alinda: Namba 14
diana: Namba 15
gladys: Namba 10
glory: Namba 8
hasnat: Namba 13
jackies: Namba 6
jackline: Namba 19
lightness L: Namba 7
lightness M: Namba 16
lucky: Namba 5
Mary J: Namba 12
mary M: Namba 9
mwajabu: Namba 11
mwatatu: Namba 2
reson: Namba 18
shamim: Namba 3
sharon: Namba 4
violet: Namba 17
zahra: Namba 1

KISURA WA TANZANIA 2009

Kuwa mwanamitindo si kujua kupanda jukwaani na kufanya catwalk tu bali uwanamitindo ni pamoja na kujua mambo mengi kama kujiamini, kutambua wewe ni nani, unaweza kuwa nani, kutambua kuwa unaweza kuleta mabadiliko katika jamii na nchi yako kwa ujumla, unaweza kushika hatamu ya maisha yako na kutambua ni uamuzi wako kutokupata ukimwi.

Hivi karibuni washiriki wa Kisura wa Tanzania 2009 walipewa jaribio kubwa sana la kupiga picha na nyoka uku wakiwa wamevalia nguo nadhifu za mbunifu maarufu hapa nchini, Fatuma Amor.
Zoezi ili lilikuwa ni gumu sana kwa visura wengi lakini kwa ajili ya uelewa wao, kujiamini kwao na ujasiri wao waliweza kupiga picha kama wanamitindo wa kimataifa wakiwa na bonge la chatu.

Shindalo hili la Kisura wa Tanzania 2009 limedhaminiwa na Serengeti Breweries Limited ambapo visura 19 wapo kambini kwa sasa.
Siku ya Jumapili, Novemba 29 Visura wote waliwekwa kwenye Ukanda wa hatari ili kuwapa fursa ya watazamaji wa TBC1 na watanzania wote kwa ujumla kupata nafasi ya kuchagua visura 10 tu ambao wanatakiwa kuingia kwenya fainali.
Kumpigia kura mshiriki unayempenda aingie kwenye top 10 andika neno Kisura acha nafasi halafu andika namba ya mshiriki kama zinavyoonekana mbele ya jina la kila mmoja wao, halafu tuma kwenda namba 15771.
Mshindi wa Kisura wa Tanzania 2009 anategemewa kutangazwa tarehe 18 Decemba pale kwenye hoteli ya kitalii Movenpick.

Wadhamini wengine wa shindano la Kisura wa Tanzania 2009 ni Kiromo View Hotel, Family Health International (FHI), TBC1, Air Tanzania, Mwananchi Communication, Clouds FM, Hugo Doming, Mercy G Beauty Parlour na EM Entertainment.
Beautiful Tanzanie Agency (BTA)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Hata kwa dawa.....acha tu na uwo uMiss Africa!!! yaani sitaweza kulala hata kidogo baada ya kumshika huyo nyoka.

    ReplyDelete
  2. heeeeeeeee

    yani uhatarishe moyo wako kwa BP kisa izi pesa?wakitoka apo wamepata saikolojiko problem ao lazima wataweweseka jaman vibinti ivi

    me ningeacha kabisa apo apo ayo mashindano

    ReplyDelete
  3. No.11 NI BOMBA

    ReplyDelete
  4. agh sasa hilo joka ndio litasaidia nn,mambo mengine bana...
    nonsense......

    ReplyDelete
  5. Mambo ya Nigeria tena?Wazuri lakini wanatisha na nyoka wao...kamwe siwawezi

    ReplyDelete
  6. shukuruni Mungu hilo ni joka la kibisa otherwise mngelijua jiji lol!

    ReplyDelete
  7. NONE OF THEM, WASTE OF MONEY AND TIME.

    ReplyDelete
  8. waz dis na manyoka nyoka tena...

    ReplyDelete
  9. To hell!!!!! picha zenyewe siwezi angalia sembuse kushika, kazi kweli kweli, watashika na visivyoshikika lol!!!!

    ReplyDelete
  10. Uwiiiih!!!nimeogopa kumuona huyo nyoka jamani bila shaka mkitoka hapo bp 199 poleni sana.Real!no.03 yuko makini nimemkubali

    ReplyDelete
  11. Eee simadogo !!!

    ReplyDelete
  12. mamodo wa ukweli i mean wenye kujua pozi za kimodo ni no 17 na 11 tu.

    ReplyDelete
  13. fashion gani hiyo ya warembo kucheza na nyoka? wala hata haipendezi ndo kuongezea urembo au? vipo vitu vingi vya tanzania waweza kucheza navyo kuliko hicho.

    ReplyDelete
  14. mimi nataka kujua atakayeshinda atapata contract ya aina gani. Au ataishia bongo na dili zisizokuwa na maendeleo

    ReplyDelete
  15. Safi sana kama American next top model, wafanyieni majaribio mengine kama kutangaza TV commercials,kupiga picha sehemu ngumu kama kwenye miti n.k kuwa waandishi wa habari, kuigiza wakapiga picha wakiparua samaki feri na bado picha inaonekana bomba na kubakii kisura katika hali zote. kisura lazima awe na sifa nzuri na nzito sio kujua kutembea tu

    ReplyDelete
  16. michuzi fanya ondoa hii post, mimi sijaangalia mtu hapo nilifumba macho na kuscroll down.

    sio issue

    ReplyDelete
  17. jamani mbona tuko nyuma sana katika picha, mapozi na mazingira? aise inatisha..hadi leo tuko katika hali hii? mamodo bado kabisa...
    ila namba 17 nimemkubali sana..pozi limetulia, urembo unaaminika na style imekaa vizuri.

