

















Kuwa mwanamitindo si kujua kupanda jukwaani na kufanya catwalk tu bali uwanamitindo ni pamoja na kujua mambo mengi kama kujiamini, kutambua wewe ni nani, unaweza kuwa nani, kutambua kuwa unaweza kuleta mabadiliko katika jamii na nchi yako kwa ujumla, unaweza kushika hatamu ya maisha yako na kutambua ni uamuzi wako kutokupata ukimwi.
Hivi karibuni washiriki wa Kisura wa Tanzania 2009 walipewa jaribio kubwa sana la kupiga picha na nyoka uku wakiwa wamevalia nguo nadhifu za mbunifu maarufu hapa nchini, Fatuma Amor.
Zoezi ili lilikuwa ni gumu sana kwa visura wengi lakini kwa ajili ya uelewa wao, kujiamini kwao na ujasiri wao waliweza kupiga picha kama wanamitindo wa kimataifa wakiwa na bonge la chatu.
Shindalo hili la Kisura wa Tanzania 2009 limedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambapo visura 19 wapo kambini kwa sasa.
Shindalo hili la Kisura wa Tanzania 2009 limedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambapo visura 19 wapo kambini kwa sasa.
Siku ya Jumapili, Novemba 29 Visura wote waliwekwa kwenye Ukanda wa hatari ili kuwapa fursa ya watazamaji wa TBC1 na watanzania wote kwa ujumla kupata nafasi ya kuchagua visura 10 tu ambao wanatakiwa kuingia kwenya fainali.
Kumpigia kura mshiriki unayempenda aingie kwenye top 10 andika neno Kisura acha nafasi halafu andika namba ya mshiriki kama zinavyoonekana mbele ya jina la kila mmoja wao, halafu tuma kwenda namba 15771.
Mshindi wa Kisura wa Tanzania 2009 anategemewa kutangazwa tarehe 18 Decemba pale kwenye hoteli ya kitalii Movenpick.
Wadhamini wengine wa shindano la Kisura wa Tanzania 2009 ni Kiromo View Hotel, Family Health International (FHI), TBC1, Air Tanzania, Mwananchi Communication, Clouds FM, Hugo Doming, Mercy G Beauty Parlour na EM Entertainment.
Wadhamini wengine wa shindano la Kisura wa Tanzania 2009 ni Kiromo View Hotel, Family Health International (FHI), TBC1, Air Tanzania, Mwananchi Communication, Clouds FM, Hugo Doming, Mercy G Beauty Parlour na EM Entertainment.
Beautiful Tanzanie Agency (BTA)
Hata kwa dawa.....acha tu na uwo uMiss Africa!!! yaani sitaweza kulala hata kidogo baada ya kumshika huyo nyoka.
ReplyDeleteheeeeeeeee
ReplyDeleteyani uhatarishe moyo wako kwa BP kisa izi pesa?wakitoka apo wamepata saikolojiko problem ao lazima wataweweseka jaman vibinti ivi
me ningeacha kabisa apo apo ayo mashindano
No.11 NI BOMBA
ReplyDeleteagh sasa hilo joka ndio litasaidia nn,mambo mengine bana...
ReplyDeletenonsense......
Mambo ya Nigeria tena?Wazuri lakini wanatisha na nyoka wao...kamwe siwawezi
ReplyDeleteshukuruni Mungu hilo ni joka la kibisa otherwise mngelijua jiji lol!
ReplyDeleteNONE OF THEM, WASTE OF MONEY AND TIME.
ReplyDeletewaz dis na manyoka nyoka tena...
ReplyDeleteTo hell!!!!! picha zenyewe siwezi angalia sembuse kushika, kazi kweli kweli, watashika na visivyoshikika lol!!!!
ReplyDeleteUwiiiih!!!nimeogopa kumuona huyo nyoka jamani bila shaka mkitoka hapo bp 199 poleni sana.Real!no.03 yuko makini nimemkubali
ReplyDeleteEee simadogo !!!
ReplyDeletemamodo wa ukweli i mean wenye kujua pozi za kimodo ni no 17 na 11 tu.
ReplyDeletefashion gani hiyo ya warembo kucheza na nyoka? wala hata haipendezi ndo kuongezea urembo au? vipo vitu vingi vya tanzania waweza kucheza navyo kuliko hicho.
ReplyDeletemimi nataka kujua atakayeshinda atapata contract ya aina gani. Au ataishia bongo na dili zisizokuwa na maendeleo
ReplyDeleteSafi sana kama American next top model, wafanyieni majaribio mengine kama kutangaza TV commercials,kupiga picha sehemu ngumu kama kwenye miti n.k kuwa waandishi wa habari, kuigiza wakapiga picha wakiparua samaki feri na bado picha inaonekana bomba na kubakii kisura katika hali zote. kisura lazima awe na sifa nzuri na nzito sio kujua kutembea tu
ReplyDeletemichuzi fanya ondoa hii post, mimi sijaangalia mtu hapo nilifumba macho na kuscroll down.
ReplyDeletesio issue
jamani mbona tuko nyuma sana katika picha, mapozi na mazingira? aise inatisha..hadi leo tuko katika hali hii? mamodo bado kabisa...
