Baada ya kutokuwepo mjini kwa muda wa siku chache, niliporudi tu nikatua ktk Blogu ya Jamii ya ankal ili kujua mambo yameendaje mjini. Nilistaajabika kukutana na story ambayo mimi nilikuwa na taswira zinazoelezea hali halisi.

hii ni story ya twiga wa Arusha national park kutokuwa na sehemu ya mwisho ya mkiani ambayo huwa na manyoya. Juu ni taswira za twiga amba tulibahatika kukutana nae ndani ya Arusha park akiwa hana sehemu ya mwisho ya mkia wake.
------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi za dhati kwa tembeatz.blogspot.com kwa kuendeleza libeneke, mlengo ukiwa kuonesha taswira ya mandhari nzuri za nchi yetu hii iliyobarikiwa. Kwa kweli libeneke hilo ni mfano wa kuigwa kwani kunahitajika aina mbali mbali ya globu ili mambo yawe mswano kwenye kila nyanja.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hivi ni kweli hawa Twiga hawana hivyo vishina vya mkia au Watu wamesha kwinshehi?? Mi nadhani kuna biashara haramu inaendelea hapo na wahusika lazima watakuwa watu wa karibu yani kuanzia askari wanayama pori!! Please wizara ianze kuwajibika msitufanye sisi karaga bao!!

    ReplyDelete
  2. Jibu la kitafiti ni kwamba, predator mkubwa wa twiga ni simba. Arusha National Park kwa sasa hivi hamna simba. mara ya mwisho kuonekana simba ni mwaka 1998. Ila kuna fisi (spotted hyena) au Crocuta crocuta kwa lugha ya kitaalam. Hawa sasa ndo wamekuwa top predator kwenye food chain. Tofauti na simba ambao wana mbinu maalum ya kumuua Twiga, mathalani kumnyemelea mnyama na kisha kumkamata kiunoni, na bila kuchelewa kuhamia shingoni ili kuziba pumzi mpaka mnyama afe. Fisi yeye mbinu hizo hana, yeye anafukuza tu na kuuma popote pale hadi mnyama atakapo kosa nguvu kwa kuchoka ua kupoteza damu nyingi. Kwa hili naamini kabisa itakuwa ni fisi alimvamia akiwa mdogo...akakata huo mkia.. kisha huyo twiga akafanikiwa kukimbia wakati fisi anaendelea kupata hiyo finyango.....

    ReplyDelete
  3. Twiga huyu anapendeza sana kumwangalia,lakini cha ajabu kuna njemba zina mpigia mahesabu ya ngozi yake,hata soko zinalijua lilipo,cha ajabu ni watu ambao wala huwezi kuwadhania kama wanafanya huo uharamia.Tubadirike jamani shughuri zipo nyingi tu si lazima uangamize kizazi cha wanyama ili uishi vizuri.Kama wewe ni mmoja wao au unamjua anayeua wanyama kiharamia kuwa mzalendo na MUNGU akubariki.

    ReplyDelete
  4. lifisi ni limnyama lisilo na mvuto hata kidogo kwa nini wasikamatwe wapelekwe serengeti? kule kuna simba wa kufa mtu weeeengi watapata hiyo mizoga kwa wingi kuliko kuwaacha waendelee kuharibu hawa mamiss twiga wanaaribia urembo wao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...