    Tujifunze kwa wenzetu jamani!

    ReplyDelete
  18. sasa mbona werembo wote woke kwenye style moja ya joka? then wamejiremba kama wachawi usoni! kweri ni mambo ya Nageria, warembo ni wazuri ila kupiga na nyoka sijaona
    kila mtu abuni style yake aipendae sizani kama wote wanapenda nyoka wengine roho zinadunda pale

    ReplyDelete
  19. Excuse me, but what are they posing with a python (Chatu)??? Ruins all the pics for me!!!! I don't think its our culture to worship snakes, we used to kill them when we saw them.

    ReplyDelete
  20. muadaaji na mpiga picha ameona nyoka ndio scene itakuwa kivutio kwa hao mamiss....poor creativity.

    ReplyDelete
  21. Mademu wote washamba tu...mie namwona Mwajabu tu hapo..# 11...sneak peek pajaz...mmmmwah!

    ReplyDelete
  22. picha ya kiusuper model ni no. 17 violet hongera dada.

    ReplyDelete
  23. udhalilishaji tu, kushika nyoka na urembo kuna uhusiano gani? hiyo inaonyesha kuna mengi dada zetu huwa wanpitia katika kufikia malengo yao ya umodo

    ReplyDelete
  24. naona sasa tunaiga American next top model, ila sio mbaya hata UK na Canada nao waliiga, big up Tyra. Ila kusema ukweli sis bado sana tena sana tu kufika kule. Idea ni nzuri, ila make up no and big no yani bado, afu hizo pozi tofauti na mazingira na nguo na kila kitu, yani haziendani. Huyo chatu sio real but hey somehow have to act like it. Ila hapo yani picha inasema vingine, na mamodo wako mile hamsini kwingine, kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  25. michuzi hii blog yako sasa inaelekea kubaya. wengine tukiona hilo dude presha inafikia dangerous zone. hapa nipo maktaba nimeruka na kupiga kelele wazungu wote waliokuwa karibu yangu imebidi walale mbele wakidhani nimeona bomu. wafanyakazi wa library wote wameacha kazi zao wamenijalilia huku wakiwa wameshapiga simu police na fire department baada ya kuona wazungu wanabanana milangoni kisa kelele zangu. imebidi niwaonyeshe hii picha na kuwaomba radhi kwa usumbufu nimewaambia huwa naweweseka nikiona chatu. bwana uangaliage vitu vya kutuwekea vinginevyo blog itanishinda mimi. nitashukuru kama utakuwa umenielewa.
    Wako mdau, UK.

    ReplyDelete
  26. Usimchezee chatuu, oooooh chatu eeh
    fimbo usimtumpie eeeeh, utaukosa ushindiiii!!
    natoa onyo kwa yeyote yule anayemchezea chatu...ni hatari!, atakuja adhirika asipate lolote la manufaa...
    na hatari imkuteee bila ya kutegemea, atakuja adhirika ajute na duniaaaaaa!! usimchezeee chatuuu...ohoo chatu eeh, fimbo usimtupie utaukosa ushindii..x2
    kaka unakumbuka mwimbo huo lakini??
    Anyway nilitaka kusema kuwa ama kweli chatu si mchezo, hebu angalia sura za hao mabinti woote hakuna hata mmoja ambaye ame-potray sura yake halisi!! wote wamekunja sura kuonyesha wanajikaza haswa kulibeba hilo joka. ni kama walilazimishwa vile. mh joka limewafanya wote waonekane polygons facewise ha ha ha!!
    kaka, southside, NY.

    ReplyDelete
  27. Jamani sio ushamba.ila nchi nyingi sasa hasa america na nchi nyingine za ulaya ndo naona wamekuwa na style hii.Ila labda tuseme tusifate sana utamaduni wa nje.msemakweli ni mpenzi wa Mola,mie sikubali kupiga nao hata kwa dola ngapi mwee!!!

    ReplyDelete
  28. kweli yako anony hapo juu,no 17 na 11 wana pozi la kimodo,watiliwe maanani vipaji vyao viendelezwe.

    ReplyDelete
  29. mambo mengine bwana nyoka wa nini saa ndio wanaleta sura halisi ya tanzania au?badala ya kuangalia visura unabaki kuangalia minyoka wabuni kitu kingine sio nyoka bwana kitu cha hatari hata kama ni nyoka wa kibisa lakini bado wanatisha haileti maana

    ReplyDelete
  30. Number 13 amenichekesha na posi lake. Aliogopa kumshika ikabidi amuwekee kiuno tu LOL!!!!!

    labda quality ya camera lakini picha zote sioni mtu aliyetoka vizuri. Labda number 17.

    Huyo nyoka tu ndio kawin kwa kweli

    ReplyDelete
  31. kaka michuzi jman mimi mpka nimeshindwa kula huku mambo gani hayo sasa kushikishwa joka hilo ina maana waandaaji hawakauona means nyingine?wamewatesa tu wabint wawatu.
    wasichana wote wazuri hapo ila huyo no 17 amekaa kimodo hasa..and she`s very fotogenik..anavutia

    ReplyDelete
  32. acheni kujishaua kwani eti mnafumba macho mkiona mijoka,zamani mlivyokua mnaenda kibisa je PALE MAGOMENI? nyoo kila siku kukosoa tu jaribu kucreate idea zako sio lawama na kasoro

    kiukweli no 17 ndio supermodel

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...