mwenzao Mwl Dalphone Lameck kilichotokea katika hospitali ya Bugando leo tarehe 28/12/09.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Rwamlimi –Musoma. Marehemu ameacha Mke na watoto.

Marehemu Mwl Lameck katika uhai wake alishika nyadhifa tofauti hasa ualimu mkuu katika shule zifuatazo za msingi Nyakato, Nyasho, Rwamlimi zilizopo Musoma Mjini.

Habari ziwafikie ndugu wa marehemu popote pale walipo,Walimu wote waliowahi kufundisha nae ,wanafunzi wote waliofundishwa nae wakatika wa uhai wake,Majirani na marafiki wote pale Rwamlimi Musoma bila kuwa sahau washiri wote wa kanisa la wasabato Rwamlimi na Nyakato

Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
-Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. RIP Mwl Lameck Etunga, tunakukumbuka sana, hasa kwa utunzi wako mahiri wa nyimbo pamoja na ngojera!

    Umetutoka kimwili lkn kiroho huko pamoja nasi!

    frm Germany

    ReplyDelete
  2. Tutamkumbuka sana hasa katika fani yake ya kiswahili.Pia wanafunzi waliofundishwa nae,wekeni majina.

    ReplyDelete
  3. Bwana alitoa na Bwana ametwaa,ulale kwa amani Mwl.Lameck

    Nakukumbuka sana,hasa ulipo kuwa mwl.mkuu shule ya msingi nyakato mwaka 1991,nami nikiwa mmoja wa wanafunzi wako wa darasa la saba,ukiwa na mwl.Karugila wa somo la hisabati na marehemu somo la english.

    POLEENI WOTE MLIOGUSWA NA MSIBA HUU,NA MUNGU ATAWATIA NGUVU NA UVUMILIVU.

    MAGESA,CJ TANGA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...