ReplyDeleteila namba 17 nimemkubali sana..pozi limetulia, urembo unaaminika na style imekaa vizuri.
Tujifunze kwa wenzetu jamani!
sasa mbona werembo wote woke kwenye style moja ya joka? then wamejiremba kama wachawi usoni! kweri ni mambo ya Nageria, warembo ni wazuri ila kupiga na nyoka sijaona
ReplyDeletekila mtu abuni style yake aipendae sizani kama wote wanapenda nyoka wengine roho zinadunda pale
Excuse me, but what are they posing with a python (Chatu)??? Ruins all the pics for me!!!! I don't think its our culture to worship snakes, we used to kill them when we saw them.
ReplyDeletemuadaaji na mpiga picha ameona nyoka ndio scene itakuwa kivutio kwa hao mamiss....poor creativity.
ReplyDeleteMademu wote washamba tu...mie namwona Mwajabu tu hapo..# 11...sneak peek pajaz...mmmmwah!
ReplyDeletepicha ya kiusuper model ni no. 17 violet hongera dada.
ReplyDeleteudhalilishaji tu, kushika nyoka na urembo kuna uhusiano gani? hiyo inaonyesha kuna mengi dada zetu huwa wanpitia katika kufikia malengo yao ya umodo
ReplyDeletenaona sasa tunaiga American next top model, ila sio mbaya hata UK na Canada nao waliiga, big up Tyra. Ila kusema ukweli sis bado sana tena sana tu kufika kule. Idea ni nzuri, ila make up no and big no yani bado, afu hizo pozi tofauti na mazingira na nguo na kila kitu, yani haziendani. Huyo chatu sio real but hey somehow have to act like it. Ila hapo yani picha inasema vingine, na mamodo wako mile hamsini kwingine, kazi kweli kweli
ReplyDeletemichuzi hii blog yako sasa inaelekea kubaya. wengine tukiona hilo dude presha inafikia dangerous zone. hapa nipo maktaba nimeruka na kupiga kelele wazungu wote waliokuwa karibu yangu imebidi walale mbele wakidhani nimeona bomu. wafanyakazi wa library wote wameacha kazi zao wamenijalilia huku wakiwa wameshapiga simu police na fire department baada ya kuona wazungu wanabanana milangoni kisa kelele zangu. imebidi niwaonyeshe hii picha na kuwaomba radhi kwa usumbufu nimewaambia huwa naweweseka nikiona chatu. bwana uangaliage vitu vya kutuwekea vinginevyo blog itanishinda mimi. nitashukuru kama utakuwa umenielewa.
ReplyDeleteWako mdau, UK.
Usimchezee chatuu, oooooh chatu eeh
ReplyDeletefimbo usimtumpie eeeeh, utaukosa ushindiiii!!
natoa onyo kwa yeyote yule anayemchezea chatu...ni hatari!, atakuja adhirika asipate lolote la manufaa...
na hatari imkuteee bila ya kutegemea, atakuja adhirika ajute na duniaaaaaa!! usimchezeee chatuuu...ohoo chatu eeh, fimbo usimtupie utaukosa ushindii..x2
kaka unakumbuka mwimbo huo lakini??
Anyway nilitaka kusema kuwa ama kweli chatu si mchezo, hebu angalia sura za hao mabinti woote hakuna hata mmoja ambaye ame-potray sura yake halisi!! wote wamekunja sura kuonyesha wanajikaza haswa kulibeba hilo joka. ni kama walilazimishwa vile. mh joka limewafanya wote waonekane polygons facewise ha ha ha!!
kaka, southside, NY.
Jamani sio ushamba.ila nchi nyingi sasa hasa america na nchi nyingine za ulaya ndo naona wamekuwa na style hii.Ila labda tuseme tusifate sana utamaduni wa nje.msemakweli ni mpenzi wa Mola,mie sikubali kupiga nao hata kwa dola ngapi mwee!!!
ReplyDeletekweli yako anony hapo juu,no 17 na 11 wana pozi la kimodo,watiliwe maanani vipaji vyao viendelezwe.
ReplyDeletemambo mengine bwana nyoka wa nini saa ndio wanaleta sura halisi ya tanzania au?badala ya kuangalia visura unabaki kuangalia minyoka wabuni kitu kingine sio nyoka bwana kitu cha hatari hata kama ni nyoka wa kibisa lakini bado wanatisha haileti maana
ReplyDeleteNumber 13 amenichekesha na posi lake. Aliogopa kumshika ikabidi amuwekee kiuno tu LOL!!!!!
ReplyDeletelabda quality ya camera lakini picha zote sioni mtu aliyetoka vizuri. Labda number 17.
Huyo nyoka tu ndio kawin kwa kweli
kaka michuzi jman mimi mpka nimeshindwa kula huku mambo gani hayo sasa kushikishwa joka hilo ina maana waandaaji hawakauona means nyingine?wamewatesa tu wabint wawatu.
ReplyDeletewasichana wote wazuri hapo ila huyo no 17 amekaa kimodo hasa..and she`s very fotogenik..anavutia
acheni kujishaua kwani eti mnafumba macho mkiona mijoka,zamani mlivyokua mnaenda kibisa je PALE MAGOMENI? nyoo kila siku kukosoa tu jaribu kucreate idea zako sio lawama na kasoro
ReplyDeletekiukweli no 17 ndio supermodel